Sumba-Wanga
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 5,353
- 1,234
si vizuri kwa sasa kuyaweka wazi sana kabla mume hajafanya maamuzi kwani taarifa ulizouliza zikisambaa sana mapema na bwana harusi akijua hilo litampa shida kisaikolojia.
Jamani wana jamvi kuna hili limetokea ,bibi harusi amefumaniwa gest ndani ya room tena akiwa amevua shela{gauni la harusi} baada ya kutoroka saloon akiwa anarembwa kwa ajili ya harusi na kwenda kumuaga mpenziwe wa zamani kwa mahaba,
kwa bahati mbaya au nzuri mmoja wahudumu wa gest husika alikua anamjua bi harusi huyo kwani na yeye alitarajia kuhudhuria hio harusi ndipo akatoa taarifa kwa ndugu wa bi harusi kwa kua hakufurahishwa na hilo, kwa hio watu wachache upande wa bi harusi na mmewe mtarajiwa ndo wamejua hilo tukio,mme yuko njia panda kwani maandalizi yote yalishakamilika na hata ndugu wa mbali washafika kwajili ya harusi.
Tumshauri bwana harusi afanyeje au achukue uamuzi gani kuhusu harusi?
Pilu nisamehe kwam nitakukwaza BUT siamini hii habari kwa sababu zifuatazo....
- Bibi harusi kaenda na shela guest.... Jamani hivi waelewa karaha ya kuvaa shela let alone kuanza kuzunguka nalo? Kwamba yee ni mjinga kiasi gani aende ku cheat na nguo ambayo kila mmoja lazima amtazame apitapo.
- Mwanaume ambae ana cheat na mwanamke wa mtu hasa wa ndoa/anatarajia kufunga ndoa yupo soo makini. Sidhani kama alikua amebanwa saaana kutaka fanya hilo tendo to the extent ya kumpokea bi dada na shela tena guest.
- Ni kweli Uchumba/ndoa nyiingi zimekua za kisanii.... but siamini kua watu wahusika huagana karibu na eneo la tukio (in the sense kua vijimtaa vya karibiana saana).
- Kwamba bwana harusi anataka ushauri? Huyo mwanaume wa wapi? Bi harusi mtarajiwa afumaniwe ndani ya shela na woote mwajua alafu atake ushauri zaidi ya kubwaga manyanga? Dah! Enways.... Labda utakuja na wapi yameishia...