Biblia imeandika Yakobo alipigana na Mungu usiku kucha na akashinda pambano hilo. Inakuwaje Mungu anapigana na anapigwa na kiumbe chake ?

Biblia imeandika Yakobo alipigana na Mungu usiku kucha na akashinda pambano hilo. Inakuwaje Mungu anapigana na anapigwa na kiumbe chake ?

"Barua zako zina hubiri ushindi..
Kutangaza vita wakati mtutu tu haushiki .. cha ajabu maadui ni wakurithi chanzo ni kitendawili nilichokisoma kwenye hadithi njoo.."


Dizasta vina: Hatia VI
 
ukisoma biblia katika kitabu cha Mwanzo 32 kuanzia mstari wa 22 mpaka mstari wa 32

utaona mistari ikielezea jinsi ambavyo Yakobo Alipambana na Mungu


22 Usiku huo, Yakobo akaamka, akawachukua wake zake wawili, wake wake wawili wa kufanywa wake wa mitala, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki. 23 Baada ya kuwavusha mto, akapeleka pia mali zake zote. 24 Basi Yakobo akabaki peke yake, na mtu mmoja akapambana naye mpaka alfajiri. 25 Huyo mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, akaugusa fundo la paja la Yakobo, hata paja lake likavunjika alipokuwa akipambana naye.


26 Kisha huyo mtu akasema, "Niachilie, kwa kuwa alfajiri imekaribia."


Lakini Yakobo akajibu, "Sitakuacha uende mpaka unibariki."


27 Yule mtu akamuuliza, "Jina lako ni nani?"


Yakobo akajibu, "Jina langu ni Yakobo."


28 Kisha huyo mtu akasema, "Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli, kwa sababu umepambana na Mungu na wanadamu, nawe umeshinda."


29 Yakobo akamuuliza, "Tafadhali niambie jina lako."


Lakini yule mtu akamjibu, "Kwa nini unaniuliza jina langu?" Kisha akambariki hapo.


30 Yakobo akapaita mahali pale Penieli, akisema, "Ni kwa sababu nimemwona Mungu uso kwa uso, na bado maisha yangu yameokolewa."


31 Jua lilipochomoza juu yake alipokuwa akipita Penieli, alikuwa akichechemea kwa sababu ya paja lake. 32 Kwa hiyo, hata leo hii, Waisraeli hawali kano iliyoko kwenye fundo la paja, kwa sababu fundo la paja la Yakobo liliguswa karibu na kano hiyo.


Najiuliza kwa nini Mungu anapigwa na kiumbe alichokiumba ?
Ili uelewe maandiko lazima pia ufahamu context na tamaduni na Waisraeli. Kwa wana wa Israeli kila kiumbe wa kiroho walimuita mungu. Na kila jambo lililotokea lililo juu ya uwezo wao walijua ni Mungu kafanya. Hivyo, hapo anaposema alishindana na mungu maana yake alishindana na Malaika. Na ile kusema alimshinda maana yake Yakobo alimsonga huyo Malaika akihitaji ambariki hadi Malaika kakubali. Na Yakobo alitambua kuwa alikuwa akiishi ktk laana ya kumlaghai ndugu yake. ESAU. Hivyo kwa Malaika kukubali kumtamkia baraka na kumbadilishia jina kutoka Yakobo hadi Israel ndio maana ya kushinda. Kwa hiyo ujumbe wa Biblia hapo ni kwamba tusikate tamaa ktk kumwomba Mungu bali tuombe tupambane hadi tupate ushindi.
 
Minajia tu kwamba Jacob was so stubborn God had to break him before he would surrender himself to God's will....😔
 
Japo hakuna sehemu Jacob kapigana na Mungu, ni vile umeamua kuelewa utakavyo wewe...
Jambo lingine swali lako linajibiwa na huo Mstari wa 26.
Ukiona huelewi maana yake huna utashi wa kutosha na hujasoma vzuri ukaelewa andiko
 
Ukisoma biblia katika kitabu cha Mwanzo 32 kuanzia mstari wa 22 mpaka mstari wa 32

Utaona mistari ikielezea jinsi ambavyo Yakobo Alipambana na Mungu

22 Usiku huo, Yakobo akaamka, akawachukua wake zake wawili, wake wake wawili wa kufanywa wake wa mitala, na wanawe kumi na mmoja, akavuka kivuko cha Yaboki. 23 Baada ya kuwavusha mto, akapeleka pia mali zake zote.

24 Basi Yakobo akabaki peke yake, na mtu mmoja akapambana naye mpaka alfajiri. 25 Huyo mtu alipoona kuwa hawezi kumshinda, akaugusa fundo la paja la Yakobo, hata paja lake likavunjika alipokuwa akipambana naye.

26 Kisha huyo mtu akasema, "Niachilie, kwa kuwa alfajiri imekaribia."

Lakini Yakobo akajibu, "Sitakuacha uende mpaka unibariki."

27 Yule mtu akamuuliza, "Jina lako ni nani?"


Yakobo akajibu, "Jina langu ni Yakobo."

28 Kisha huyo mtu akasema, "Jina lako halitakuwa tena Yakobo, bali Israeli, kwa sababu umepambana na Mungu na wanadamu, nawe umeshinda."

29 Yakobo akamuuliza, "Tafadhali niambie jina lako."

Lakini yule mtu akamjibu, "Kwa nini unaniuliza jina langu?" Kisha akambariki hapo.

30 Yakobo akapaita mahali pale Penieli, akisema, "Ni kwa sababu nimemwona Mungu uso kwa uso, na bado maisha yangu yameokolewa."

31 Jua lilipochomoza juu yake alipokuwa akipita Penieli, alikuwa akichechemea kwa sababu ya paja lake. 32 Kwa hiyo, hata leo hii, Waisraeli hawali kano iliyoko kwenye fundo la paja, kwa sababu fundo la paja la Yakobo liliguswa karibu na kano hiyo.

Najiuliza kwa nini Mungu anapigwa na kiumbe alichokiumba ?
'Huyo mtu' ni wapi imetajwa Mungu?
 

Kwanini Yakobo alimshinda Mungu, Je! Mungu huwa anashindwa na wanadamu?


SWALI: Je! Mungu anashindwa na mwanadamu? Kama sio Kwanini siku ile aliposhindana na Yakobo alikiri kushindwa?

JIBU: Jibu ni ndio Mungu anakubali kushindwa, Pengine utauliza unakubalije kushindwa wakati yeye ni Mungu asiyeshindwa na chochote.
Tabia za Mungu sio kama zetu, Mungu huwa anathamini sana, NIA, BIDII na MATAMANIO ya mtu, kiasi kwamba hata kama matamanio hayo yatakuwa kinyume na mpango wake, au mapenzi yake, ikiwa tu mtu huyo ataendelea kuking’ang’ania basi mwisho wa siku atamwachia, akipate anachokitafuta haijalishi kitakuwa ni kibaya au chema. Huko ndiko kushindwa kwa Mungu.
Na ndicho kilichotokea kwa Yakobo, aliposhindana na Mungu usiku kucha, akiomba apewe jambo ambalo halikuwa mpango wa Mungu kumpa wakati ule, lakini alipong’ang’ania bila kukata tamaa, kwa kupigana mieleka, ikambidi Mungu ampe tu kulingana na haja yake.
Jambo hili hili utaliona pia wakati ule Bwana Yesu akiwa duniani, utakumbuka kuwa mwanzoni kabisa alitumwa kwa Wayahudi na sio kwetu sisi mataifa, lakini siku moja alikutana na mwanamke mmoja king’ang’anizi wa kimataifa aliyeishi nchi moja iliyoitwa Tiro. Mwanamke huyo alikuwa na binti yake aliyesumbuliwa na mapepo. Na alipokutana na Yesu alitaka aponywe, lakini Yesu hakuongea naye chochote, kwasababu sio hakutumwa kwao, lakini mama huyo hakukata tamaa, baada ya kumlilia sana, ndipo Yesu akafungua kinywa chake akamwambia, maneno haya;

Unaona, hapo, neema ya wokovu ilikuwa haijatufikia bado watu wa mataifa, kwasababu Kristo alikuwa hajasulibiwa bado, lakini mwanamke huyu, aliiwahi kabla hata ya wakati wenyewe kujika, jambo ambalo lilikuwa kinyume kabisa na mpango wa Mungu. Na ndio maana Kristo alitumia maneno magumu kama yale ili mradi tu adhoofishe mataminio yake, akawa hajibiwi, akawa anaitwa mbwa. Lakini mwisho wa siku Yesu kuona bado ni king’ang’anizi basi akakubali kushindwa. Akampa haja ya moyo wake, kama alivyofanya kwa Yakobo.
Hata wewe leo hii, unaweza shindana na Mungu nawe ukamshinda, hilo linawezekana kabisa, pengine hukustahili kupokea uponyaji wa ugonjwa wako sasa, kutokana na mambo uliyomkosea Mungu, pengine,hustahili kupewa hilo hitaji lako kwa sasa hivi, labda pengine limekusudiwa ulipokee baadaye sana, baada ya miaka 15, pengine hustahili kuwa na hiyo karama sasa hivi, lakini uking’ang’ana na Mungu, anaweza kukusogezea karibu hilo hitaji lako haijalishi alitaka litimie baada ya miaka 20.
Na ndio maana Bwana Yesu alituambia mfano huu, naomba nawe pia uutafakari vizuri;

Usichoke kung’ang’ana na Mungu wako..
Bwana akubariki.

Kutoka wingulamashahidi.org
Umetupatia uelewa mzuri sana mkuu, mm pia napenda kujua, lipo andiko lisemalo hakuna mtua awezae kumuona Mungu na akaishi..je mbona yakobo aliishi hata pale alipoonana na Mungu na kushindana nae!
 
Hata wewe ukiwa na bidii na nia utashinda kama Yakobo.
Asingeshinda asingepewa nchi
 
Back
Top Bottom