Bidhaa za kutoka Kenya zina usalama kweli? Kwa kiwango gani?

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,988
Reaction score
30,183
Wakuu Kwema,

Nimewaza Tanzania tunatumia Bidhaa nyingi sana kutoka Kenya. Za matumizi ya ndani ya Mwili wa Binadamu, mpaka matumizi ya nje ya Mwili wa Binadamu na matumizi mengine. Kuanzia Dawa za Meno, Mafuta ya Kupaka, Dawa za Viatu (KIWI), etc.

Nawaza tu hivi vitu vina usalama gani kwa Binadamu? Dawa za Meno hata tukiosha kinywa baada ya kutumia dawa hizi bado kuna mabaki tu yatabaki mdomoni. Na pia mafuta ya kupaka tunayotumia vipi usalama wa ngozi wetu? Mafuta yametumia Kemikali gani kutengenezwa?

Kuna Biscuits, Pipi, Juice, Maziwa na vitu vingine vingi tu tunatumia kutoka kwa hawa Jirani zetu, usalama wake ukoje? KIWI nayo ikigusa ngozi zetu haina madhara?

Nadhani umefikia wakati sasa Serikali kuzuia "importation" ya hizi bidhaa mpaka kwanza ichunguze usalama wake. Uchunguzi ufanyike polepole tu hata kwa miaka mitano au zaidi haina haja ya kuharakisha ili matokeo tutakayoyapata based on uchunguzi huo yawe ni matokeo sahihi.
 
Muda si mrefu majibu yatapatikana. Muda huu wazee wa fitna nao wamejifungia huku wakitafakari namna ya kujibu mashambulizi.

Just wait and see! Katika hizi fitna, hakika serikali ya magufuli haijawahi kushindwa. Wako vizuri kweli.
 
Ahsante Mkuu,
Vyote hivi na vya kupiga BAN mpaka tujue usalama wake kwanza
Mmejiandaa au ndio kukurupuka, wenzenu walipotaka kupiga ban mahindi walijiandaa kwanza
 
Ahsante Mkuu,
Vyote hivi na vya kupiga BAN mpaka tujue usalama wake kwanza
Mmejiandaa au ndio kukurupuka, wenzenu walipotaka kupiga ban mahindi walijiandaa kwanza.
 
Mmejiandaa au ndio kukurupuka, wenzenu walipotaka kupiga ban mahindi walijiandaa kwanza
Hatutakosa kwengine pa kuagiza, hata China poa tu
 
Itakuwa ni upuuzi. Maana Tbs tutawauliza walikuwa wapi kubaini hizi defects?
Mkuu,

Hata Wao mahindi ndo haya haya wanayatumia miaka na miaka, wanavyosema yana sumu "TBS" ya kwao ilikua wapi miaka yote hiyo?? Defects hazitaweka na TBS, bali wao watapewa tu order waseme nini? Yaan hii issue ni beyond TBS capacity.

Hapa wao wamebip acha na sisi tuwapigie tu
 
Sisi ni Nchi ya uchumi wa kati, tungeomba ripoti ya uchunguzi wa kisayansi ambayo wakenya wameifanya, na ushahidi wa sample (specimen) walizotumia kama kweli zimetoka TZ. Donor country huendesha mambo yake kisayansi.
 
Mkuu sio kila bidhaa inakuja na ndege.

Kwanza Usafiri wa ndege ingawa ni wa haraka lakini ni gharama mno. Mizigo mingi mikubwa mikubwa ya kibiashara kutoka China huingia nchini kupitia usafiri wa majini.

Hawa mpaka waombe Poo.
 
Unaonyesha ulivyo mweupe kichwani! Kwani TBS yenu ina kazi gani au wamelala usingizi wa pono?
Mkuu sidhani kama hata umeelewa msingi wa mimi kuandika hicho ulicho-quote. TBS iweke pembeni kwenye hili, ni beyond their level.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…