Bibi alietembea kwa miguu ampe Rais zawadi ya kuku apewa gari

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Mwanamke mwenye umri wa miaka 52, Maggie Sapatu, kutoka Mwinilunga nchini Zambia, amezawadiwa gari baada ya kutembea kwa miguu karibu kilomita 1,000 hadi Lusaka kwa lengo la kumshukuru Rais Hakainde Hichilema.

Maggie alianza safari hiyo Agosti 15, 16, akiwa amebeba kuku wawili wa kienyeji aliokusudia kumkabidhi Rais kama ishara ya shukrani na pongezi kwa mikakati na sera mbalimbali za Serikali yake, ikiwemo elimu bure.

Baada ya kufika Ikulu, Maggie alikutana na Rais Hichilema, na kupata chakula cha pamoja akiwemo Jeremiah Tembo, ambaye alisafiri kwa baiskeli kutoka Lusangazi hadi Ikulu. Zawadi ya gari kwa Maggie ilitolewa na Jelumu Zambia kama kutambua ujasiri na jitihada zake.
1788847203813.png
 
View attachment 3665581
Masikini huwa wanahisi gari ndicho kitu cha maana sana. Huyo kama ametembsa hana pesa hilo gari linahitaji mafuta na service. Wangemtengenezea nazingira ya kupata kipato
 
Back
Top Bottom