Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Sijui kuhusu makofi na Bibi Titi.Katika mazungumzo ya hapa na pale ya watangazaji wa clouds fm, majibizano kati ya Gadner Habashi na Efraim Kibonde mwaka 2013 yalifanya nifuatilie legitimacy ya alichokuwa akisema bwana Kibonde kwamba Biti Titi Mohammed alileta ubishi mbele ya mwalimu Nyerere, na akaambulia kibao cha shavu la kushoto na Mwalimu Nyerere kujishtukia baadae kwamba alichofanya ni sawa lakin si kwa njia ile,
Kama kawaida yangu nikachimba kwenda kwa wazee wengi wenye busara kujua ukweli wa habari hii,
Maana hata kama habari Haina ukweli lakin imesikika katika chombo cha habari maarufu sana hata kama haikuwa habari kamili, ila ni mazungumzo ndani ya chombo hicho,
Nikamuuliza mzee mmoja ambaye amehudumu ikulu kwa muda mrefu R.I.P na sitamtaja jina,
Alinijibu hivi, bwana unashangaa kofi tu kwa Biti Titi? Nyerere alikuwa rais kweli na si mfano wa rais, angekufanya chochote kile na ukashindwa cha kufanya maana ukiangalia unakuwa kwenye upande wa makosa,
Suala la Biti Titi ni kwamba kuna maagizo alipewa akafanye nje ya nchi akaenda kinyume na maagizo ya boss wake, lakin akaomba ushauri kwa watu mbali mbali jinsi ya kumuingia Nyerere na kumueleza hasara Ile na ukweli ni kwamba kwa kosa lile Titi alistahiri adhabu kubwa mno, ila alipewa heshima kwa sababu ni mmama pekee aliyejitoa kwa nchi hii katika ukombozi, hivo suala la kofi sipendi kuliongelea zaidi,"
Akaendelea
" usiangalie mambo ya kofi angalia hata taifa lilipata hasara gani kwa wakati huo,
Pia mbona siyo Biti Titi tu, kuna wakuu wa wilaya waliwahi kurushiwa stepple machine kisa mauaji yaliyoendelea nchini mwao, kuna wakuu wa shule walichapwa viboko kwa kutuhumiwa ulevi, na kuharibu Mirada ya shule, ila habari hizo zilikuwa kimya kimya,"
Nyerere alikuwa ana kaa ikulu katika corridor fulan ndefu yenye zuria jekundu, alafu unapoingilia mlango unamuona kulee anakuangalia aangalii Pembeni, ukiwa na kosa ukaitwa na Nyerere ikulu, mtihani ulikuwa uanze mguu gani kuingia kwenye corridor, maana mpaka unamfikia anakuangalia una loose confidence,
Kwa kifupi Yule mzee alikuwa mkali sana, lakin hakuonea mtu alikuwa mkali kwa mambo ya msingi"
Britannica
Upande mwingine wa Nyerere, he was the consummate gentleman.
Mama yangu alifanya kazi Ikulu ya Nyerere. Hii nadhani ni baada tu ya kutoka chuo. Alinihadithia siku moja bado kidogo agongane uso kwa uso na Nyerere kwenye hiyo corridor iliyosemwa. Alikuwa anakata kona kuingia huko ndani kupeleka makaratasi ya Reuters, halafu hajajua Nyerere naye anakata kona kutoka. Ikawa bado kidogo tu wagongane uso kwa uso.
Mama akawa kaogopa sana ikawa kama ame freeze. Kugongana na Nyerere kwenye corridor Ikulu si mchezo. Akawa kajiona kama kakosa uangalifu na heshima. Akawa anasubiri kukaripiwa kwa maneno makali tu kwamba inakuwaje akose uangalifu vile, na maneno makali mengine kama hayo. Nyerere alikuwa anaogopwa. Lakini akajikuta sio tu hajakaripiwa, bali akamuona Nyerere tofauti aliyekuwa concerned na yeye (mama) zaidi kama yupo OK, Nyerere inaelekea alimuona huyu kashapanic ngoja nimsaidie kumrudisha kuwa normal tu. Akamwambia asighafirike sana, aendelee tu na kazi zake, ile kona imekaa vibaya.
Basi tangu siku hiyo mama akawa anamuona Nyerere si tu huyu lionized head of state, bali pia mtu anayeweza kuwa muungwana katika mahusiano ya kazini ya kila siku.
I just thought I should share that to give perspective.
Last edited: