Jamani mbona siwaelewi hawa? wanabishana nini? naomba msaada jamani.
http://beta.mnet.co.za/mnetvideo/browseVideo.aspx?vid=20848
Leonel hana akili na ndiye aliyesababisha yote. But Mzamo nae ana mchango wake kwenye haya mabishano.
Leo alianza kumtongoza Gerry, akakataliwa. Gerry akawa rafiki wa K1. Then Mama Ushauri (Nkenna) akamuonea huruma Leo kwamba alikuwa anaumia, akamwambia forget about Gerry na hata ukiwaona wako na K1, ni urafiki wa kawaida. Baada ya ushauri huo, Nkenna akamshauri Leo kwamba Mzamo yuko available kama Leo yuko interested anaweza kumuunganishia. Leo akacheka sana, akasema labda kama ni Nkenna mwenyewe lakini si vinginevyo. Nkenna akasema NO, yeye ni dada.
Ukaja u-comrade in arms, ukawaunganisha Leo na Mzamo. Nkenna akamropokea Mzamo kwamba Leo ana interest ila he is a shy guy ndo maana hajasema. Mzamo akaenda kumuuliza Leo, Leo akakubali. Ni kama Mzamo alijilengesha kwa Leo na Leo kwa kuwa alikuwa anahitaji some, akajua ngoja a-take advantage na akafanya kweli. Shida yake ilipoisha akawa hamhitaji tena Mzamo.
Leo na Mzamo walipofanya mara ya kwanza ilikuwa ni siri. Mara ya pili walifanyia kwenye chumba cha kulala, so kila mtu aliwaona na alijua kwamba wamefanya. Baada ya hapo Leo akasema hataki tena, lakini Mzamo bado alikuwa na interest. Mojawapo ya vitu ambavyo vilimfanya Leo aache ni kutaka kumfuatilia tena Gerry kwa kuwa K1 alikuwa avicted. Asingeweza kumfuatilia Gerry wakati bado yuko na Mzamo, so alihitaji ku-break kwanza ndipo aanzishe mashambulizi.
Mzamo alipotaka kujua kwanini kijana alikuwa anataka ku-break, kijana hakutoa jibu la kweli, Mzamo akamwambia bado yuko kwenye denial kwa kuwa anaonekana bado ana interest kwa Gerry, na hivyo Mzamo akamruhusu asonge mbele na kila mmoja ashike njia yake. Wakakubaliana waendelee kuwa marafiki wa kawaida tu.
Kwenye hiyo clip, kajamaa kalikuwa kameanza kumwingia Gerry kwa mara ya pili ndipo Gerry akawa anamwambia kwamba hakumtendea vyema Mzamo na kwamba alimtumia na kum-dump. Leo anajitetea kwamba waliongea na kuubaliana kufikia mwisho na ndipo Mzamo akaingia ku-clarify.
Kwa kifupi Moz Boy (Leo) ni mjinga sana, yaani alitaka kuwachanganya wakiwa ndani ya Jumba na alitarajia Gerry amkubali wakati aliwaona na alisikia kwamba wamefanya kabisa. Labda kama angemtaka baada ya Mzamo kutoka na pia inategemeana, kama Gerry alikuwa na interest na pia kama hawaufanya. Lakini kama walishafanya na watu wote wakawa wanajua na waliwaona, hapo lazima na msichana nae akikubali atakuwa anajidhalilisha.