Big Brother Africa 2009: The Revolution


Kweli jamani dunia hii ina watu wa kila aina! mwaka jana yule dada Latoya alikuwa angawa uroda ,wakamtukana weee mpaka basi.Sasa Eliza naye anatunza maadili naye mnasema anaboa mnataka mgawaji.tuwaweke kundi gani enyi binadamu?mbona hamueleweki!? Aaargh!
 
Hata hivyo amechelewa sana kutoka, alistahili kutoka mapema zaidi. Amshukuru Kevin kwa kumbeba kipindi wako kama 'comrade in arms'.

Alikuwa ana bore sana, ishu ndogo tu ye anapanic!! Akiambiwa 'I love you' ye ananuna!! Mwache atoke, we need housemates who can entertain us bcoz we are paying!!

Aende zake kwa mabwana zake wa kizungu!!! Aliniudhi sana, one day alisema eti she dont find confortable dating black guys!!
 
Poole muzee
Poole muzee
kwa kufungwa!😀

Docebit VOS Omnia......mimi simo humo.......nyati kajeruhiwa.......ha!ha!ha!ha!!

On the other hand poleni sana washabiki na wapenzi wa BBA mkiongozwa na BBA star ...Mbogela pamoja na mwenyekiti wa kamati ya ushindi.....Keil!
 

inatia huruma! wabongo kwa mtindo huo wa kuwa kama ndumi la kuwili hatutafika popote!
 

suala la kulipia show halina umuhimu kama vipi acha kulipia! hauko peke yako! mzamo anavyojiachia wengine wanasema oooh she is cheap! aaagr wabongo bana! kazi kweli kweli. for your information unaweza kuwa entertained hata bila kulipia! akili ku mkichwa!
 
Fimbo uliyoitumia kumtandika pacha wa Eddy hatimae imekutandika.Alliance imemponza Eliza alimswap Pacha wa addy sasa naye yamemkuta.
 
Docebit VOS Omnia......mimi simo humo.......nyati kajeruhiwa.......ha!ha!ha!ha!!

On the other hand poleni sana washabiki na wapenzi wa BBA mkiongozwa na BBA star ...Mbogela pamoja na mwenyekiti wa kamati ya ushindi.....Keil!

Mkuu tunashukuru kwa Pole, Dada yetu alijitahidi, mimi naamini angeweza kuchukua huu mrungura angetulia, alikuwa na nafasi kubwa sana, angeaacha kufuata maelekezo ya akina Paloma na Emma (Alliance) Pia angeonyesha ukomavu wa kuhandle issue ikiwa wanaume wanaomtaka na yeye hayupo tayari kuwa nao, aache kulia lia kila anapopata hisia za huruma. Nadhani Elizabeth ametufundisha mengi zaidi, tukichanganya character ya Richard, Latoya, Elizabeth naamini sasa tunajua mtu anayetakiwa kwenda huko afanyaje. Mwisho Mwampamba hatumsemi sana kwani yy BBA yao ilikuwa ya kwanza na haikuwa na mvutano mkali kama hizi zilizofuata.

Sister Elizabath karibu home, Jina lako limeshakuwa kubwa kwa hiyo ni namna utakavyotumia kukusaidia kwa manufaa yako.

washabiki wa BBA mimi na Keil tutaendelea mpaka Mtanange utakapoisha ndio tutaifunga hii thread ha ha ha
 
BHAGOSHA,

Tatizo letu sie watanzania ni tokea juu kwa viongozi wenye mamlaka ya kufanya kitu na hupenda kufanay mambo kwa interest zao wajua kwanini wanaigeria wanatushinda hata kwa upigaji kura kwenye Big Brother na sio tu huko ni kwenye matamsha mengi mfn:Big Brother, Chanel O wakiandaa Awards, Juzi yu hapa MTV Mama Africa Awards,Tusker Project Fame, yani sie tuwa wasemaji sana, Ila mbali ya yote hii ni inatokana na Uongozi wa ajabu katika sector hizi ndani ya Nchi yetu DSTV,TBC,VODACOM,TIGO,ZAIN,ZANTEL, kwanini nimewasema hao ni kuwa wao wanamiliki asilimia kubwa ya mawasiliano kuto nchi tuliopo kwenda kwa wenzetu i mean customer care ni duni sana wenzetu huko Nigeria Dstv zimetapakaaaaa tena kwa bei rahiiiisi sana wakuta like 75% ya Nigerian they can watch kila matukio yoyote duniani na kutoa hata hoja kwa kutumia TV's na Simu bei huko ni cheeeep sana katika swala la mawasiliano ila hapa kwetu kutuma tu SMS kwenda Big bro ni Tsh 600 kwa hali hiii mtanzania ata weza kweli Lets be Honesty hapa na tusijaribu kudanganyana ni kuwa twapenda kudandia Train kwa mbele ni kuiga full kila jambo. Maisha Plus ya Bro Masoud tu hapa hata kutuma sms ni taaabu kweli kweli.

Me naomba sana wale Viongozi wenye nyadhifa za juu na mamlaka ya kuamua mambo wajaribu kufunguka macho kwa niaaba ya Taifa na sio kwa niaba yao wenyewe au kwa maslahi ya mtu fulani au fulani kuwa na Customer care kwa ajili ya maslahi ya watanzania wote na wananchi ndio wanao changia sn kukuwa kwa hizo sector zao na kuwaingizia kipato kwanini wasitupe burudani ya kutosha nasi tukwa ka Wanigeria na nchi zingine basi SMS to big Bro Africa TSh 600 Kweliiiiiii Jamani
 
Afrika haikupendezwa na kauli yake kwamba hajawahi kuwa na uhusiano na mwanaume mweusi. Eti yeye mabwana zake ni whites tu. Alikuwa akimkataa Kevin aliyeonyesha kumpenda kwa dhati. Kwa maoni yangu kauli hii iliwaudhi waAfrika wengi kiasi cha kupoteza kura nyingi za kubaki ndani ya jumba. Hakuwa na sababu ya kumwambia vile Kevin. Katika hili yeye angeweza ku-pretend huku akijua msimamo wake.
 

ZD,

Tatizo siyo maadili, na ninaomba nikurekebishe. Mwaka jana Latoya hakugawa uroda kama wewe ulivyoweka hapo juu. Ni watu ndiyo waliozusha, baada ya Latoya kumuacha Morris na kwenda kwa Ricco. Wala hakugawa uroda kwa Morris ingawa kulikuwa na dalili zote kwamba kama angebaki kwa muda mrefu may be angeweza kugawa uroda kwa Ricco.

Tatizo la Eliza ni kwamba alikuwa too moody, huwezi kujua ni wakati gani mzuri wa kuongea nae. Ndiyo maana siku zote alikuwa anagombana na Kelvin. Hilo la kugombana na Kelvin kila siku ndio ambayo lilifanya apoteze kila na watu wakaanza kumchukia na kuona hafai.

Kushindwa kwa Eliza hakuna uhusiano wowote na kutunza maadili, labda aseme kwamba alikuwa anampenda Kelvin na alikuwa anaogopa kuwa nae close kwa kuwa angeweza kumgawia uroda. Jana alisema kwamba kujiweka karibu na mtu kama Kelvin na huku nje una mtu wako, ni hatari sana. Na akasema akipata mwanaume kama Kelvin huku mtaani she can go for him.

Kwa kifupi, hajui kuishi na watu. Iwe ni wasichana wenzake ama wavulana na ndiyo maana wengi ambao alijichanganya nao aliishia kugombana nao ama kujenga chuki dhidi yao.
 
Docebit VOS Omnia......mimi simo humo.......nyati kajeruhiwa.......ha!ha!ha!ha!!

On the other hand poleni sana washabiki na wapenzi wa BBA mkiongozwa na BBA star ...Mbogela pamoja na mwenyekiti wa kamati ya ushindi.....Keil!

Aliyemchagua Eliza alichemsha sana, labda alitumia kigezo cha kiingereza na hakujua hayo matatizo mengine. Kuishi kwenye jumba na watu wenye culture/malezi/makuzi tofauti ni ngumu. Tunahitaji kuwa na mwakilishi ambaye ni flexible na asiwe strict sana. Ukiwa strict sana utagombana na kila mtu.

Kuna kajamaa kalikuja toka Botswana kwenye BBA2, kalishindwa kuishi humo ndani mpaka kakawa kanataka kuondoka. Bahati nzuri kalikuwa nominated hiyo wiki, so wapiga kura wakampa ride ya kutoka. Kosa lilikuwa dogo sana, aliambiwa na mshiriki wa Namibia (binti) kwamba angem-spank ass yake. Kwake hilo lilikuwa ni tusi kubwa sana, akasema kwao wanaume wanaheshimiwa sana na hawawezi kuambiwa hayo maneno.

So, tuwaombe mwakani watuchagulie mwakilishi mzuri ambaye anaweza kuwa flexible na asiwe anachukulia kila kitu seriously mpaka inakuwa ni kero.

Tutaendelea na libeneke hapa mpaka tuone mshindi hapo December mwanzoni.
 
Fimbo uliyoitumia kumtandika pacha wa Eddy hatimae imekutandika. Alliance imemponza Eliza alimswap Pacha wa addy sasa naye yamemkuta.

Alliance ilimtumia, na hayo ndo matatizo ya alliance. Unakubaliana na strategy ambayo haina manufaa kwako, may be ina manufaa kwa yule anaetoa hilo wazo. Eliza alijua kwamba kumtoa twin mmoja ni kujenga uadui kwa twin mwingine, lakini bado akaingia kichwa kichwa na jamaa hakuficha alisema wazi kwamba alikuwa analipa kisasi.
 
Nominations za leo:

Edward: Itai & Leonel
Geraldine: Itai & Leonel
Nkenna: Itai & Leonel
Itai: Leonel & Emma
Mzamo: Itai & Leonel
Kevin: Mzamo & Edward
Emma: Nkenna & Geraldine
Leonel: Geraldine & Nkenna

Preliminary Results:

Itai - 5
Leonel - 4
Geraldine - 2
Nkenna - 2
Eddie - 1
Mzamo - 1
Emma - 1

Tusubiri maamuzi ya BB kwamba ataweka wangapi na pia maamuzi ya Eddie ataokoa nani na atamtosa nani.

Ile informal alliance naona imejitokeza kwenye pattern ya nominations zao. Mzamo, Nkenna, Geraldine na Eddie wamewa-nominate watu wale wale. Kelvin na Emma wame-part ways, kila mmoja ka-nominate kivyake.

Itai na Leonel inaonekana hawakupata access ya kupiga kambi mahali popote. Hii inawezekana imetokana na kusambaratika kwa alliance ya akina Emma. Itai alijaribu kwenda kwa Nkenna jana, lakini akaambiwa kwamba Nkenna is done with alliances na ameamua kwenda solo. Nkenna ndiyo alikuwa link ya Itai kwa akina Eddie, lakini Eddie hana imani na Itai. Pia Itai alienda kwa Kelvin jana, Kelvin akaomba aachwe peke yake. Matokeo yake wamebaki wana hang.

Lakini nina mashaka Leonel na Emma waliongea, na makubaliano yao hayakumhusisha Kelvin kwa kuwa asingekubali kushiriki kutoa vichwa viwili vya dada zake na ilhali alikuwa na kazi ya kulipa kisasi kwa Eddie na Mzamo.

Ngoja tusubiri saa moja jioni tuambiwe ni wangapi wako up na Eddie atafanya mabadiliko gani.
 
News: Eddie Puts Kevin Up

Big Brother reveals to Housemates that Leonel and Itai are up. The Head of House, Edward, is asked to go to the Diary Room to make his switch.

Edward saves Itai and replaces him with Kevin. Kevin has said to Big Brother that he feels that Edward is his biggest competition in the House. Kevin's love interest, Elizabeth, was Evicted this past Sunday.

Edward, during his first tenure as Head of House, replaced Mzamo with Elizabeth. The switch was Edward's way of getting back at Elizabeth for being instrumental in getting his twin brother, Erastus, out of the House.

Leonel and Kevin are now up for Eviction.
 
Eddie anazidi kuimaliza kambi ya Kelvin. Leonel alishaamua kuingia kwenye alliance ya Emma. Sasa come Sunday, either Kelvin or Leonel will walk.

Nilimsikia Emma kwenye diary session akisema wameamua kila mtu kivyake, lakini inaonyesha Emma na Leonel waliongea na kukubaliana ila hawakumshirikisha Kelvin.

Kitendo cha Eddie kum-save Itai automatically kinamfanya Itai awe loyal kwa kambi ya Eddie, japo Itai siyo mtu wa kumwamini sana. Akina Kelvin na wao wanasema hawamwamini wamembatiza jina la Politician na kwamba ni muongo muongo sana.

Kelvin amepewa njia nyeupe sana, I wish wiki hii angesimama na Eddie. Lazima angerudi kwao. Lakini kitendo cha kusimama na Leonel sioni kama Kelvin atapata shida ku-win.

Labda kama SADC wataamua kupiga kura kikanda kwamba nchi zipige kura kulingana na alliance Eddie & Mzamo + Nkenna na Geraldine (ambao hawatoi advantage yoyote kwenye alliance in terms of kura za nje).

Leonel angekuwa hana matatizo sana angetoa ushindani kwa Kelvin kwa kuwa kuna nchi zinataka kichwa cha Kelvin strategically na wengine ikiwa ni kisasi. Nchi kama Malawi, Uganda, South Africa, Namibia, Ethiopia, Zimbabwe na Mozambique zingemuunga mkono kama kijana angekuwa ana-entertain. Lakini kwa mwelekeo ulivyo sioni dalili ya jamaa kufurukuta.

Tusubiri matokeo Jumapili, lakini yako more predictable.
 

hili la kwamba eti hatupendi sisi mablack limeniudhi! sasa hebu arudi atuambie vizuri!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…