Biblia ndio Chuo Pekee Duniani unachoweza kujifunza Upendo, Amani, Furaha na Uvumilivu

Agano la kale hili
1. Kumbukumbu la Torati 20:16-17
“Lakini katika miji ya mataifa haya akupayo Bwana, Mungu wako, kuwa urithi, hutawaacha hai mtu ye yote...”

2. 1 Samweli 15:3
“Sasa nenda, ukawapige Amaleki, ukaangamize kabisa vitu vyote walivyo navyo, wala usiwaachilie; uwauwe mume na mke, mtoto na mtoto anayenyonya, ng’ombe na kondoo, ngamia na punda.”

3. Yoshua 6:21
“Wakaangamiza kabisa kila kitu kilichokuwa mjini, mwanamume na mwanamke, kijana na mzee, ng’ombe na kondoo na punda, kwa makali ya upanga.”

4. Hesabu 31:17-18
“Basi sasa, waueni wavulana wote; na kila mwanamke aliyekwisha kujua mume kwa kulala naye, mwueni.”

5. Zaburi 137:9
“Heri atakayewakamata watoto wako na kuwaponya mwambani!”

6. Yeremia 50:21
“…Ua kabisa, uwaangamize, asema Bwana, fanya yote kama nilivyokuamuru.”

7. Hosea 13:16
“Samaria atachukuliwa hatiani, kwa maana ameasi dhidi ya Mungu wake. Watanguliwa kwa upanga; watoto wao wachanga watavunjwavunjwa, wanawake wao wenye mimba watatumbuliwa.”

8. Kumbukumbu la Torati 7:2
“Na Bwana Mungu wako atakapowatia mikononi mwako, nawe ukawapiga, waangamize kabisa…”

9. Yoshua 10:40
“Yoshua akapiga nchi yote… Hakusaza chochote kilicho hai, kama Bwana, Mungu wa Israeli, alivyomwagiza.”

10. Ezekieli 9:5-6
“Akawaambia wale wengine, ‘Piteni mji nyuma yake, mkiua; jicho lenu lisione huruma, wala msiache. Muweni wazee, vijana, wanawali, watoto wachanga na wanawake...’”

Twende agano jipya
1. Mathayo 5:21-22
“Mmesikia kwamba watu wa kale waliambiwa, ‘Usiue, na mtu atakayemuua atastahili hukumu.’ Lakini mimi nawaambia, kila mtu anayemkasirikia ndugu yake atastahili hukumu...”

2. Mathayo 26:52
“Ndipo Yesu akamwambia, ‘Rudisha upanga wako mahali pake, kwa maana wote wautwao upanga kwa upanga wataangamia.’”

3. Luka 12:45-47
“Lakini mtumishi huyo akisema moyoni mwake, ‘Bwana wangu anakawia kuja,’ akaanza kuwapiga watumishi wenzake wa kiume na wa kike, na kula na kunywa na kulewa, bwana wake huyo mtumishi atakuja siku asiyotarajia na saa asiyojua, atamkata vipande viwili na kumweka pamoja na wasioamini.”

4. Yohana 8:44
“Ninyi ni wa baba yenu ibilisi, nanyi mnataka kutimiza tamaa za baba yenu. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli, kwa kuwa hakuna kweli ndani yake...”

5. Tito 1:12
“Mmoja wa wao mwenyewe, nabii wao, alisema, ‘Wakrete daima ni waongo, wanyama wabaya, walafi wavivu.’”

6. 1 Wakorintho 4:21
“Je, mnataka nije kwenu na fimbo, au kwa upendo na roho ya upole?”

7. Ufunuo 2:22-23
“Tazama, nitamtupa kitandani, na wale wazini pamoja naye nitawatupa katika dhiki kuu, wasipotubu matendo yao. Na watoto wake nitawaua kwa mauti; na makanisa yote yatatambua ya kuwa mimi ndimi nichunguza nia na mioyo...”

8. Ufunuo 19:15
“Na kutoka kinywani mwake hutoka upanga mkali, ili awapige mataifa kwa huo; naye atawachunga kwa fimbo ya chuma...”
 
unataka kusema nn?
 
Yaani kwa zaidi ya vitabu maelfu kwa mamia wewe ulichofanikiwa kukisoma ni biblia tu labda na Quran sababu hii nchi tuna dini kuu hizi mbili alafu unahitimisha kwa kudai hicho ndicho kitabu cha upendo wakati huo hujui kilichomo ktk vitabu vingine.

Haya tueleze kuna dini inasisitiza upendo zaidi ya Ubudha+uhindu?, ushawai ona wapi wahindu+wabudha waliuwa maelfu ya watu kisa maandiko na tofauti za kidini kama ilivyofanya hiyo biblia yenu?

Yaan wajinga hii nchi hawawezi kuisha jinsi unavyoisifia hiyo biblia hata aliyezaliwa ktk uislamu na kuijua Quran anaisifia the same way unavyofanya, hakuna maajabu hapo.

Kila mtu akileta mahaba ya kitabu chake sidhani kama kutakuwa na amani zaidi ya mitifuano, maana dini zote zinavutia upande wake.

Dini zote na vitabu vyake zimeundwa kwa manufaa ya watu wachache kuwatala wengi, biblia ingakuwa na maana sana basi upendo ungeanzia huko huko makanisani mlikojazana wezi, majambazi washirikina, wanafiki, wauwaji, wachoyo, walafi na tabia za kila aina.

Huwezi kuupata upendo kupitia dini wala kitabu cha dini, upendo wa kweli ulishakufa baada ya ujio wa hizi TAKATAKA za ukristo na uislamu kutawala fikra za watu weusi,
Nina uhakika hata wewe mtoa mada ukikutana na wahitaji wawili wa dini ya uislamu na ukristo, nina hakika utamsaidia wa dini yako maana hayo ndio mafundisho ya hizi TAKATAKA zenu zilizoleta huu ubaguzi.

Biblia ingekuwa ya maana sana basi sadaka makanisani zingepungua kwa kuanzia/kuwawezesha masikini na wahitaji wa mitaani badala yake mnawaacha hawa wahitaji mnapeleka pesa kwa hao majambazi wanaojiita mitume, manabii, wachungaji.

Biblia+Quran ni siraha za kuharibu akili ya mtu mweusi, huwezi kuupata uzima kwa kuamini hizi ngonjera za wazungu.
 
Hoja yako ni nini?

Biblia sio chuo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…