Swala la kuprinti chochote chenye Brand yako unaweza, issue ni quality yako na idadi ya mashabiki wako!
Flaviana yeye alikuja na Idea ya kusaidia watoto wa shule kwa michango mbalimbali ya wadau waliokuwa wanajitolea!
Tena shule nyingi ilikuwa ni Msingi,
Jokate ameanzia ktk Nywele na Mitindo Mingine Mingi, Alianza kwa kukarabati uwanja wa Basket Jangwani, Sasa inawezekana amewaona wadogo zake hawana Bags za kueleweka kwa ajili ya shule na vyuo mbalimbali kaamua kuwaletea ili wajivunie, Wote ni watanzania tunapaswa kuwapa support! Msichana mwenye ndoto ni Moto wa kuotea mbali!
Binafsi nimevaa sana Adidas, Nike, Jordan, hawa wote wanatoa kwa sababu wanajua wana mashabiki!
Ni kama Tshirts za Man U, Arsenal, Yanga, Hizi ni Biashara lakini zinategemea Mashabiki!
Kama ambavyo wema sepetu alivyotengeneza Ndala,
Kama walivyotengeneza WCB zile za TIPTOP CONNECTION na za ALIKIBA
Kama alivyotengeneza JUX na Shetta
Wapeni sapoti Vijana wetu
Kesho na kesho kutwa me naibuka na kiwanda cha kutengeneza viatu vya Ngozi na Raba kalii zenye lebo tofauti tofauti na rangi tofauti halafu unaambiwa umeiba wazo, siyo kweli! Tusichukiane watanzania kwa mambo madogo.