Biblia inasema Fungu la kumi apewe mlawi, Je hapa Tanzania kuna walawi? Je wachungaji ndio walawi ?

Biblia inasema Fungu la kumi apewe mlawi, Je hapa Tanzania kuna walawi? Je wachungaji ndio walawi ?

Mchungaji ndio mlawi
mchungaji mweusi mzaramo anakuwaje Mlawi ?

Walawi katika Biblia

Walawi walikuwa mojawapo ya kabila kumi na mbili za Israeli, wakitokana na Lawi, mwana wa tatu wa Yakobo na Lea. Katika Biblia, walitengwa kwa ajili ya kazi za kidini na huduma ya hekalu, wakihudumu kama wasaidizi wa makuhani (ambao walitoka katika ukoo wa Aroni, aliyekuwa Mlawi).
 
Agano jipya linafuatwa sema kuna mabadiliko yalitokea kutokana na kuwa na mapungufu ndio mana likaja jipya kuhusu fungu ka kumi hata agano jipya walitoa fungu la kumi soma waebrania 7:1_10,ni lazima utoe sehem ya kumi ya mapato yako sadaka kama fungu la kumi sadaka nyingine ni sehem ya maamuzi yako.lkn hii ni amri.
Hakuna ulazima au amri yoyote ya kutoa. Soma 1 Nyakati 29: 14, 16-17 na 2 Kor 9:7. Hata hivyo hakuna tunachotoa maana vyote ni vya Mungu. Tunampa yeye vyote kwa imani na kubaki navyo wenyewe vyote, tukivisimamia na kula wenyewe. Soma Matendo 4: 32, 34-37. Kisha nenda sura ya 5 usome habari za Anania na Safira.
 
mchungaji mweusi mzaramo anakuwaje Mlawi ?

Walawi katika Biblia

Walawi walikuwa mojawapo ya kabila kumi na mbili za Israeli, wakitokana na Lawi, mwana wa tatu wa Yakobo na Lea. Katika Biblia, walitengwa kwa ajili ya kazi za kidini na huduma ya hekalu, wakihudumu kama wasaidizi wa makuhani (ambao walitoka katika ukoo wa Aroni, aliyekuwa Mlawi).

Kwanza mpango wa Mungu Sio walawi tu bali waisrael wote walitakiwa wawe makuhani fursa ambayo sasa tumepewa hadi sisi wasimbiti.
Kutoka 19.
Aliahidi qngewafanya kuwa ukuhani wa kifalme.

Mjmi naweza kuwa mlawi wako.
 
ha ha ha, mkristo mtanzania leo ndio muisrael halisi, huku waisrael wenyewe sio wakristo
Muisrael asiye mkristo ni mmataifa kama mataifa wengine. 70% ya wale wanaojiita waisrael pale middle east hawaamini uwepo wa Mungu. Ni wamataifa tu kama wasandawe wasiojua kitu maporini.
 
Tuambie kwanza Fungu la kumi ni nini?

Mkulima anaesubiri mazao yaive baada ya miezi mitano inakuaje atoe fungu la kumi kila Jumapili wakati havuni kila wiki?
Unaweza ukawa sawa, lakini jaribu kuwaza haya;

1. Fungu la kumi ni asilimia 10 ya pato lako. Hutakiwa kutoa fungu la kumi kama hujapata. Anayesubiri mazao yaive baada ya miezi mitano anatakiwa atoe baada ya miezi mitano.

2. Pamoja na hiyo namba moja hapo juu, wakati anasubiri hiyo miezi mitano mazao yaive, anakuwa hali chakula? anachokula hakitokani na kipato? Kama anachokula kinatokana na kipato, basi atoe 10% ya anachokipata wakati akisubiria mazao yaive.

3. Kipato cha huyo anayesubiri mazao yaive kwa miezi mitano, ni hayo mazao pekee?? Kama hapana, basi basi anasubiria mazao yaive, atoe fungu la kumi kwa hicho kipato kingine.
 
hilo fungu la kumi anapaswa akabidhiwe nani ?
 
Back
Top Bottom