geofreyngaga
JF-Expert Member
- Sep 7, 2014
- 658
- 946
Biashara nyingi za kiafrika zinakufa pale baba anapoaga dunia sababu kubwa ni baba kutomshirikisha mama pamoja na watoto katika uendeshaji wa biashara tofauti na makabila kama wahindi, lebanuni, Israeli etc. Baadhi ya sababu ya wanaume kufanya hivyo ni kwamba wanawake sio waaminifu wanaiba na kujenga kwao na watoto nao ukiwashirikisha wanaweza kukuibia.
Kweli kabisa haya mambo yanatokea lakini kwanini iwe kwa watanzania mbona kwa wenzetu mambo tofauti japo yanatokea?
Naamini wengi wetu tuna washirikisha wake zetu na watoto kwenye biashara katika stage ya mwisho, nayo ni matumizi. Kwahiyo mama na mtoto hawajui ugumu na mbinu thabiti za utafutaji pesa ila wanachojua ni kutumia tu na sio vinginevyo.
kwa msingi huu mama na mtoto hawapati picha halisi ya biashara na kama wangeshirikishwa kila mmoja kwa level yake naamin mambo yangekua tofauti na ilivyo sasa.
Je, kuna maoni au mchango tofauti ili tuweze kulinda biashara zetu pindi tutakapotangulia mbele za haki?