Biblia inasema fungu la kumi litolewe mara moja tu kwa mwaka, hawa wanaodai fungu la kumi kila wiki ni wezi. Fungu la 10 waweza kulinywea hata pombe

Zaka ni sehemu ya kumi
1: katika mbegu au matunda hii inawakilisha mazao ya kilimo

Mambo ya Walawi 27:30 Tena zaka yote ya nchi, kama ni mbegu ya nchi, au kama ni matunda ya nchi, ni ya BWANA; ni takatifu kwa BWANA.

2: wanyama wa kufugwa
Mambo ya Walawi 27:32 Tena zaka yote ya ng’ombe, au ya kondoo, kila apitaye chini ya fimbo; sehemu ya kumi watakuwa ni watakatifu kwa BWANA.
Nyakati hizo za kale shughuri kuu ilikuwa kilimo na ufugaji ndio maana hapa tunaona zaka ikitajwa katika maeneo haya mawili
Ya kilimo na ufugaji
Zaka ni takatifu kwa bwana maana yake nini
Ni kitu ambacho kimetengwa mahususinkwa ajili ya bwana yani kitu hicho ni wakfu kitu hichonwana wa israeli hawakutakiwa kukichukua ipo mfano mingi lakini unaweza kusoma habari hii ya yoshua sura ya sita karibu yote
Yoshua 6:18 Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo mtayafanya matuo ya Israeli kuwa yamelaaniwa na kuyafadhaisha.
Zaka inatolewaje
1: mahali alilipo jina lake

Kumbukumbu la Torati 12:11 wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA.

Kumbukumbu la Torati 12:13 Ujihadhari usitoe sadaka zako za kuteketezwa katika kila mahali upaonapo;

2: zaka wamepewa wanq wa lawi

Hesabu 18:21 Na wana wa Lawi, nimewapa zaka yote katika Israeli kuwa urithi wao, badala ya huo utumishi wautumikao, maana, ni huo utumishi wa hema ya kukutania.
Wana wa lawi walichagukiwa kufanya kazi moja tu ya utumishi katika nyumba ya Mungu ndipo aliamulunwapewe zake kama posho zao ya kujikimu za maisha yao hawakutakiwa
Kufanya biashara wala kuwa na kazi za aina nyingine yoyote
Kwa leo wana wa lawi ni sawa na watumishi lakini je watumishi hawa wa leo wanazo sifa hizo za wana wa lawi na je ni kweli hao tunaowapa zaka leo wana mwakilisha Mungu wa kweli aliyetoa agizo hilo?

Hesabu 18:24 Kwa kuwa zaka ya wana wa Israeli, waisongezayo kuwa sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA, nimewapa Walawi kuwa urithi wao; kwa hiyo nimewaambia, ya kwamba, katika wana wa Israeli hawatakuwa na urithi uwao wote.
Wana hawa wa lawi hawakupewa sehemu yoyote wakati wana wa israeli wana gawana maeneo baada ya kuvuka wao walipewa tu zaka kwa utumishi wao

Sasa tuchambue andiko la mada yetu kumb 14 :22
Kwa kifupi kabla ya kusoma kumb 14 tunatqkiwa kuanza na na sura ya 12

Kumbukumbu la Torati 12:11 wakati huo itakuwa kwamba mahali pale atakapopachagua BWANA, Mungu wenu, alikalishe jina lake, hapo ndipo mtakapoleta kila kitu ninachowaamuru; sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu zote teule mtakazoweka kwa BWANA.
Hapantunaona aina mbali mbalimbali za matoleo na kwa kawaida ilikwa inatolewa mala moja kwa mwaka na ikiwa mtu alikuwa tajiki basi ulikuwa mzigo mkubwa sana na haikuwa zaka pekee kama tunavyozani

Baada ya kuuza na kubadilisha kuwa pesa walifanya nini waligawa mafungu kulingana na sheria yao na pale kulikuwa na sadaka za kuteketezwa ,sadaka za unga nk hivyo walitakiwa kutao walivipqta wapi wakati wameuza walinunua katika mji hule na baadaye watu walipoona imekuwa biashara kubwa walisogea adi hekalunimkuuza vitu mbalimbali ndipo wakati wa yesu alipindua meza

Yohana 2:15 Akafanya kikoto cha kambaa, akawatoa wote katika hekalu, na kondoo na ng’ombe; akamwaga fedha za wenye kuvunja fedha, akazipindua meza zao

Yohana 2:16 akawaambia wale waliokuwa wakiuza njiwa, Yaondoeni haya; msiifanye nyumba ya Baba yangu kuwa nyumba ya biashara.
Ili lilitokana na watu kuwa na mahitaji ya sadaka na kwamba pesa yote walinunua vitu na kula na kufulahi la hasa ila walikwenda huko na ilikuwa sikukuu kubwa walimtolea bwana sadaka na kula na kufulahi

Je kwa nyakati zetu tunapaswa kutoa zaka jibu ni ndio ikiwa aliyetoa agizo ni Mungu wako
Changamoto za utoajinwa zaka nyakati za leo
Kuna changamoto ya hesabu kutokana ma changamoto ya uchumi na mahitaji makubwa watumishi wengi wamewaingiza watu kufata kanuni za ma hesabu mengi yakiwa sio sahihi
Kumbuka mzigi wa uchumi wa leo sio kilimo na mifugo ni pesa so hesabu zake zikoje hapo ndio kwenye mtihani je inapawa kuwa vipi ni sehemu ya kumi ya faida ikiwa ni biashara ikiwa kazi basi sehemu ya kumi ya mshahara sasa watumishi wengine wanataka basic bila makato hapo napo ni changamoto nyingine
Hakuna zaka ya kujipaliza wala ya mshahara mzima zaka ni sehemu ya kumi inatolewa na mtu aliyeamua Mungu wa Israeli kuwa ndiye Mungu wake na kwa mtumishi halisi wa Mungu huyo
Wengi leo wanatoa zaka kama michango tu ya kawaida haina aina hualisia hule ulio kusudiwa kanuni nyingi hazifatwi mlawi nyenyewe anafanya biashara na kazi mbalimbali kinyume na utaratibu hakutakiwa kuwa na urithi wowote ndio akapewa hiyo zaka
Mda hautosh kuchambu mambo mengi sana haya ni kwa ufupi ikiwa unaona bado kuna maswali jua haya ni kwa ufupi
 
Sasa kama moyo wako unapenda chini inakuwaje?, utaenda kuila hiyo fungu la kumi na dada zetu hawa au?
 
Maandiko yako wazi kabisa hapo Ila umeandika bila kutafakari ndugu yangu. Unajua maana ya neno Zaka? Ni sadaka ya Aina gani?
 
To me, 10% ya hela ya kila mwezi ukiijumlisha kwa mwaka mzima (hiyo 10%), ni sawa na kujumlisha kipato chako cha mwaka, then upige hesabu ya 10%. Mfano kwa mwenye kipato cha 100,000/- kwa mwezi;

1. 10% ya mwezi mmoja ni 10,000/-, hii kwa mwaka (miezi 12) ni 120,000/-

2. Kipato cha mwezi ni 100,000/- hivyo kwa mwaka mzima ni 1,200,000/-, 10% yake ni 120,000/-

Hivyo, hakuna tofauti kwa maana ya jumla ya fedha unayoitoa kama fungu la kumi kwa mwaka. By the way, hii ya kulipa 10,000/- kila mwezi, psychologically utajisikia nafuu kuliko kulipa 120,000/- kwa mara moja
 
Huyu hakuambiwa sahihi. 10% ya 300,000/- ni 30,000/-
Mimi nimekadilia tu kipato chake huenda labda alisema kuwa anafikishaga mpaka laki 5

Maana ana kiduka cha uchafu alikinunua laki 5 kwa jamaa pia nimnunuz wa samaki,kwenye samak anaweza pata faida mpaka elfu 50 kwa siku ila sio kila siku kuna siku wanakosa na kuna siku anaambulia hata elfu 20 faida
 
Kwa mtu ambaye kipato chake siyo kile kile kila mwezi, huyu alipe kwa mwezi au ajumlishe kipato cha kila mwezi then alipe mwishoni kwa mwaka 10% ya jumla ya kipato chake cha mwaka. Mfano, kama Januari umepata 500,000/-, then lipa 50,000/-. Kama februari umepata 700,00/- then lipa 70,000/- etc au jumlisha za kila mwezi then mwisho ukalipe 10% ya jumla
 
Kuna jamaa yangu kipato chake kwa mwez ni kama 300,000

Aliambiwa awe anatuma 50,000 kila mwez alifanya hvyo mara kadhaa baadae alichomoa
Sehemu ya fungu la kumi kwa 300,000 ni 30,000 tu hiyo anayoambiwa atoe 50,000 ni wizi
 
Hata hivyo kuna watu wana sifa ya jutoa zaka na wengine wanatakiwa kutoa sadaka tu

Zaka ni sehemu ya kumi ya mapato yako , Sasa kuna mtu yeye hajafika kumi kwenye mapato yake, mfano awe mkulima au mfugaji amelima amepata kipimo cha nne au tano ,mfugaji ana mifugo saba au tisa hapo atoe nini?
Wanao paswa kuotoa zaka ni wale waliovuka kumi chini ya hapo ni matokeo ya hiari tu.
 
Sehemu ya kumi ya hyo ni 30000 na sdaka yake 30000 jumla 600
00
Mkuu sadaka ni hiari ya moyo wako Aina kiwango Wala upangiwi Cha kutoa. Ila sehemu ya kumi ndiyo ina kiwango ambacho kitatokana na ulichokipata kwa mfano umefanya biashara umepata faida ya 20000 na mtaji wako ni 100000. Jumla ni 120, 000. Unachotakiwa kufanya toa mtaji wako wa laki weka pembeni. Katika 20000 ya faida unatoa 2000 ndiyo sehemu ya funguo la kumi unabaki na 18000 yako unaweka kwenye mtaji wako au unatumia. Ukiona unapangiwa sadaka ondoka hapo ni utaperi tu
 
umemtaja mleta mada kuwa hana akili,kumbe ww ndio chenga kabisa umempinga bila facts zaidi ya kusema Fungu la kumi ni sadaka ya HEKALU wala sio kwa ajili ya KANISA,MSIKITI,SINAGOGI lakini ulivyo kiazi hata hiyo maana ya HEKALU huijui zaidi ya krudia rudia tu HEKALU HEKALU lakini huelezi maana ya hilo HEKALU ndio kitu gani hasa na linafanyaje kazi zake na mambo gani yanafanyika huko ndani ya Hekalu..na ili liitwe HEKALU linatakiwa liweje au liwe na vigezo vipi na liongozwe na nani na kwanini linastahili hilo fungu la kumi.? sio ww unaimba tu kama kasuku HEKALU HEKALU na kupinga wenzio unaona wanapotosha.. kwanza tujibu hayo maswali hapo juu nasi totoke gizani ili tufanye yaliyo sahihi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…