Biblia kwa Jicho Jingine

Swali ni muhimu kwa sababu ukijibu hilo ndio tutaweza kuelewa unachokiimanisha unaposema hautaki kuamini bali unataka kujua.

Unaweza kuamini kitu ambacho haukijui?
Unaweza.

Watu wote wanaomuamini Mungu ambaye nikiwauliza maswali wanashindwa kuyajibu, wanamuamini Mungu ambaye hawamjui.

Wangemjua, wasingepata tabu kujibu maswali yanayomhusu.

Watu wote wanaosema wanamuamini Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, wakati akili zao hazina uwezo wa kuujua uwezo wote ukoje, ujuzi wote ukoje wala upendo wote ukoje, wanamuamini Mungu ambaye hawamjui.

Ndiyo maana hawawezi kuthibitisha yupo.

Ndiyo maana hawawezi kuondoa contradiction iliyo katikadhana ya kuwepokwake.

Ndiyo maana kuamini si muhimu, kwa sababu unaweza kuamini usichokijua, ukasema kipo, wakati hakipo.

Ndiyo maana sisisitizi sana habari za kuamini.

Kwa sababu unaweza kuamini mavi yako ni Mungu.

Bila kujua uungu wa mavi yako unakuja vipi.

Wakati mavi yako si Mungu.

Kuaminikwamba mavi yako ni Mungu, wakati si Mungu, hakuyafanyi mavi yako yawe Mungu.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?

Hujathibitisha.
 
Ujumbe mzito sana huu
 
Hata wewe huna imani kwamba naweza kuamini.

Hatuchekani.

Hujajibu akili ni nini.

Hujathibitisha Mungu yupo.

Huwezi kuthibitisha Mungu yupo.

Kwa sababu hayupo.

Ni hadithi za uongo tu.
Yani jamaa anajaribu kukuelewesha ila sema unajikuta hutaki kuelewa...kubali kushindwa muda mwengine mkuu
 
Kwa haya majibu yako,hata mtu aandike page 100 kukueleshwa unadhani utamuelewa kweli?

Mind set yako isha kuwa programmed kupinga uwepo wa Mungu...otherwise iwe re-programmed huwezi kukubali chochote kuhusu uwepo wa Mungu
 
Mkuu unapata tabu sana na mchungaji kiranga.
Yeye hataki kuamini...anatafta kujua.
Wewe unalazimisha aamini .
Uwepo wa Mungu ni imani..... Bila hiyo ni bure.
Mungu huthibitika uwepo wake ukiwa karibu nae.
Uko sahihi. Lakini Kiranga anataka kila kitu akijue kwa kuona na kigusa. Nikamuuliza, anaamini kama ana akili? Akashindwa kujibu.
 
Reactions: Ok9
Yani jamaa anajaribu kukuelewesha ila sema unajikuta hutaki kuelewa...kubali kushindwa muda mwengine mkuu
Anajaribu kunielewesha nini? Mbona hanijibu maswali yangu? Atanielewesha vipi bila kuweza kujibu maswali niliyo nayo?

Unajuaje kwamba ana uwezowa kunielewesha mimi ikiwa maswali yangu hawezi kuyajibu?
 
Kwa haya majibu yako,hata mtu aandike page 100 kukueleshwa unadhani utamuelewa kweli?

Mind set yako isha kuwa programmed kupinga uwepo wa Mungu...otherwise iwe re-programmed huwezi kukubali chochote kuhusu uwepo wa Mungu

Nimeuliza maswali mawili rahisi sana, ambayo mpaka sasa hayajajibiwa, hayawezi kujibiwa na naona hayatajibiwa.

Kwa sababu, habari ya kuwepo Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote ni uongo.

Maswali hayo ni.

1. Je unaweza kuthibitisha Mungu huyo yupo? Kama unaweza, thibitisha. Mapaka sasa hakuna aliyethibitisha Mungu huyo yupo.


2. Imekuwaje Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wotena upendo wote akaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana, wakatialikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kufanyika wala kufikirika na hayapo kabisa?

Sijajibiwa swali hili.

Hakuna anayeweza kulijibu.

Kwa sababu limehoji habari ya uongo.

Habari kwamba Munguhuyo yupo.

Kama unasema Mungu yupo, nijibu maswali haya mawili.
 
Kwahiyo kwa maelezo hayo ni kusema kwamba watu walitakiwa wamjue kwanza Mungu baada ya kumjua kisha ndio waamini?

Mfano walitakiwa wajue kwanza Mungu yupo wapi na sio kuamini tu yupo bila kujua yupo wapi?
 
Kwahiyo kwa maelezo hayo ni kusema kwamba watu walitakiwa wamjue kwanza Mungu baada ya kumjua kisha ndio waamini?
Ukijua kitu, hukiamini, unakiamini tu kile ambacho hukijui.

Kitendo cha kujua kinakutoa kwenye imani, kinakupeleka kwenye ujuzi.

Mathalani, nikiwa nataka kuja kwako, sina hakika kama upo, lakini nakisia utakuwepo, mida ya jioni unapenda kubarizi nyumbani, naanza kuja kwa mategemeo ya kukukuta nyumbani, sijui, naamini utakuwepo.

Nikifika nyumbani, nikakukuta upo, nishavukakuamini tena, nimejua upo, nimethibitisha upo, siamini upo nyumbani, najua upo nyumbani. Siwezikuamini upo nyumbani tena, najua upo nyumbani.

Ndiyo maana nasema, wanaomuamini Mungu, hawamjui.

Ndiyo maana mimi na waamini Mungu hatuwezi kuelewana, wao wataniambia habari za kuamini (kukubali bila uthibitisho) wakati mimi sitaki kuamini, nataka kujua kwa uthibitisho.
 

"Watu wote wanaomuamini Mungu ambaye nikiwauliza maswali wanashindwa kuyajibu, wanamuamini Mungu ambaye hawamjui."

Maelezo yako yanajichanganya kabisa.
 
"Watu wote wanaomuamini Mungu ambaye nikiwauliza maswali wanashindwa kuyajibu, wanamuamini Mungu ambaye hawamjui."

Maelezo yako yanajichanganya kabisa.
Hapana, wewe tu una tongotongo hujui kusoma.

Watu wote wanaomuamini Mungu ambaye nikiwauliza maswali wanashindwa kuyajibu, wanamuamini Mungu ambaye hawamjui.

Wanamuamini kwa sababu hawamjui.

Wangemjua, wasingemuamini, wasingekuwa na sababu ya kumuamini, wangemjua.

Kamini ni kukubali bila uthibitisho.

Ukiamini kitu, huna uhakika nacho, huna uthibitisho, umekubali tu.

Ukijua kitu, una uhakika nacho, una uthibitisho, huna haja ya kuamini, huwezi kuamini, kwa sababu unajua.

Kuamini na kujua ni mtutually exclusive.

Huwezi kuamini kitu, halafu ukakijua pia hapo hapo, kuamini maana yake hujui, umekubali bila uthibitisho.

Kujua maana yake huamini, umeshapata uthibitisho, umetoka kwenye kuamini, umeondoa shaka, hukubali tu bila uthibitisho, umethibitisha.

Umeelewa?

Of course not.
 
Sasa ajabu wewe unataka uthibitisho wa uwepo wa Mungu kwa watu ambao wanaamini Mungu(wanakubali Mungu yupo bila uthibitisho),
 
Sasa ajabu wewe unataka uthibitisho wa uwepo wa Mungu kwa watu ambao wanaamini Mungu(wanakubali Mungu yupo bila uthibitisho),
Nawaonesha kwamba hawamjui, wanaamini, kwa sababu hayupo.

Kama unasema yupo, thibitisha yupo.
 
Nawaonesha kwamba hawamjui, wanaamini, kwa sababu hayupo.

Kama unasema yupo, thibitisha yupo.
Wanaamini kwa sababu hayupo ndio nini?wakati umesema kuamini ni kukubali jambo bila uthibitisho,sasa wewe unawadai uthibitisho huku ukijua kuwa kabisa kuwa kuamini ni kukubali jambo bila uthibitisho.

Vyovyote vile wanavyomuelezea Mungu ndivyo walivyoamini kwa maana wamekubali bila uthibitisho,ila wewe unakuja kusema hakuna Mungu halafu et kama mtu anabisha atoe uthibitisho.

Hauoni kuwaambia watu wenye kuamini Mungu(kukubali jambo bila uthibitisho) wathibitishe Mungu ni sawa na wewe unaposema haiwezekani kuthibitisha kitu kisichokuwepo?maana wangekuwa na uthibitisho wasingekuwa wanaamini tena.
 
Ukiamini mavi yako ni Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, mavi yako yanakuwa huyo Mungu?
 
Ukiamini mavi yako ni Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, mavi yako yanakuwa huyo Mungu?
Point sio unachokiamini ni kweli au sio hasa ukizingatia hicho kitu hukijui wala huna uthibitisho nacho bali umekubali tu,tatizo hapa ni wewe kutaka uthibisho kwa huyo mtu ambaye yeye mwenyewe hana uthibitisho na hakijui hicho kitu na ndiyo maana anaamini kama angekuwa anakijua hivyo angekuwa na uthibitisho asingeamini.

Kwani wewe ukisema kitu fulani hakipo inakuwa kweli hakipo kwa sababu umesema hakipo?
 

Point ni kutafuta ukweli.

Na ukweli haupatikani kwa kuamini tu, unapatikana kwa uthibitisho.

Swali lako la kusema kitu hakipo, kitu hakiwi hakipo kwa kusemwa tu.

Kitu pia hakiwi kipo kwa kusemwa tu kipo.

Ndiyo maana kuna uthibitisho.

Ili kuthibitisha ukweli.

Unaweza kuthibitisha Mungu yupo?
 
Kama ni hivyo kwanini ukiambiwa uthibitishe hakuna Mungu huwa unasema haiwezekani kuthibitisha kitu kisichokuwepo,inamaana tutawezaje kupata ukweli maana ukweli unajulikana kwa uthibitisho?

Halafu tafsiri yako neno kuamini ni kukubali jambo bila uthibitisho,kwahiyo kitendo cha mtu kuamini kitu fulani maana yake hana uthibitisho wa hilo jambo,sasa mtu anayeamini Mungu kumwambia hakuna Mungu hayupo na ndiyo maana hawawezi kuthibitisha,hauoni inakuwa sio sahahihi? kwa sababu ni kweli hana uthibitisho ila pia haina maana kuwa kuamini jambo maana yake hilo jambo si la kweli kwa sababu linaweza kuwa kweli au sio kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…