Agano jipya tunatoa vyote, yaani asilimia 100 siyo 10%, kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo na kuvitumia wenyewe vyote. Ndivyo walivyokuwa wanafanya kanisa la kwanza chini ya mitume. Vyote tupatavyo ni vya Bwana na tunasimamia na kuvitumia wenyewe. Soma Matendo 4: 32 na kuendelea
Hata sisi wenyewe ni wa Bwana baada ya kutununua kwa damu ya thamani. Na kwa sasa kila aliyeokoka ni kuhani kama walivyokuwa Walawi. Aidha, utoaji wa agano jipya ni kadri moyo upendavyo, siyo shinikizo au kama sheria ya agano la kale.