JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkazi wa Kitongoji cha Kalilangwa Kijiji cha Mchangani Kata ya Ikola, Tarafa ya Karema Wilaya ya Tanganyika, Mkoa wa Katavi Winfrida Athanas (63) amenyofolewa masikio yote na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe baada ya kumvizia wakati akiwa amelala usingizi chumbani mwake.
Tukio hilo la kusikitisha na la kikatili limetokea hapo juzi majira ya saa tano usiku chumbani kwa mama huyo alipokuwa amelala kitandani.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Ikola Mwela Mrugwa amesema mama huyo amenyofolewa masiko yake mawili na mtoto wake wa kumzaa mwenyewe aitwaye Michael Msapi (40).
Siku hiyo ya tukio mtuhumiwa Michael Msapi alimvizia mama yake mzazi wakati akiwa amelala usingizi chumbani mwake na ndipo alipoingia ndani ya chumba hicho na kumnyofoa masikio yake yote mawili kwa kutumia meno yake na kumsababishia mama huyo maumivu makali sana.
Baada ya kuwa amefanya ukatili huu kwa mama yake mzazi mhumiwa huyo alitokomea baada ya kuwa mama yake amepiga mayowe ya kuomba msaada.
Mwela Mnugwa amesema baada ya majirani kusikia mayowe hayo walifika haraka kwenye eneo hilo na kumchukua Winfrida na kumkimbiza haraka kwenye kituo cha Afya cha Karema ambako hadi sasa anaendelea kupatiwa matibabu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ally Hamad Makame amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limeripotiwa katika jeshi la Polisi.
Chanzo: Walter Mguluchuma, Katavi