Bibi Titi Mohammed: Historia, harakati na wasifu wake

Bibi Titi Mohammed: Historia, harakati na wasifu wake

acha kuongea unafiki usio na tija.eti wakristu hawakushiriki kwenye kupigania uhuru.Julius Kambarage Nyerere, Ali
Sykes, Lameck Makaranga,
Gosbert Milinga, Gelmandus
Pacha, Joseph Kimalando, Japhet
Kirilo, Abubakar Ilanga, Saadan
Kandoro, Suleiman Kitwara,
Kisunguta Kabara, Chewa Said
Chewa, Dosa Aziz, Patrick
Kunambi, Joseph Kasela Bantu,
John Rupia, Abdulah Sykes.kuna Christians wangapi hapo.na hizo pesa wanazopewa makanisa zinatolewa na nani? ikiwa serikali haijengi msikiti wala kanisa.shule zilirudishwa kw kukosa hela? mbona hata historia fupi kama hiyo unataka

kuipotosha leo pesa yakuen
desha hizo shule wamezipata wapi? huo ni ushabiki wakidini eti kanisa linapewa pesa na serikali

well said
 
Duh, mchango imefichwa wakati mimi namsikia Bibi Titi kabla hata huyo Mwamedi hajaandika zile pumba zake...
Kuuliza si ujinga.

Huyu mama amefanya mambo mengi kwenye nchi yetu unaweza kusoma kitabu cha hivi karibuni kinaitwa UAMUZI WA BUSARA mtunzi Mohamed Said AU LIFE AND TIMES OF ABDULWAHID SYKES.

Michango mingi ya wazalendo imefichwa.
 
Huyu Mwanasiasa Muasisi wa TANU na baadae CCM maarufu kama "IRON LADY" kwa misimamo yake kusisitiza USAWA WA KIJINSIA toka Enzi hizo na Mwl. Nyerere anamtambua haswaaa! Iweje leo Mfumo wa siasa zetu za sasa unamsahau? au kwa sababu alikuwa Muislamu? Wagalatia kwa ubinafsi balaa. Eti sasa mnataka Nyerere awe MTAKATIFU. kwa lipi hasa?
 
[QUOTE
mimi nataka kujua huyu mama alikuwa chamagani cha siasa?.
=Bikra;505071]
Habari Wana JF ! Naomba kama kuna Mtu Yoyote anajua Historia ya Bibi Titi anijuvye. Huyu Mama anaonekana kutajwa sana hapa Tanzania Mpaka kuna Barabara inaitwa Bibi Titi Street, Je Huyu alikua ni Mwanasiasa au ? Umaarufu wake unatokana na Nini ? Wadau Naomba Majibu yatakanifunua Macho na Kujua Historia ya Taifa Letu. ---------------------------------------------------------------------------------------------------- Kwa habari zaidi zinazo Mhusu Soma Hapa
[/QUOTE]
 
bibi Titi alitaka
kumpinduwa Rais Kambarage, sababu kubwa
ya kushukiwa kuwa alitaka kumpinduwa
nyerere ni kule kuwa rafiki mkubwa wa
kambona na wale watu wanne.

hao wengne wanne ni akina nani ?
 
Kuna jambo moja la ajabu lilitokea katika mazishi ya mwl nyerere nikiwa mfuasi na mshabiki mkubwa wa mwalimu.lakini wakati wa mazishi ulitokea mlipuko mithili ya bomu nikiwa mbali sikuweza kuona baadhi ya watu hasa polisi walianguka chini.katika uchokonozi nikaambiwa na wenzangu kuwa ni mizimu na wengine wakaninong'oneza kuwa nyerere kafanya mambo maovu ambayo hata maadui zake wanaogopa kuyatamka.swali lililokuwa linasumbua akili yangu ni vipi mtu kama nyerere mjamaa, mkristo safi akawa muovu kiasi hiki.nikaanza kutafuta historia yake kuanzia kwa marafiki mpaka maadui,ile kuanza tu nimekutana na taarifa ambazo nadhani Tundu Lissu kaziona na ndiyo maana kasema aliyosema.Nyerere hakuwa mjamaa wala muumini wa muungano wa afrika.Nyerere alikuwa mkabila mwenye chuki za kidini.na ndiye aliefanya mapinduzi ya zanzibar(kwaheri ukoloni kwaheri uhuru by al ghassany).mapinduzi yaliyofanya Genocide zanzibar(wikipedia zanzibar revolution).kawaua na wengine kawafunga marafiki wa kambona kwa kumhofia tu kambona kwa charisma yake.kavunja chhama cha waislam cha maendeleo yao east african muslim welfare society.kaiunga mkono biafrra kujitenga na akapeleka jeshi.kachochea ukabila zanzibar na udini kwa watu waliokaa pamoja toka mwaka 1500 wakristo na waislam wameishi pamoja na sultan alitoa ardhi kwa wakristo kujenga makanisa.kamuua edwado mondlane kwa bomu dar.kazuia msaada kwa patrice lumumba mpaka kauawa.kakosana na joshua nkomo kwa misimamo yake ya kibaguzi kama alivyokosana na mondlane.kataifisha mali za wakristo na waislam lakini karudisha za wakristo kakataa kurudisha za waislam hasa za aghakhan na shia ithanaashari kwa kifupi tusipojifunza namna ya kuelewa hatutajifunza namna ya kuokoka bomu alilotuachia nyerere tusipolitegua tumekwisha kuna vita baina ya tanganyika na zanzibar na tanganyika baina ya waislam na wakristo.tujadiliane vizuri turekebishe vinginevyo mzimu wa nyerere upo pamoja nasi.wakati dunia nzima wanasameheana makaburu na waafrika,marekani na japan yeye kaweka doctrine ambayo kina lukuvi wanaifuata yaani MWARABU NA MUISLAM MASHETANI.ndiyo maana tukitaka mabadiliko tu utasikia waarabu/waislam watakuja wakati hata us,uk na western wote wanaenada mashariki ya kati kufanya mashirikiano na hawa jamaa wenye mafuta ya bure sie tumekaa na chuki za nyerere.mungu amuweke panapomsitahili.
 
Habari Wana JF !

Naomba kama kuna Mtu Yoyote anajua Historia ya Bibi Titi anijuvye.

Huyu Mama anaonekana kutajwa sana hapa Tanzania Mpaka kuna Barabara inaitwa Bibi Titi Street, Je Huyu alikua ni Mwanasiasa au ?

Umaarufu wake unatokana na Nini ?

Wadau Naomba Majibu yatakanifunua Macho na Kujua Historia ya Taifa Letu.

----------------------------------------------------------------------------------------------------






Kwa habari zaidi zinazo Mhusu Soma Hapa

B,
Ingia hapo chini Cntrl-Click.

Huo ni mswada wa Maisha ya Bibi Titi Mohamed (1926 - 2000) kama Allah alivyoniwezesha kuuandika una maneno 8629:

https://mail.google.com/mail/u/0/?u...&attid=0.1&disp=safe&realattid=f_hvdqmqw30&zw
 
Duh, mchango imefichwa wakati mimi namsikia Bibi Titi kabla hata huyo Mwamedi hajaandika zile pumba zake...

Mphamvu,
Iweje ndugu yangu unanitukana?

hapa JF tunaingia kwa khiyari zetu hatulazimishwi ya nini kutukanana nasi
hapa tunabadilishana fkra?

Ungeliweza kusema maneno hayo hayo lakini bila kibri na kejeli.

Ukiniita, ''Mwamedi,'' ni sawa kwani hivyo ndivyo marehemu mama yangu
akiniita na wakati mwingine akiniita, ''Mwalimu Mohamed'' au ''Baba Mzee
Mohamed,'' ikitegemea ''mood,'' yake.

Hujaniudhi kwa kuniita ''huyo Mwamedi...''
Nini kinakuchoma ndugu yangu?

Ni hii ''knowledge'' yangu ya historia ya wazee wangu?

Hata wewe kama ungelizaliwa na wazee hawa na wakati ule wa 1950s
na mahali pale, Mtaa wa Kipata, Dar es Salaam na ukapata ''exposure,''
niliyopata na wewe ungelikuwa kama mimi na pengine zaidi.

Mimi sikuomba ila Allah alinileta kwa wazee wale bila ya mie kutaka.

Mimi sina sababu ya kukuchukia au kukuona wewe umepungukiwa kwa kuwa
tu uko hivyo ulivyo au kwa kuwa umezaliwa bara.

Halikadhalika nawe huna sababu wala haki ya kunichukia kwa ajili ya nasaba
yangu na ujuzi wangu.

Huo ni mswada wangu wa kitabu cha Bi. Titi Mohamed nakuzawadia:

https://mail.google.com/mail/u/0/?u...&attid=0.1&disp=safe&realattid=f_hvdqmqw30&zw
 
kanyang'anywa nyumba? and of all places Temeke.Nyerere can not be that bad,would someone enlighten us please

actually Nyerere was really 'that' bad when it comes to double-crossing him.... many families and clans suffered b'coz of their 'difference in govt/state perspectives'.... and this explains the monoparty system at that time... no one dared to even think otherwise. no body is perfect!
 
Bariadi,
Ahsante kwa link ya Bibi Titi.

Nimeisoma lakini kwa kweli hamna kitu mle ndani.

Hivi ndivyo nilivyoanza utangulizi kwa kitabu changu kuhusu Bibi Titi Mohamed (1926-2000):

''Ni vigumu kusema ni lini nimekuja kumfahamu Bi. Titi Mohamed. Nimefumbua macho nikikuwa
katika mitaa ya Dar es Salaam ya miaka ya 1950 na 1960 nikimuona na kumfahamu kuwa huyu
ndiye Bi. Titi. Mwanamke shupavu na kiongozi wa TANU.

Haikunipitikia kwa wakati ule nikiwa bado kijana mdogo wakati mwingine nikimuona katika mikutano
ya TANU pale Mnazi Mmoja au Jangwani kuwa ipo siku nitakaa nitafiti historia ya mashujaa wa uhuru
wa Tanganyika na Bi. Titi awe mmoja wa mashujaa wangu ambao nilataka sana kuandika maisha yao.

Siku moja tu kabla ya kifo cha Bi. Titi nilikuwa nikihojiwa na mwanafunzi wa kike wa Kitaliana kutoka
Chuo Kikuu cha Napoli, Italia ambae alikuwa akifanya utafiti kuhusu nafasi ya wanawake katika harakati
za kudai uhuru wa Tanganyika.

Binti huyu alikuwa alinihoji kuhusu Bi. Titi na akataka kujua kwa nini hatajiki katika historia ya TANU na
kwa nini wanawake wenzake aliokuwa nao katika harakati za kudai uhuru wanaonekana kutopenda
kueleza habari za Bi. Titi.

Nilimfahamisha binti yule kuwa sisi Watanzania tuna historia rasmi ya uhuru wa Tanzania ambayo
tunatakiwa kuienzi. Historia hiyo inaanza na Mwalimu Nyerere na kuishia na Mwalimu Nyerere.

Historia hiyo imewatoa wazalendo wengi katika historia pamoja na Bi. Titi. Binti huyo alikuwa na
masikitikokuwa wakati alipofanya mipango ya kutaka kwenda kumuhoji Bi. Titi akamkuta mgonjwa
kwa hiyo hakuweza kufanya mahojiano.

Nilimfahamisha mtafiti huyu yale niliyokuwa nayajua kuhusu Bi. Titi kisha tukaagana. Siku ya pili
nikapata habari kuwa Bi. Titi amefariki.

Kama alivyokuwa akisema mwenyewe marehemu, ‘Yote kuhusu mimi yameshaandikwa nyie waandishi
wa leo mtaandika nini ?'

Ni kweli Bi. Titi kaandikwa sana lakini waliomuandika hawakummaliza, kwa kuwa hawakummaliza ndiyo
maana na mimi nimepata nguvu ya kuweza kumuandika lau kama kwa muhtasari. Kwa hakika wengi wa
waandishi hao walikuwa wageni ; na wale waandishi wazalendo walipomwandika Bi. Titi walimwandika
kwa mtazamo wa agenda zao na vilevile bila kuwa na ujuzi wa historia ya Dar es Salaam katika miaka
ya 1950.

Wageni walimtazama Bi. Titi kwa jicho la ugeni mimi nataka kumwandika Bi. Titi kama alivyokwenda na
historia ya kudai uhuru. Nataka kumueleza Bi. Titi tokea mwanzo alipokuwa na Mwalimu Nyerere.
Nyerere akibandua hatua yake unyayo wa Bi. Titi unafuatia.

Nataka kumuandika Bi. Titi jinsi alivyopanda kutoka msichana mdogo wa Ki-Dar es Salaam akiwa na
miaka 26 hadi kufikia umaarufu mkubwa kabisa. Kisha ghafla nyota yake ikachujuka akaanguka na
akaishia kufungwa kifungo cha maisha kwa kosa la uhaini ambalo hadi kufa kwake alikana kuhusika.

Nataka kumuandika Bi. Titi jinsi alivyotoka kifungoni akiwa fukara mali yake yote imepotea na jinsi
alivyoyakabili maisha ya upweke na kutengwa. Nataka kumuandika Bi. Titi jinsi kwa ufundi mkubwa
na subra ya hali ya juu alivyomtegemea Mungu kama nilivyopata kumsikia akisema na Mungu akaitika
dua zake na kamrudishia siyo mali zake tu bali hata na hadhi yake.

Mtaa aliopewa kwa heshima yake ambao alinyang'anywa ukaja kurudishwa jina lake. Na wale waliomfanyia
khiyana ile wakiwa wa hai na hawana uwezo wa kufanya lolote.

Vipi Bi. Titi akaja kuuguzwa na kuzikwa na walewale watu waliolitangazia taifa kuwa alikuwa msaliti na
ta'azia zao baada ya kifo chake zikajaa maneno ya kumsifu. Ilikuwaje ikawa hivyo?

Nikiwa mtu mzima nilifanyiwa mihadi ya kuzungumza na Bi. Titi katika ya miaka ya 1990 nyumbani kwake
Upanga. Baada ya kusalimiana na kuniuliza nilikotoka nilimfahamisha wazazi wangu. Nilishangaa kuwa
alikuwa anamfahamu baba yangu vizuri sana hata akanieleza wajihi na umbo lake.

Nilimfahamisha kuwa nilikuwa nataka kuandika maisha yake. Bi. Titi akanikatalia kwa njia ya kistaarabu
kabisa. Kwa hekima kubwa sana aliweza kunitoa katika mazungumzo ya harakati za siasa za kudai uhuru
na akaelekeza fikra zangu katika senema ya watoto Cinderella niliyokuta akitizama pamoja na wajukuu
zake.

Kwa wale ambao walikuwa karibu na Bi. Titi watakuwa wanajua jinsi alivyokuwa fasaha wa kuzungumza
na jinsi alivyokuwa hodari wa kushinikiza hoja zake. Niliishia kunywa soda na kutazama ile senema katika
TV kisha tukaagana.

Lakini kwangu mimi nilikuwa nimefarajika sana. Miaka michache iliyopita rafiki yangu mmoja alikuwa anamuoa
binti ya ndugu yake Bi. Titi na harusi hii ilifanyika nyumbani kwa Bi. Titi Temeke. Hali niliyomkutanayo pale
Upanga ilikuwa tofauti sana na nilivyomuona Upanga mara tu alivyotoka kifungoni.

Kabla sijaondola Bi. Titi alinifahamisha kuwa hazina yake ya nyaraka za wakati wa kudai uhuru pamoja na picha
zake nyingi za kihistoria zilichukuliwa na askari wapelelezi wakati walipokuja kufanya upekuzi katika nyumba yake
kwa ajili ya tuhuma za kupindua serikali zilizokuwa zimemkabili katika miaka ya 1970.

Nilisikitishwa na hili kwa kuwa nilijua yeyote atakaekuja kuandika habari za Bi. Titi atakuwa amekosa zana za
kumsaidia kumwandika mama huyu kwa usahihi.''
 
KIlio cha BIBI TTI ndugu yangu mpaka leo kipo bado na hakika WAISLAM wanamini ni UDINI ulitumika., Kiukweli sisi tumekuw ana aKILi fupi sana na FINYU siku zote, kila kitu tunakimbilia UDINI.
HIVi kambona naye alikuwa MUISLAM.
Kambona alikuwa anataka kuslimu.Naona story tellers wamejigeuza historians.
 
Kuna jambo moja la ajabu lilitokea katika mazishi ya mwl nyerere nikiwa mfuasi na mshabiki mkubwa wa mwalimu.lakini wakati wa mazishi ulitokea mlipuko mithili ya bomu nikiwa mbali sikuweza kuona baadhi ya watu hasa polisi walianguka chini.katika uchokonozi nikaambiwa na wenzangu kuwa ni mizimu na wengine wakaninong'oneza kuwa nyerere kafanya mambo maovu ambayo hata maadui zake wanaogopa kuyatamka.swali lililokuwa linasumbua akili yangu ni vipi mtu kama nyerere mjamaa, mkristo safi akawa muovu kiasi hiki.nikaanza kutafuta historia yake kuanzia kwa marafiki mpaka maadui,ile kuanza tu nimekutana na taarifa ambazo nadhani Tundu Lissu kaziona na ndiyo maana kasema aliyosema.Nyerere hakuwa mjamaa wala muumini wa muungano wa afrika.Nyerere alikuwa mkabila mwenye chuki za kidini.na ndiye aliefanya mapinduzi ya zanzibar(kwaheri ukoloni kwaheri uhuru by al ghassany).mapinduzi yaliyofanya Genocide zanzibar(wikipedia zanzibar revolution).kawaua na wengine kawafunga marafiki wa kambona kwa kumhofia tu kambona kwa charisma yake.kavunja chhama cha waislam cha maendeleo yao east african muslim welfare society.kaiunga mkono biafrra kujitenga na akapeleka jeshi.kachochea ukabila zanzibar na udini kwa watu waliokaa pamoja toka mwaka 1500 wakristo na waislam wameishi pamoja na sultan alitoa ardhi kwa wakristo kujenga makanisa.kamuua edwado mondlane kwa bomu dar.kazuia msaada kwa patrice lumumba mpaka kauawa.kakosana na joshua nkomo kwa misimamo yake ya kibaguzi kama alivyokosana na mondlane.kataifisha mali za wakristo na waislam lakini karudisha za wakristo kakataa kurudisha za waislam hasa za aghakhan na shia ithanaashari kwa kifupi tusipojifunza namna ya kuelewa hatutajifunza namna ya kuokoka bomu alilotuachia nyerere tusipolitegua tumekwisha kuna vita baina ya tanganyika na zanzibar na tanganyika baina ya waislam na wakristo.tujadiliane vizuri turekebishe vinginevyo mzimu wa nyerere upo pamoja nasi.wakati dunia nzima wanasameheana makaburu na waafrika,marekani na japan yeye kaweka doctrine ambayo kina lukuvi wanaifuata yaani MWARABU NA MUISLAM MASHETANI.ndiyo maana tukitaka mabadiliko tu utasikia waarabu/waislam watakuja wakati hata us,uk na western wote wanaenada mashariki ya kati kufanya mashirikiano na hawa jamaa wenye mafuta ya bure sie tumekaa na chuki za nyerere.mungu amuweke panapomsitahili.
Hii stori ukiitupia FB utapata washabiki wengi sana.
Huko FB kuna watu wengi sana wanaoweza kuamini stori za mizimu na maruhani kama za kwenye Aladin Na Taa Ya Ajabu.
 
Huyu bibi alikuwa mkosoaji mkubwa wa siasa mbovu za Nyerere (yes call me anti Nyerereism if you please) na aligombana na Nyerere baada ya kumlaumu sana na hatua yake ya kutaifisha mali za wananchi (wajasiriamali wa siku hizo) na kilichomuudhi sana bibi Titi ni kule kuwadhulumu waislamu kwa kuwanyan'ganya mali zao na kuuwa jumuiya zao za kimaendeleo. Nyerere alipovyomshughulikia bibi huyu ni hadithi ambayo haipaswi kusimuliwa mbele ya mtu wa chini ya miaka 18, ni aibu na udhalilishaji wa hali ya juu kuwahi kufanyiwa mwanamke mtu mzima na heshima yake kama yeye ndani ya Jamhuri hii ya Muungano tena na mtu aliyemsukuma kwa nguvu na mali yake kuwa rais wa nchi.

Bibi Titi kama alivyokuwa Kasella Bantu na Eli Anangisye, walikuwa ni miongoni mwa watanzania wachache wa siku hizo waliokuwa na uthubutu wa kukosowa uozo wa serikali ya Nyerere, ingawa Nyerere alitumia ubabe kuwashughulikia, bado walibaki katika haki na kusimamia ukweli wa kile walichokiamini, ni historia baadae ilikuja kutoa hukumu kuwa walikuwa sahihi na Nyerere alikuwa wrong kushabikia siasa za kijambazi na unyan'ganyi, alizoziita "ujamaa na kujitegemea", ambazo zilishindwa.

Bibi Titi anabaki kuwa ni alama ya harakati za wanawake waliokuwa mstari wa mbele katika mapambano ya uhuru wa kweli na haki za wananchi, mawazo ambayo alikuwa aki share na mwanasiasa machachari wa Kenya siku hizo, Jaramog Oginga Odinga (baba yake Raila Odinga), ambaye hakupendezwa kabisa na uhuni wa watawala wa Kiafrika baada ya uhuru waliojifanya "wakoloni weusi", katika maandishi yake yaliyokuja kuwa kitabu "Not Yet Uhuru", anabainisha wazi kuwa Afrika haijapata kile ilichokipigania kwa jasho na damu kwa kuwa "ukoloni wa mtu mweusi" umechukuwa nafasi yake.

Oginga, kama Bibi Titi, waliona viongozi waliopewa dhamana za kuyaongoza mataifa machanga baada ya uhuru,wanageuka wabinafsi, wachoyo, makatili na wasiopenda kusikiliza bali kusikilizwa na kukataa kata kata kukosolewa kwa namna yoyote ile, wamekuwa wabaya zaidi ya wakoloni weupe, kwao wao (Bibi Titi na Oginga) uhuru ulikuwa bado kwa watu weusi kutoka na siasa chafu za kidikteta za Kenyatta na Nyerere,Nkurumah n.k.

WEll said mkuuu!!! Ila kuna watu hawaijui historia vyema,mie kuna siku nilikuwa natoa photocopy hapo PEACOCK HOTEL,kuna mzee aliiingia hapo akaanza kumwaga data mpaka nikaogopa its true kwamba NYERERE hakuwa mtu pekee katika kudai uhuru wa TANGANYIKA wapo wengi sana tena hasa wale waliokuwa na majina ya KIARABU wengi hawajaandikwa kabisa kwenye historia
 
bibi titi hapewi heshima yake hila kwakuongezea tu bibi titi no mzaliwa Wa rufiji ni mndengereko na wakati huo temeke yote ilikuwa inakaliwa na wandengereko alipokuwa waziri alipeleka rami kwao rufiji rami hile ya zamani sio hii ya sasa lakini halipo tumiwa tu kumpindua nyerere mkuu alihilani rufiji yote vitu vingi rufiji hili nyimwa ikiwemo elimu

tukajikita kwenye dini yetu ndo maana ukisikia shehe katoka rufiji shehe kweli
akiwemo braza kipozeo
 
BIBI TITI MOHAMMED; MWANAMKE SHUJAA WA HARAKATI ZA UHURU WA TANGANYIKA ALIYEONJA JELA.

Na. Comred Mbwana Allyamtu


Kila binadamu hupitia magumu tena mara nyingine magumu hayo ambayo mimi huyaita ‘kipimo cha uimara wa mtu’ hupelekea kutoka kwa roho.

Leo nimeona si vibaya kuwakumbusha juu ya mwanamke aliyepata kujitoa kwa moyo wote ili nchi yetu ya Tanzania iwe huru lakini inaelezwa kuwa maisha yake ya mwisho hapa duniani yalijawa na huzuni, upweke, kubaguliwa na ufukara mkubwa.

Huyu ni Bibi Titi Mohammed, bila shaka vijana wengi wa sasa hawamjui kabisa mama huyu shupavu na wamekuwa wakisikia au kuiona tu barabara ya Bibi Titi. Kati ya miaka ya 1970 mwanamke mwenye wajihi wa ushupavu Bibi Titi Mohammed alihusishwa katika tukio la kujaribu kutaka kuipindua serikali ya wakati huo, Alihukumiwa kifungo cha maisha jela. Haikuwa rahisi kulipokea hilo kwani baadae alitolewa lakini ameendelea kukana kabisa mpaka umauti ulipomfika mwaka 2000.

Bibi Titi Mohammed aliingia TANU kwa kushawishiwa Schneider Plantan(Wanahistoria wengi huandika Nyerere-Baba wa Taifa ndo alimuingiza kwenye Chama si jambo la kweli) akapata kadi namba 16 na mumewe ndugu Boi Selemani alipewa kadi 15. Bibi Titi alikuwa mwasisi wa Umoja wa Wanawake Tanganyika (UWT) uliokuja kuundwa rasmi mwaka 1962.

Wakati wa harakati za kupigania uhuru alisimamia vikundi vya muziki kama vile lelemama’ na mara zote alitangulia kuongea na umati mkubwa kabla hata Nyerere hajaongea na watanganyika. Alikuwa na maneno makali dhidi ya ukoloni na alikuwa ana nguvu kubwa ya ushawishi. Akiwa na miaka 26 tu alikuwa ni mmoja kati ya wanawake wachache walioaminiwa katika kuongoza mapambano dhidi ya udhalimu waliokuwa wakifanyiwa Watanganyika.


Mwaka 1955, Nyerere na Bibi Titi Mohammed walifanya mkutano mkubwa huko Tabora. Hii ni kutokana na mualiko walioupata toka kwa watu wa huko, Ikumbukwe kuwa Tabora ya wakati huo ilikuwa na hamasa kubwa katika kudai uhuru. Hivyo mualiko ulitoka kwenye kamati ya wazee kama Hassan Mohamed Ikunji, Hamis Khalfan, Swedi Mambosasa, Germano Pacha, Juma Mrisho, Shaaban Mohamed Silabu, Bilali Rehani Waikela, Mohamed Mataka wakati ule akiwa muadhin wa Masjid Nur - msikiti wa Wamanyema pale Tabora.


Kuna mikutano mingi tu ya harakati za uhuru aliyoongoza Bibi Titi mfano ule wa Mombasa akishirikiana na Tom Mboya katika Ukumbi wa Tononoka. Kiujumala mkutano mkuu wa kwanza tabora ulifungua njia kukubalika kwa TanU baadaye kulifanyika Azimio La Tabora’. Azimio hilo liliongozwa na Nyerere na wengine kama Sheikh Suleiman Takadir,Mzee Jumbe Tambaza, Juma Selemani na Bibi Titi.

Baada ya uhuru 1961 alichaguliwa kuwa mbunge na waziri pia. Halikuwa jambo la kushtua kwani alistahili. Mwaka 1963 inaelezwa kulitokea kutokuelewana kati ya Bibi Titi na Mwalimu Nyerere wakati wa mkutano wa Halmashauri Kuu ya TANU uliofanyika Ukumbi wa Karimjee.

Hapo walitupiana maneno makali kabisa. Inaelezwa kuwa kati ya mambo mengine mengi sababu zilikuwa ni Halmashauri Kuu ya TANU kulivunja Baraza la Wazee wa TANU ambao kwa hakika walisaidia wakati wa harakati za uhuru, Hilo lilipingwa na Bibi Titi.


Jambo jingine linaelezwa na mwandishi Said Mohammed katika maandishi yake kuwa ni uamuzi wa Bibi Titi kuitetea jumuia ya EAMWS ambapo Mwalimu Nyerere alipinga hilo kwani aliona ni hatari kuchanganya ‘Dini na Siasa’. Bado kumekuwa na ugumu kupata taarifa hasa chanza cha mtifuano huo kwani wengi wanaelezea mkutano huo ulikuwa ni nafasi ya kuonesha tofauti zao wazi wazi.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1965 Bibi Titi na Tewa(Tewa Said Tewa alikuwa rais wa jumuia ya EAMWS) wakapoteza viti vyao ndani ya TANU na serikalini. Mwaka 1968, Bibi Titi alikamatwa na kuhusishwa na tukio la uhaini’ Mahakama ilimkuta na hatia ,alihukumiwa kwenda jela maisha. Mwaka 1972 aliachiwa huru kwa msamaha wa rais. Bado aliendelea kukana kuhusika kabisa na tukio hilo. Alirudi na kuendelea na maisha yake ya kawaida huko maeneo ya Temeke.

Inaelezwa kuwa kuwa alipoteza kumbukumbu za harakati za uhuru kama vile picha na taarifa nyingi za vikao.
Aliporudi walikuwa na urafiki kama zamani na Mwalimu Nyerere kama zamani, Aliumwa na kupelekwa na serikali ya Tanzania katika hospitali ya Net Care huko Afrika ya Kusini. Alifariki dunia akiwa hapo hospitalini akipata matibabu tarehe 5 Novemba 2000. Hakika ni ‘mama wa nguvu’ na shujaa mwanamke wa Tanzania yetu.

Ndimi

Comred Mbwana Allyamtu

+255679555526
+255765026057
Mbwanaallyamtu990@gmail. Com
ATTACH=full]361464[/ATTACH]
 

Attachments

  • 1467281543483.jpg
    1467281543483.jpg
    28.6 KB · Views: 127
Back
Top Bottom