Biashara za kiafrika zinakufa mmiliki anapofariki

geofreyngaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2014
Posts
658
Reaction score
946
Biashara nyingi za kiafrika zinakufa pale baba anapoaga dunia sababu kubwa ni baba kutomshirikisha mama pamoja na watoto katika uendeshaji wa biashara tofauti na makabila kama wahindi, lebanuni, Israeli etc. Baadhi ya sababu ya wanaume kufanya hivyo ni kwamba wanawake sio waaminifu wanaiba na kujenga kwao na watoto nao ukiwashirikisha wanaweza kukuibia.

Kweli kabisa haya mambo yanatokea lakini kwanini iwe kwa watanzania mbona kwa wenzetu mambo tofauti japo yanatokea?
Naamini wengi wetu tuna washirikisha wake zetu na watoto kwenye biashara katika stage ya mwisho, nayo ni matumizi. Kwahiyo mama na mtoto hawajui ugumu na mbinu thabiti za utafutaji pesa ila wanachojua ni kutumia tu na sio vinginevyo.

kwa msingi huu mama na mtoto hawapati picha halisi ya biashara na kama wangeshirikishwa kila mmoja kwa level yake naamin mambo yangekua tofauti na ilivyo sasa.
Je, kuna maoni au mchango tofauti ili tuweze kulinda biashara zetu pindi tutakapotangulia mbele za haki?
 
Kwanza kabisa sisi biashara zetu hatuzi-formalize. tunaenda tu ilimradi. hata ikifikia unataka kuomba mkopo kwenye taasisi za fedha unaanza kuhangaika kutengeneze mahesabu matokeo yake unalipa hela nyingin kugharimia mkopo ambao hujaupata.

Nikirudi kwenye mada, ni kweli biashara zetu nyingi ni sole proprietorships na promoters ndo huendesha biashara hiyo. Survival ya business kama hizo hutegemea sana na fitness ya promoter ambaye aweza kuwa mama au baba. ikitokea baba mgonjwa, biashara inafungwa, ikitokea amepata dharura hata ya kwenda kuwaona tanesco inabidi afunge.
Ushauri ni kwamba,

1. Kama unachofanya ni kizuri basi mfundishe na mwanao na mkeo ili na yeye akupige tafu wakati unapokuwa huwezi. after all hawa ndo watu wa karibu na wewe

2. usiwajengee tabia ya kuona kama kuwaweka dukani au kwenye ofisi yako ni kuwanyanyasa. unawasaidia na wenyewe kujua.

3. chukua biashara yako kama legacy utakayoacha kwa familia yako utakapo ondoka maana na uweke miiko ya nini hawapaswi kufanya na nini wanapaswa kufanya.

4. Rasimisha biashara yako kwa kusajili kampuni na hao watoto na mama wawe ni shareholders. na uwaambie kwamba mkiua hii biashara mnamaliza investment yenu wenyewe na mnajiua wenyewe

5. Tunza kumbukumbu vizuri na andaa mahesabu vizuri kila baada ya kipindi fulani ili ijulikane.

Kumbuka, kama promoter wa biashara unatakiwa kuweka misingi sahihi ili kila anaekuja baada ya hapo azingatie hivyo vitu
 
Failing to plan is planning to fail!!!!

Hatujipangi na successors wetu, kuhodhi power, control, access, benefits, authority over our resources na kama hayo ndio yanatufelisha weusi wengi sana!!!
 
Tatizo kubwa ni namna ya wafanyabiashara wafanyavyo biashara zao. Biashara nyingi azifanywi kimahesabu, wengi hawajui wamepata profit au loss kiasi gani katika mwezi. Pia mfumo mzima wa wizi na ufisadi umepelekea mpaka baba kutomwamini mke na hata watoto. Umefungua duka umemweka mke mkisaidiana kuendesha biashara punde unasikia mke wako ana viwanja na pengine utagundua pia kajenga kisirisiri.
 
yaani mkuu umeandika yote ambayo yalikkuwa moyoni mwangu niliyotaka kuandika asante sana kwa wazo hili be blessed
 
ni kweli mkuu ulichonena kuna baadhi ya watu ninaowafahamu wake zao wamekuwa na uwizi pindi mzee anaposafiri yeye huchukua ile fedha ya duka au biashara na kufanya mambo wayatakayo na mwishoe wa siku kinakuwa kimemnukia

hujidanganya na kudhani biashara ni ya mzee peke yake na kumbe ni yao wao wote inashangaza sana
 

Una busara sana, laiti kama!!!!
 
Wanawake ukiwa kabidhi biashara wataiba sana kuna siku nilikwenda kwa mama mdogo maili moja kibaha akanituma nikamuwekee kama milioni moja benki walikuwa na duka la hardware nilivyorudi nikaweka risiti mezani baba mdogo alivyorudi akaikuta risiti akaniuliza hii ya nini nikamjibu nimetumwa kumbe anaficha hela kwenda kuangalia kuna milioni 16 wakaitoa zote lawama zikahamia kwangu sikurudi tena mpaka leo
 
watu huogopa kuwashirikisha wanawake mambo ya kibiashara kwasababu wengi wao n wezi na hukimbilia kuua waume zao ili wazimiliki wao.
 

Ha ha haaaaaa uliangukiwa na jumba bovu
 
hahahahhaaaaa mkuu malizia hapo hiyo sentensi bhana haaaa.

Ha haaaaa weeeeee ngoja niishie hapo mamii, nafsi itaniponza bureeee!!!

Ally Kiba anajisemea "ulichokikimbia umekipoteza na ulichokikimbilia hujakipata"!!!!!!
Yaani we jua.. .. laiti kamaaa!!!!!
 
mama yangu yule hela alikuwa anaficha baada ya kutoa wakanunua kigari kipya ila ni muda mrefu kweli

Aaaargh mkuu bila we kuwa na roho ya uwazi kama ulivyofanya mbona mzee ilikuwa ni kama imekula kwake pakubwaa!!!!
 
Aaaargh mkuu bila we kuwa na roho ya uwazi kama ulivyofanya mbona mzee ilikuwa ni kama imekula kwake pakubwaa!!!!

mzee mwenyewe alikuwa wa kichaga tena mtoto wao wa pili walimuharibu kwa ajili ya mambo yao baadaye akafariki inasikitisha kwa kweli
 
my dia mbona unaniambia kimafumbo kiasi hicho jamani
unashindwa niini kuniambia nami nikaelewa bestito

ujue unanichanganya mwenzio babito? hebu weka wazi basi
achana na hizo songi za fumbo fumbo
Ha haaaaa weeeeee ngoja niishie hapo mamii, nafsi itaniponza bureeee!!!

Ally Kiba anajisemea "ulichokikimbia umekipoteza na ulichokikimbilia hujakipata"!!!!!!
Yaani we jua.. .. laiti kamaaa!!!!!
 
Mnanikumbusha my ex,nilipompa wazo la biashara alinisapoti na kusema "bebi una akili kama yahudi".Siku ilipofika namwambia atafute m 2,mie natoa 4,utata ukaanza,akawa anaponda kweli wazo la kumiliki biashara yoyote ile."Uyahudi" wangu ukaisha.

Nikapiga dili mwenyewe na washkaji chini kwa chini,hakujua tena.

Kuna matatizo ya kucentralize mambo yote mikononi mwako mwenyewe hasa biashara inapokuwa kubwa,unakuwa limited kukua zaidi.

Ninachofanya ni kushirikisha watu walio tayari kushare,wanatoa hela au nguvu kazi tunawekeana hesabu,nakuwa selective kwa aina ya biashara ambazo ni rahisi kuziendesha kwa mfumo huo wa hesabu,mf badala ya kuendelea kukuza duka kubwa la reja reja au kufungua maduka ya reja reja mengi,naweza kuanzisha biashara ya jumla na kuwapa wenye maduka wengine mzigo,wanalipia kidogo,halafu nyingine wanarudisha taratibu,tunashirikiana hivyo,unapunguza risk yako kwa kushare capital na labour kwa kutumia wengine.

Wafanya biz wengi bongo na duniani huenda hivyo,inabidi tu uwe social kuintergrate na watu wa aina yako kwenye jamii.

Chances za kufanikiwa ukiwa na watu wengine wenye imani yako ni kubwa kuliko kushirikisha ndugu ambaye huenda hana hiyo imani yako ila analazimika tu kwa kuwa ni ndugu yako na anataka pesa pia.Atakusumbua sana.

Puzzle kufanya biz na watu baki ni uaminifu,hiyo ni risk pia,ila unaweza kuiminimize kwa kumshirikisha mtaji,iwe ni pesa au nguvu kazi.

Nakumbuka jamaa yangu fulani alikuwa na cafe ya bakhresa,akaniambia chumba kapanga yeye,cafe ni kama yake,na hata vibali ni vyake,isipokuwa mzigo wote mle ndani ni wa Azam,anarudisha kidogo kidogo kila akiuza,anatoa chake,kinachobakia anampelekea mwenyewe.

No wonder Bakhresa yuko kama alivyo hivi sasa!

The same applies to Sony,Samsung,etc!

Otherwise kama huwezi hayo,ni bora ubaki na biashara ndogo unayoweza kuimiliki mwenyewe na kupata hicho kidogo,kuliko kuendelea kufanya uwekezaji ambao hauwezi kuusimamia,huko ni kutupa hela,bora uzifanyie mambo mengine,especially kwetu sie tulioajiriwa huku tukiwa na biz,zinapotanuka huwa ni shida kweli,kila unayemweka anapiga hela,yaani ni heri umwambie mtu akupe hesabu ya wastani,ugawane nae faida na expenses,kuliko utake faida yote wewe na kumlipa mshahara,huku expenses zote ukibeba wewe,bongo hii,utaumia.

Kubali tu faida ndogo isiyo na expenses wala risk,akiiba anajiibia mwenyewe,akiwa na akili atanufaika,atafungua kwake,atakuacha kwa amani huku mkishirikiana,unatafuta mwingine,tena wanaambizana,"ukifanya pale unatoka, mzee mstaarabu sana, ana utu yule", hiyo tayari ni biashara yenye uhakika wa faida ya kila siku na nguvukazi isiyoisha,na jina zuri kwenye jamii na hata ukifa, kama umerecruit mtu kuwa katika nafasi yako,ukaformalize biz yako na kumpa nguvu ya umiliki kisheria,hatopata shida kuiendeleza,kwa vile inaendeshwa na watu wengi,haitegemei saana creativity ya marehemu,bali creativity ya pamoja ya wadau wengi,wenye maslahi nayo pia.
 

hya matatizo unaweza kuyadhibiti kabla ya ndoa kabla ya kuoa\kuolewa hakikisha mwezako anakuwa partner WA kweli maishani na cyo kitandani peke yake
 
Ni kweli kabisa wakuu wanawake wanaweza kuiba ktk biashara zetu, ila ni vema tujiulize kwa nn wanaiba katika biashara ambayo nao ni wamiliki wa moja kwa moja?
Nadhani ni kwasababu zifuatazo;

1)kwanza ndoa zetu nyingi zimejengwa kwenye mausiano magumashi

2)mfumo dume

3)hatuko na wake zetu mara kwa mara katika hili wahindi wako vzur kinoma(out wanatoka baba, mama na watoto) hii inasaidia kujenga upendo, kuaminiana, kujuana, ushirikiano, amani, hatimaye familia yenye nguvu ikifika stage hii ni vigumu kwa member of the family kwenda kinyume na mipango ya familia hiyo.

4)kukosekana kwa Hiyo juu kunamfanya mwanamke kutokua na amani na uhakika ndani ya famili na kujihisi hana nafasi katka mali wanazochuma na mwema wake. Matokeo yake anaiba, baga ningekua mm ningeiba.
Mnaonaje wadau?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…