Biblia inasema Fungu la kumi apewe mlawi, Je hapa Tanzania kuna walawi? Je wachungaji ndio walawi ?

MKATA KIU

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2010
Posts
3,410
Reaction score
8,184
Wakristo wenzangu naombeni majibu.

Fungu la kumi ni sheria ya Musa katika agano la kale.

kwenye agano la kale Hesabu 18:21 imeandika Fungu la kumi lilitolewa kwa kabila lililokosa ardhi linaitwa kabila la Walawi kwa ajili ya kazi yao katika hema la kukutania.

Leo tunaambiwa tupo kwenye agano jipya alilokuja nalo yesu kristo. tunaambiwa UKRISTO NI DINI YA WAFUASI WA YESU AMBAO TUNAFATA AGANO JIPYA.

Sheria nyingi za agano za kale hazifatwi. Ila swala la fungu la kumi makanisa yanakusanya kwa kasi kubwa.

Napenda kujua kuhusu fungu la kumi ambalo biblia inasema wapewe walawi. Je hapa Tanzania walawi ni kina nani ?

1740914658588.png
 
Tuambie kwanza Fungu la kumi ni nini?

Mkulima anaesubiri mazao yaive baada ya miezi mitano inakuaje atoe fungu la kumi kila Jumapili wakati havuni kila wiki?
Zaka siyo sadaka mtumish hivyo huwa haitolewi kiholela

Zaka huwa inatolewa kulingana na kipato chako je unakipata kwa siku au kwa week au kwa mwezi au kwa mwaka?
Bas kama unakipata kwa mwaka toa zaka ya mwaka kama ni kwa mwezi basi toa zaka kwa mwezi kama ni kwa week basi toa kwa week

Asante mtumish
 
Wakristo wenzangu naombeni majibu.

Fungu la kumi ni sheria ya Musa katika agano la kale.

Leo tunaambiwa tupo kwenye agano jipya alilokuja nalo yesu kristo.

Sheria nyingi za agano za kale hazifatwi. Ila swala la fungu la kumi makanisa yanakusanya kwa kasi kubwa.

Napenda kujua kuhusu fungu la kumi ambalo biblia inasema wapewe walawi. Je hapa Tanzania walawi ni kina nani ?
Agano jipya tunatoa vyote, yaani asilimia 100 siyo 10%, kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo na kuvitumia wenyewe vyote. Ndivyo walivyokuwa wanafanya kanisa la kwanza chini ya mitume. Vyote tupatavyo ni vya Bwana na tunasimamia na kuvitumia wenyewe. Soma Matendo 4: 32 na kuendelea

Hata sisi wenyewe ni wa Bwana baada ya kutununua kwa damu ya thamani. Na kwa sasa kila aliyeokoka ni kuhani kama walivyokuwa Walawi. Aidha, utoaji wa agano jipya ni kadri moyo upendavyo, siyo shinikizo au kama sheria ya agano la kale.
 
Agano jipya tunatoa vyote, yaani asilimia 100 siyo 10%, kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo na kuvitumia wenyewe vyote. Ndivyo walivyokuwa wanafanya kanisa la kwanza chini ya mitume. Vyote tupatavyo ni vya Bwana na tunasimamia na kuvitumia wenyewe.

Sasa kusema tutoe asilimia 10 ya mapato yetu sio utekelezaji wa sheria na shinikizo? Kwa nini isiwe kiasi chochote hadi iwe hiyo asilimia 10? Ktk sheria hii ndio unafiki wa hizi dini unadhihirika!
 
Kwa hiyo watu kupangiwa kiwango cha sadaka au michango ni upagani?
 
Zaka siyo sadaka mtumish hivyo huwa haitolewi kiholela

Zaka huwa inatolewa kulingana na kipato chako je unakipata kwa siku au kwa week au kwa mwezi au kwa mwaka?
Bas kama unakipata kwa mwaka toa zaka ya mwaka kama ni kwa mwezi basi toa zaka kwa mwezi kama ni kwa week basi toa kwa week

Asante mtumish
Zaka unayoisema haikuwa lazima pesa, bali chochote upatacho. Soma Mathayo 23:23. Hata uchumapo mchicha, mashina 9 yalikuwa yako, shina la 10 ni zaka. Kwa sasa hakuna zaka ya fungu la 10 au asilimia 10. Utoaji wa sasa ni asilimia 100 na kisha tunatumia wenyewe vyote. Soma Matendo 4: 32-37
 
Sasa kusema tutoe asilimia 10 ya mapato yetu sio utekelezaji wa sheria na shinikizo? Kwa nini isiwe kiasi chochote hadi iwe hiyo asilimia 10? Ktk sheria hii ndio unafiki wa hizi dini unadhihirika!
Agano jipya hatupaswi kupangiwa au kulazimishwa kiasi cha kutoa, bali tutoe kadri moyo wa kila mmoja upendavyo. Ukitaka kutoa vyote, nusu, robo au kutotoa kabisa ni sawa tu. Soma 2 Wakorintho 9:7 na 1 Timotheo 6:18
 
Wakristo wenzangu naombeni majibu.

Fungu la kumi ni sheria ya Musa katika agano la kale.

Leo tunaambiwa tupo kwenye agano jipya alilokuja nalo yesu kristo.

Sheria nyingi za agano za kale hazifatwi. Ila swala la fungu la kumi makanisa yanakusanya kwa kasi kubwa.

Napenda kujua kuhusu fungu la kumi ambalo biblia inasema wapewe walawi. Je hapa Tanzania walawi ni kina nani ?
Haijasema walawi pekee yake mkuu,imesema Kuhani, mlawi na mjane

Sasa Kuhani ni mchungaji
mlawi(mhudumu yeyote wa kanisani, hata mlinzi ni mlawi)
 
Back
Top Bottom