Bibi na babu yako bado wako hai? ni kipi unakipenda na kukikumbuka kuhusu wao?

Mimi bibi na babu zangu wote wameshatangulia mbele za haki ila tuliishi nao kwa miaka 5 wakati niko mdogo.

Babu yangu mzaa mama alikua mwalimu na alianza kunifundiusha kusoma na kuandika nikiwa na miaka mitatu.
Bibi yangu naye alikua mwalimu, nakumbuka alikua anatukimbiza kwenda kuoga kila jioni na kutunywesha uji kila tukirudi toka shule πŸ™‚.

Nawakumbuka sana kwa upendo na zawadi kede kede.

********* ** *****
CC:

Nomadix , Mallerina
makutupora , bonjov
Mje kutuambia kuhusu wazee wenu!
 
Babu yangu mzaa baba alifariki mwaka 1991, sikufanikiwa kumuona kabisa.

Bibi yangu nilimuona, alikua mpole sana, alikua anaongea kwa busara..

Aliomba sana akizaliwa mtoto wa kiume aitwe yeye (utamaduni wa wakurya huo)

Bahati ikanidondokea mimi😭😭😭
 
Ooooh bahati iliyoje kuitwa jina la bibi, inapendeza sana ! 😍
 
namisi uchapakazi wao ,sikuhizi hata wababu wa vijijini wakichimba shimo fupi tu ,eti vidole vinachubuka

umeona vidole vya Babu pichani hapo, ukipigwa kibao mjukuu unaweza hisi umepigwa na ubao
Umenichekesha sana, eti ukipigwa kibao unaweza kuhisi umepigwa na ubao" 🀣 🀣 🀣
 
Mimi ninachokipenda na kukikumbuka ni pale inqpofika usiku bibi alipokua ananiambia tukae kwenye shuka tukunje miguu nifunge na macho nikifungua macho najikutq tupo sehemu nyingine tofauti na pale tulipokuwa,na kingine ni pale tunapofika tulikoenda tunaingia kwenye nyumba bila mlango wa hiyo nyumba kufunguliwa
 
Bibi mzaa mama, nlikua nkimchokoza kwa kupiga chafya yenye keleleee, nikipiga ya kwanza anageuka ananiangalia tu, narudia ya pili chaaaaaaaafyaaaaa anaguna "mh we bibi, mwanamke hapigi chafya hivyo" basi anaanza na story za kikungwi......

Alikua anaamka mapemaaa kumi yupo macho akiamka anaanza kuniita bibi, bibi, bibi nikiamka bibi vipi anasema aaah kumbe umelala basi lala nilikua nadhani umeamka nlikua namind aaagrrrr 😁
 
huo muda bibi alikuwa kashanyolewa manyoya na Babu saa 10 alfajili kwa wanandoa ngumusana mana mwenye tundu haelewagi kitu

mjukuu wake unakoroma TU ,badala uamke kufagia au Radio Tanzania daresalaam ulikuwa huisikii
 
Duuuh bibi yako alikufundisha kuwanga πŸ˜…
Pia ID yako na Avatar vinaendana na ulivyolelewa.
 
 
Bibi yako ninja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…