Biblia imeandika Yakobo alipigana na Mungu usiku kucha na akashinda pambano hilo. Inakuwaje Mungu anapigana na anapigwa na kiumbe chake ?

"Barua zako zina hubiri ushindi..
Kutangaza vita wakati mtutu tu haushiki .. cha ajabu maadui ni wakurithi chanzo ni kitendawili nilichokisoma kwenye hadithi njoo.."


Dizasta vina: Hatia VI
 
Ili uelewe maandiko lazima pia ufahamu context na tamaduni na Waisraeli. Kwa wana wa Israeli kila kiumbe wa kiroho walimuita mungu. Na kila jambo lililotokea lililo juu ya uwezo wao walijua ni Mungu kafanya. Hivyo, hapo anaposema alishindana na mungu maana yake alishindana na Malaika. Na ile kusema alimshinda maana yake Yakobo alimsonga huyo Malaika akihitaji ambariki hadi Malaika kakubali. Na Yakobo alitambua kuwa alikuwa akiishi ktk laana ya kumlaghai ndugu yake. ESAU. Hivyo kwa Malaika kukubali kumtamkia baraka na kumbadilishia jina kutoka Yakobo hadi Israel ndio maana ya kushinda. Kwa hiyo ujumbe wa Biblia hapo ni kwamba tusikate tamaa ktk kumwomba Mungu bali tuombe tupambane hadi tupate ushindi.
 
Minajia tu kwamba Jacob was so stubborn God had to break him before he would surrender himself to God's will....😔
 
Japo hakuna sehemu Jacob kapigana na Mungu, ni vile umeamua kuelewa utakavyo wewe...
Jambo lingine swali lako linajibiwa na huo Mstari wa 26.
Ukiona huelewi maana yake huna utashi wa kutosha na hujasoma vzuri ukaelewa andiko
 
'Huyo mtu' ni wapi imetajwa Mungu?
 
Umetupatia uelewa mzuri sana mkuu, mm pia napenda kujua, lipo andiko lisemalo hakuna mtua awezae kumuona Mungu na akaishi..je mbona yakobo aliishi hata pale alipoonana na Mungu na kushindana nae!
 
Hata wewe ukiwa na bidii na nia utashinda kama Yakobo.
Asingeshinda asingepewa nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…