Bible Error: Mwanzo 1:1-3a Kosa kubwa la Milenia, kutafsiri kutoka kwenye lugha ya Kiebrania

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
Mimi ni mkristo nimelelewa katika ukristo tangu nikiwa mdogo.

Mwanzo tu wa biblia katika kitabu cha mwanzo 1:1-3a kunakuwa na makosa makubwa ambayo yamedumu karne na karne. Haya yalitokana na kutafsiri moja kwa moja lugha ya kiebrania kwenda kwenye Lugha ya Kigriki na hatimaye lugha ya kingereza.

Inasomeka
1. In the beginning God created the heavens and the earth.
2. Now the earth was formless and empty, darkness was over the surface of the deep, and the Spirit of God was hovering over the waters.
3. And God said, "Let there be light," and there was light.

Kutoka kwenye origin (Hebrew)
1. Bereshit bara Elohim et hashamayim ve'et ha'aretz,

Maelezo Kwenye mstari wa kwanza

Kwenye kiebrania tunaona hapo anaongelea Elohim neno elohim ni wingi. Yaani Miungu. maana yake hapo anaongelea miungu na wala siyo Mungu mmoja. Umoja wa neno Elohim ni Eloah

Hapo tayari kunakuwa na mkanganyiko mwanzoni tu.

Maelezo zaidi
Katika hiyo 1:1-3a inasomwa yote kwa pamoja. Lakini yule aliyekuwa anatafsiri aliigawanya na kisha akahatibu maana nzima ya maelezo.

Kwenya hebrew bible haiongelei kuhusu the beginning of creation.

Bali inaelezea kuwa wakati Miungu walipokuwa wakiumba dunia dunia ilikuwa ukiwa.

Inaweza kusomeka:-
1 When Gods began to create heaven and earth—2 the earth being unformed and void, with darkness over the surface of the deep and a wind from Gods sweeping over the water—3a Gods said, ‘Let there be light

Hii hapa juu ndiyo tafsiri sahihi ya kitabu cha mwanzo kabisa.

Nitaendelea kuchanganua zaidi.

Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
 
Kwa
 
Mhuuuu ........unakoelekea utaanda biblia Yako...
 
My God! Umesoma biblical exegesis au hermeneutics kweli? Kwenye uandishi wa Biblia kuna matumizi ya lugha ya heshima kwa Mungu (majestic language) - 'kutumia wingi mahali pa umoja', na wala siyo makosa ya uandishi. Hata katika lugha kama Kifaransa kuna matumizi ya lugha kama hiyo. Mfano, ukimwongelea mzazi au mtu official unatumia neno 'vous' = 'nyinyi'. Mfano, "comment allez-vous": How are you? Lakini kama agemate, colleague, rafiki, utasema: "comment ca va"?: How are you? Kwenye lugha kama Chichewa, kumu'address' mzazi, mtu official au kumsalimia utasema: 'Ali bwanji'...? Sawa na kusema "Hamjambo"? Lakini kumu'address' agemate, rafiki, rafiki etc: utasema: 'mulibwanji'...? 'Ali bwanji' ni wingi wa 'muli bwanji'. Ukitumia 'ali bwanji' kwa mtu mmoja, Ina maana umetumia 'majestic language'...umeonyesha heshima kwa mtu unayemsalimia. Wakati ukitumia 'muli bwanji' kama ni mtu mkubwa kwa cheo au umri atajisikia kwamba umempa salamu ya kawaida/umemdharau. Style ya uandishi wa Kitabu cha Mwanzo, inafuata tradition hii ya majestic language, lakini siyo kosa la kiuandishi, bali style ya uandishi.
 
Eloah singular ->Elohim plural
 
Hiyo majestic language uhakika. Hata sisi wasukuma hutumia wingi kumadress mtu kwa heshima. Mfano: "bhang'wanashija nabho bhalala na ndwala = wakina mwashija nao wamelala wanaumwa". Hiyo ni taarifa inayotolewa kwa mtu, kuonesha jamaa/mume anamheshimu sana mke wake.
 
Mathayo 28:19

Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
Kama nilivyokueleza Council of Nicaea ndiyo iliyoleta mambo haya yote. Kesho nitaielezea vizuri na source of Trinity ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…