Biden awache kumtusi Putin. Hatutaki vita ya tatu ya dunia

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Baada ya raisi Putin wa Urusi kutangaza rasmi kuyameza majimbo 4 ya Ukraine hapo jana,rais Joe Biden amesema Marekani haitishwi na maneno ovyo ya Urusi.

Maneno hayo anayokusudia Biden yanaweza kuwa siku mbili kabla ya tangazo la matokeo ya kura za maoni aliyosema Putin kuwa Urusi ina silaha za aina zote za maangamizi na inaweza ikazitumia.

Akaongeza kwa kusema kuwa hatanii kwa hilo. Na zaidi ya hayo Putina akakumbusha kuwa Marekani ndio ya mwanzo kutumiza silaha za nyuklia kumaliza vita ya pila ya dunia ilipoipiganazo Japan.

Kama kwamba na yeye anataka kuzitumia kumaliza vita ya Ukraine.

Mtu (Putin) anayesema hayo na kweli vitu hivyo anavyo si wa kumchezea wala kumkasirisha zaidi.

Vitisho vyake kama hivyo na dharau raisi Biden afanye kwa mataifa ya dunia ya tatu sio kwa mbabe mwenzake.

1664602350961.png
 
Sio kisa wewe ni muoga ukataka lazimisha jamii nzima inayokuzunguka kuishi kama chawa… naionea huruma sana familia yako kama unayo aiseee, yawezekana ukigongewa na fogo unamute kama haupo vile… kama naisikia Boss ya Ferooz vile….aseee “Usione tumekonda ukadhani mateja…” in Kibla’s voice…
 
Putin ni hovyo tu ndivyo tunavyofahamu wengi wetu na kwa ujinga wake anatishia watu nyuklia wakati anafahamu fika kwamba wenzake wana nyuklia hatari kuzidi hizo alizonazo.

Katika dunia ya sasa huwezi ukafanya ujinga ukategemea watu wakuchekee tu kisa eti una nyuklia, hamna kitu kama hicho. Putin bure kabisa.
 
Kama wewe ungekaribia hicho cheo cha Putin basi ingekuwa hatari.Suala sio wenzako kuwa nazo kama za kwako.Tunazungumzia nyuklia ambazo hata ukiwa nazo mwenzako akizitumia mwanzo basi hizo za kwako hazina maana tena.Mwenye nyuklia kama hizo ama uende naye kwa hekima au umnyamazie kimya sio kumtukana.
 
Nani anakudanganya kwamba nyuklia ukiitumia mwanzo mwingine hawezi kukujibu. Unafikiri ni kwa nini wanasema There is no winner in nuclear war.!!
 
Kumbe unajua hakuna mshindi kwanini huoni shida mwenzako akitumia kabla yako.Itakuwa umepata hasara na yeye amepata hasara.Na unalosema pia halina mashiko. Fikiria hiyo nyuklia ikitua Newyork au washington mwanzo.Nani atakayeinuka kwenda kubonyeza kitufu cha kufyatua nyuklia yake.Hivyo uwezekano wa anayetumia mwanzo kuwa mshindi au atakayetia hasara kubwa upo.Kumbuka wakati Marekani alipondosha nyuklia Hiroshima na Nagasaki.Wajapani wote waliloa hawakujua nani aseme nini.Ikaonekana hakuna haja wala nguvu tena ya kuendelea na vita.
 
Baada ya raisi Putin wa Urusi kutangaza rasmi kuyameza majimbo 4 ya Ukraine hapo jana,rais Joe Biden amesema Marekani haitishwi na maneno ovyo ya Urusi.

Maneno hayo anayokusudia Biden yanaweza kuwa siku mbili kabla ya tangazo la matokeo ya kura za maoni aliyosema Putin kuwa Urusi ina silaha za aina zote za maangamizi na inaweza ikazitumia.

Akaongeza kwa kusema kuwa hatanii kwa hilo. Na zaidi ya hayo Putina akakumbusha kuwa Marekani ndio ya mwanzo kutumiza silaha za nyuklia kumaliza vita ya pila ya dunia ilipoipiganazo Japan.

Kama kwamba na yeye anataka kuzitumia kumaliza vita ya Ukraine.

Mtu (Putin) anayesema hayo na kweli vitu hivyo anavyo si wa kumchezea wala kumkasirisha zaidi.

Vitisho vyake kama hivyo na dharau raisi Biden afanye kwa mataifa ya dunia ya tatu sio kwa mbabe mwenzake.

View attachment 2373424
Huyu Mzee bure kabisa
 
Kumbe unajua hakuna mshindi kwanini huoni shida mwenzako akitumia kabla yako.Itakuwa umepata hasara na yeye amepata hasara.Na unalosema pia halina mashiko. Fikiria hiyo nyuklia ikitua Newyork au washington mwanzo.Nani atakayeinuka kwenda kubonyeza kitufu cha kufyatua nyuklia yake.Hivyo uwezekano wa anayetumia mwanzo kuwa mshindi au atakayetia hasara kubwa upo.Kumbuka wakati Marekani alipondosha nyuklia Hiroshima na Nagasaki.Wajapani wote waliloa hawakujua nani aseme nini.Ikaonekana hakuna haja wala nguvu tena ya kuendelea na vita.
Wewe nenda ukaswali hakuna unachofahamu kwenye mambo haya kwa sababu hujui kwamba ufyatuaji wa nyuklia kati ya Russia na Marekani ina reciprocal effect ya kwanza ikirushwa nyingine hujibu automatically.
 
Mimi umesema sielewi kitu.Na wewe unajidai tu ni ovyo kuliko mimi na hueleweki unakusudia kusema nini. Ya kwanza ikirushwa na nyingine hujibu automatically..Hii ina maana gani.
Hebu fafanua kidogo kama kweli unajua unachokisema.
 
Biden ni kichaa kuwahi kutokea Marekani.

Wala tusishangae, mara ngapi tumemuona Biden live ikitoa mkono kusalimia watu ambao hawapo (hewa), hakumbuki jana alisema nini!! Leo hii binadamu mwenye mapungufu ya kuchambanua mambo kwa kina, anakabidhiwa briefcase yenye CODE ya kufyatulia ICBM zenye nuclear payloads!!
 
Wewe nenda ukaswali hakuna unachofahamu kwenye mambo haya kwa sababu hujui kwamba ufyatuaji wa nyuklia kati ya Russia na Marekani ina reciprocal effect ya kwanza ikirushwa nyingine hujibu automatically.

Sijui unamaanisha nini mkuu, hisipokuwa ninacho kijua mimi ni kwamba taifa pekee lenye mfumo wa DEADMAN'S HAND ni Urusi - kazi ya mfumo huo ni kwamba in case taifa la Urusi linapigwa ghafla/shitukizwa na missiles/mabom ya nuclear Warusi wote wakafa/angamia pamoja na infrastructures zao zote mfumo huo umewekewa sensors/transducers za kutambua/baini kwamba taifa la Urusi limeshambuliwa kwa silaha za nuclear hivyo mfumo huo una uwezo mkubwa wa kufyatua missiles zilizo hifadhiwa kwenye silos na submarine kwenda kushambulia Amerika hata kama Warusi wote wamekufa, mfumo huo unajifyatua automatically, hicho ndicho nakijua mimi.
 
Back
Top Bottom