Biashara zangu zimegeuzwa kuwa za ukoo

Biashara zangu zimegeuzwa kuwa za ukoo

Piga stop hao wafanyakazi wako ndugu yeyote akija hapo hakuna kutoa chochote hadi wakukute wewe mwenyewe bila hivyo pole sana
 
Haupo serious mkuu..hao ndugu uliwatambulisha na kuwaaminisha kuwa zipo ndo maana wanazifuata.Kama biashara ulianzisha mwenyewe usiposimama na kuwa thabiti utaizika mwenyewe ...
Haswaaa. Piga marufuku ndugu yoyote kwenda kuchukua pesa kinyemela. Tena marufuku kubwa, wanune wasinune watajua wenyewe.
Wakiwa na shida wapitie kwako, la si hivyo aatamega hiyo biashara mpaka ife. Na ikifa hao hao ndio watakunyooshea vidole
 
Nasimamia mimi na mzazi wangu wa kike ikitokea pesa zimetoka unakuta kachukua dada sina la kufanya ndio maana naomba ushauri
Kaka unakuwa mnyonge sanaaaa. Badilisha account ya kuweka pesa. Haiwezekani biashara usimamie wewe hela achukue dada. Huo ni ujinga, stand up na umuarifu mkeo kuwa imetosha... wanashida wakueleze wewe sio waende kubarib biashara.
 
Nimekuelewa
 
Sawa tu mkuu ulitaka hizo hela uje uwanunulie majeneza ya 1.5m wakifa? Thamini furaha ya ndugu zako mda huu wangali hai.
Kama unabahati ya utajiri unayo tu mkuu!
Ahahahahah
 
Kaka unakuwa mnyonge sanaaaa. Badilisha account ya kuweka pesa. Haiwezekani biashara usimamie wewe hela achukue dada. Huo ni ujinga, stand up na umuarifu mkeo kuwa imetosha... wanashida wakueleze wewe sio waende kubarib biashara.
Anasema anasimamia yeye na mama yake siyo mke wake
 
Nasimamia mimi na mzazi wangu wa kike ikitokea pesa zimetoka unakuta kachukua dada sina la kufanya ndio maana naomba ushauri
Ukienda chini umeenda chini na ukoo wote,kuanzia Mama,dada,baba na wewe mwenyewe,mambo kama hayo yaliyokukuta wewe yalimkuta kaka angu,famili walipomfilisi,wa kwanza wakumuuliza alikuwa mama,mama alimuuliza kaka "sasa ndio umefanya nini?",walisahau wao ndio walikuwa sababu ya kufilisika kwake..

Ushauri wangu kuwa mkali katika mafanikio yako,kaa chini na familia yako uwafahimishe,weka sheria kali,hakuna mtu kutoa pesa ya kiwango chochote bila ya amri yako,na yeyeyote atakae toa pesa bila ya amri yako hatua kali itachukuliwa..

Usiwe na muhali,wala heshima kwa mtu anaetaka kukurudisha nyuma kimaisha,,,...
 
Back
Top Bottom