Biashara za kiafrika zinakufa mmiliki anapofariki

Mahusiano ya kifamilia yasiyo thabiti yanasababisha hii hali.Kukosa mipango katika biashara.

Ila kwa upande mwingine ni uzembe wetu sisi wenyewe wanawake,unakuta bajeti ndogo tu ya nyumbani ya chakula inakushinda unakuta unaifanyia ufisadi hii inapelekea mwanaume kutokuwa na imani na mkewe.

Pili mwanamke kutokuwa na hamu ya kujifunza,au hata kujua tu mume wake anafanya kazi gani na ni wapi,yeye huridhika tu ile hali ya kuletewa,hii hupelekea kwa mwanaume kuona ni sawa tu hamna haja ya kufahamishwa chochote.
 
Biashara nyingi za kiafrika zinakufa pale baba anapoaga dunia sababu kubwa ni baba kutomshirikisha mama pamoja na watoto katika uendeshaji wa biashara tofauti na makabila kama wahindi, lebanuni, Israeli etc. Baadhi ya sababu ya wanaume kufanya hivyo ni kwamba wanawake sio waaminifu wanaiba na kujenga kwao na watoto nao ukiwashirikisha wanaweza kukuibia.

Kweli kabisa haya mambo yanatokea lakini kwanini iwe kwa watanzania mbona kwa wenzetu mambo tofauti japo yanatokea?
Naamini wengi wetu tuna washirikisha wake zetu na watoto kwenye biashara katika stage ya mwisho, nayo ni matumizi. Kwahiyo mama na mtoto hawajui ugumu na mbinu thabiti za utafutaji pesa ila wanachojua ni kutumia tu na sio vinginevyo.

kwa msingi huu mama na mtoto hawapati picha halisi ya biashara na kama wangeshirikishwa kila mmoja kwa level yake naamin mambo yangekua tofauti na ilivyo sasa.
Je, kuna maoni au mchango tofauti ili tuweze kulinda biashara zetu pindi tutakapotangulia mbele za haki?
Nakuunha mkono kabisa mdau.
ila wanawake wa Kichagga mume akifa biashara mara nyingi inasimama kama kawaida. Kwa sababu mara nyingi anakuwa anatafuta yeye na mume wake
 
Ni kweli kabisa wakuu wanawake wanaweza kuiba ktk biashara zetu, ila ni vema tujiulize kwa nn wanaiba katika biashara ambayo nao ni wamiliki wa moja kwa moja?
Nadhani ni kwasababu zifuatazo;
1)kwanza ndoa zetu nyingi zimejengwa kwenye mausiano magumashi
2)mfumo dume
3)hatuko na wake zetu mara kwa mara katika hili wahindi wako vzur kinoma(out wanatoka baba, mama na watoto) hii inasaidia kujenga upendo, kuaminiana, kujuana, ushirikiano, amani, hatimaye familia yenye nguvu ikifika stage hii ni vigumu kwa member of the family kwenda kinyume na mipango ya familia hiyo.
4)kukosekana kwa Hiyo juu kunamfanya mwanamke kutokua na amani na uhakika ndani ya famili na kujihisi hana nafasi katka mali wanazochuma na mwema wake. Matokeo yake anaiba, baga ningekua mm ningeiba.
Mnaonaje wadau?

dah! mkuu wahindi nao wanalizana ile mbaya kwenye biashara na mali kwa ujumla. mi nishashuhudia kesi zaidi ya tatu ambapo kaka anawazidi "akili" wanafamilia wengine ukijumlisha na mama!
 
my dia mbona unaniambia kimafumbo kiasi hicho jamani
unashindwa niini kuniambia nami nikaelewa bestito

ujue unanichanganya mwenzio babito? hebu weka wazi basi
achana na hizo songi za fumbo fumbo
Atiiii? Aiseee nanihii ............. hebu njoo huku nimekukamatia laivuuuuu!
 
Ktk mahusiano ambayo mwanamke hana uhakika wa ndoa yake na wala hana uhakika na Mali wanazochuma wote ni rahisi kushawishika kuiba japo wapo lkn wachache wanohakikishiwa Kila kitu na bado ataiba.
 
Mahusiano ya kifamilia yasiyo thabiti yanasababisha hii hali.Kukosa mipango katika biashara.

Ila kwa upande mwingine ni uzembe wetu sisi wenyewe wanawake,unakuta bajeti ndogo tu ya nyumbani ya chakula inakushinda unakuta unaifanyia ufisadi hii inapelekea mwanaume kutokuwa na imani na mkewe.

Pili mwanamke kutokuwa na hamu ya kujifunza,au hata kujua tu mume wake anafanya kazi gani na ni wapi,yeye huridhika tu ile hali ya kuletewa,hii hupelekea kwa mwanaume kuona ni sawa tu hamna haja ya kufahamishwa chochote.

This is very positive post nimeiona kwenye huu izi.. Nakuunga mkono asilimia zote. Uaminifu unaanzia nyumbani, kama mkeo anajua humuheshimu na anajua we ni mzee wa michepuko lazima akuibie sababu hana guarantee na ndoa yenu. Anajua lolote linaweza tokea..

Ila kama kuanzia katika ngazi ya familia mnaishi vizuri, mnapendana na kuheshimiana na mkeo na watoto hakika hutaweza kuibiwa na biashara yako itaacha matunda mazuri kwako na vizazi vyako..
 
my dia mbona unaniambia kimafumbo kiasi hicho jamani
unashindwa niini kuniambia nami nikaelewa bestito

ujue unanichanganya mwenzio babito? hebu weka wazi basi
achana na hizo songi za fumbo fumbo

Ngoja watu wapungue ntakuuma sikio!!!!
 
Mahusiano ya kifamilia yasiyo thabiti yanasababisha hii hali.Kukosa mipango katika biashara.

Ila kwa upande mwingine ni uzembe wetu sisi wenyewe wanawake,unakuta bajeti ndogo tu ya nyumbani ya chakula inakushinda unakuta unaifanyia ufisadi hii inapelekea mwanaume kutokuwa na imani na mkewe.

Pili mwanamke kutokuwa na hamu ya kujifunza,au hata kujua tu mume wake anafanya kazi gani na ni wapi,yeye huridhika tu ile hali ya kuletewa,hii hupelekea kwa mwanaume kuona ni sawa tu hamna haja ya kufahamishwa chochote.

Daaaanh, hivi mlikuwaga wapi nyie watu wenye vichwa changamfu kiasi hiki???!!!!
 
This is very positive post nimeiona kwenye huu izi.. Nakuunga mkono asilimia zote. Uaminifu unaanzia nyumbani, kama mkeo anajua humuheshimu na anajua we ni mzee wa michepuko lazima akuibie sababu hana guarantee na ndoa yenu. Anajua lolote linaweza tokea..

Ila kama kuanzia katika ngazi ya familia mnaishi vizuri, mnapendana na kuheshimiana na mkeo na watoto hakika hutaweza kuibiwa na biashara yako itaacha matunda mazuri kwako na vizazi vyako..

Lolote kama lipi mtu kashaolewa na watoto wako ndani???!!

Hata ikiwa ni kuachana fungu likiwa kubwa si ndio mgao unaongezeka kuliko kuiba ili mtaji ukate, mtagawana chaga za kitanda au??!!

Guarantee ya ndoa inapatikana kwa juhudi za pamoja sio za ku wish bali kutenda watu wameachia wanawake makusanyo lakini ukimstukiza ghafla akupe maelezo anaishia kulia na kudai "mume wake mkali na hamuamini" lakini ukimuuliza nguo zilizoko kabatini hata akitoka usingizini anakumbuka mpaka bei, siku aliponunua na alienda saa ngapi alivaa nini na hata aliowakuta dukani that day!!!

Mkuu mapenzi, heshima, nunua dhahabu mpaka awe kama sonara kama mvivu atakuwa mvivu tu na kama ni mdokozi hali kadhalika; tatizo kuna familia hazitaki kuwaachia watoto wa kike wakishaolewa, ukipata mama mkwe wa hivyo tu kwisha kaazi!!!! Yaani hata akiambiwa mtoto wake anaenda shopping ya mashuka basi jioni atapiga simu kuulizia rangi na ukubwa wa mashuka husika!!! Hawa wamama ndio tabu sana katika jamii
 
Kwa uzoefu wangu wanawake wengi wa kiafrika ni kama wanadhani jukumu la kutafuta hela za familia ni la baba hata wakishirikishwa wanakosa umakini ni kama kumlazimisha punda kunywa maji

Pia wanawake walio wengi hawana uhusiano mzuri na wateja yaani wengi ni wepesi wa hasira au kukosa kujiamini na hivyo kuharibu biashara. Mimi nadhani kuwashirikisha watoto ni nzuri zaidi zaidi
 
Yaani ukiona nyumbani kwa dada tu mkali mkali ukimsogeza kwenye biashara watendaji na wateja wanakukimbia!!!
 
Lolote kama lipi mtu kashaolewa na watoto wako ndani???!!

Hata ikiwa ni kuachana fungu likiwa kubwa si ndio mgao unaongezeka kuliko kuiba ili mtaji ukate, mtagawana chaga za kitanda au??!!

Guarantee ya ndoa inapatikana kwa juhudi za pamoja sio za ku wish bali kutenda watu wameachia wanawake makusanyo lakini ukimstukiza ghafla akupe maelezo anaishia kulia na kudai "mume wake mkali na hamuamini" lakini ukimuuliza nguo zilizoko kabatini hata akitoka usingizini anakumbuka mpaka bei, siku aliponunua na alienda saa ngapi alivaa nini na hata aliowakuta dukani that day!!!

Mkuu mapenzi, heshima, nunua dhahabu mpaka awe kama sonara kama mvivu atakuwa mvivu tu na kama ni mdokozi hali kadhalika; tatizo kuna familia hazitaki kuwaachia watoto wa kike wakishaolewa, ukipata mama mkwe wa hivyo tu kwisha kaazi!!!! Yaani hata akiambiwa mtoto wake anaenda shopping ya mashuka basi jioni atapiga simu kuulizia rangi na ukubwa wa mashuka husika!!! Hawa wamama ndio tabu sana katika jamii

You can say it again.Mama wakwe hawa siku hizi nao vimeo sana ingawa si wote
 
Mkuu nimekuelewa vyema lakini hata wewe hukunisoma vizuri.. Anyway kama unajua mkeo ni tutusa kwanini ulimwoa?? Na kama ulijua mkiwa tayari ndani ya ndoa hapo naunga mkono usimshitikishe acha akae nyumbani tu japo si vema pia kuwa na mwanamke asiyechakalika
 
Mkuu kama sikukuelewa nieleweshe tu niko tayari sana kujifunza!!!
Sio suala la ututusa ila unaweza kuta ni good cook very nice mom to kids, engaging and all that lakini haya hayakuzi kipato sasa unapoamua kumuingiza kwa business say, ndio unakuta hayo sasa tunayozungumzia yaaani aweza kuwa sooo weak if not almost useless upande huo achilia mbali hao wadokozi!!

Maadamu ushamuoa na mengine anafanya basi unaishi kwa mapungufu yenu ila ndio ukiitika wito mkubwa basi all the efforts sums to zero!!!!
 
Back
Top Bottom