Big Brother Africa 2009: The Revolution

Big Brother Africa 2009: The Revolution

News: Itai Wins HoH

huyu jamaa kila wakitoa task ya kutumia ubongo lazima ashinde.
 
News: Itai Wins HoH

huyu jamaa kila wakitoa task ya kutumia ubongo lazima ashinde.
.....yeah....he is smart but a cunning snake......iam a kevin supporter sasa huyu jamaa hatabiriki so i can't say if King Kev is safe or not 🙁
...hehehehe...i tried the riddles without looking at the answers and got 7 out of 12 ...not bad 🙂...anywaiz...to the Kevin fans lets just wait n c wat happens....hehehehe...Mzamo better get ready to be up nxt week for sure...hehehe..i wonder who will start kissing Itai's ass today??....
 
Kelvin wenu atakuwa salama wiki ijayo.

Alliance ya Eddie itawa-nominate Itai na Emma, then Itai atajiokoa mwenyewe. Kitendawili ni replacement ... I guess Mzamo, Nkenna or Geraldine. Lakini most likely anaweza kuwa Mzamo.
 
off topic: Mbogela, Triplets na NL .... kumbe mnaongea lugha ya Taifa la Tuntemeke!
Na wakinga wote tuna Degree saba ha ha ha ha hakuna kazi tunaweza kufanya hapo bongo ndio maana tunakaa huku huku kwetu ha ha ha
 
Jamani kuna task zingine zinachekesha, niecheka hawa jamaa wanavyoimba revolution blues sikiliza jamaa anavyopiga ngoma kama hajawahi kuona ngoma zinavyopigwa kabisa, alafu sauti ya Itai yaani kama ya bundi jamani ha ha ha yaani jamaa wamenichekesha maana wamenikumbusha mambo ya kilabu ya Mfaranyaki
http://beta.mnet.co.za/mnetvideo/browseVideo.aspx?vid=21023
 
Jamani mbona siwaelewi hawa? wanabishana nini? naomba msaada jamani.
http://beta.mnet.co.za/mnetvideo/browseVideo.aspx?vid=20848

Leonel hana akili na ndiye aliyesababisha yote. But Mzamo nae ana mchango wake kwenye haya mabishano.

Leo alianza kumtongoza Gerry, akakataliwa. Gerry akawa rafiki wa K1. Then Mama Ushauri (Nkenna) akamuonea huruma Leo kwamba alikuwa anaumia, akamwambia forget about Gerry na hata ukiwaona wako na K1, ni urafiki wa kawaida. Baada ya ushauri huo, Nkenna akamshauri Leo kwamba Mzamo yuko available kama Leo yuko interested anaweza kumuunganishia. Leo akacheka sana, akasema labda kama ni Nkenna mwenyewe lakini si vinginevyo. Nkenna akasema NO, yeye ni dada.

Ukaja u-comrade in arms, ukawaunganisha Leo na Mzamo. Nkenna akamropokea Mzamo kwamba Leo ana interest ila he is a shy guy ndo maana hajasema. Mzamo akaenda kumuuliza Leo, Leo akakubali. Ni kama Mzamo alijilengesha kwa Leo na Leo kwa kuwa alikuwa anahitaji some, akajua ngoja a-take advantage na akafanya kweli. Shida yake ilipoisha akawa hamhitaji tena Mzamo.

Leo na Mzamo walipofanya mara ya kwanza ilikuwa ni siri. Mara ya pili walifanyia kwenye chumba cha kulala, so kila mtu aliwaona na alijua kwamba wamefanya. Baada ya hapo Leo akasema hataki tena, lakini Mzamo bado alikuwa na interest. Mojawapo ya vitu ambavyo vilimfanya Leo aache ni kutaka kumfuatilia tena Gerry kwa kuwa K1 alikuwa avicted. Asingeweza kumfuatilia Gerry wakati bado yuko na Mzamo, so alihitaji ku-break kwanza ndipo aanzishe mashambulizi.

Mzamo alipotaka kujua kwanini kijana alikuwa anataka ku-break, kijana hakutoa jibu la kweli, Mzamo akamwambia bado yuko kwenye denial kwa kuwa anaonekana bado ana interest kwa Gerry, na hivyo Mzamo akamruhusu asonge mbele na kila mmoja ashike njia yake. Wakakubaliana waendelee kuwa marafiki wa kawaida tu.

Kwenye hiyo clip, kajamaa kalikuwa kameanza kumwingia Gerry kwa mara ya pili ndipo Gerry akawa anamwambia kwamba hakumtendea vyema Mzamo na kwamba alimtumia na kum-dump. Leo anajitetea kwamba waliongea na kuubaliana kufikia mwisho na ndipo Mzamo akaingia ku-clarify.

Kwa kifupi Moz Boy (Leo) ni mjinga sana, yaani alitaka kuwachanganya wakiwa ndani ya Jumba na alitarajia Gerry amkubali wakati aliwaona na alisikia kwamba wamefanya kabisa. Labda kama angemtaka baada ya Mzamo kutoka na pia inategemeana, kama Gerry alikuwa na interest na pia kama hawaufanya. Lakini kama walishafanya na watu wote wakawa wanajua na waliwaona, hapo lazima na msichana nae akikubali atakuwa anajidhalilisha.
 
Na wakinga wote tuna Degree saba ha ha ha ha hakuna kazi tunaweza kufanya hapo bongo ndio maana tunakaa huku huku kwetu ha ha ha

ha ha ha ha ha ha ha ... umenikumbusha mbali sana. ipo kazi moja tu ambayo mnaweza kuifanya, ni ile ya u-JK. siku hizi wakinga wenye madigirii 7 wamekuwa wengi sana, sijui mtakuwa mnapokezana, kila mmoja miaka miwili miwili?
 
Jamani kuna task zingine zinachekesha, niecheka hawa jamaa wanavyoimba revolution blues sikiliza jamaa anavyopiga ngoma kama hajawahi kuona ngoma zinavyopigwa kabisa, alafu sauti ya Itai yaani kama ya bundi jamani ha ha ha yaani jamaa wamenichekesha maana wamenikumbusha mambo ya kilabu ya Mfaranyaki
http://beta.mnet.co.za/mnetvideo/browseVideo.aspx?vid=21023

Task ya wiki hii BB alichemsha haikuwa na mvuto na hata housemates wenyewe hawakuvutiwa sana. Hata hiyo 100% aliyowapa ni kwamba aliwapendelea baada ya kugundua wamba alichemsha.
 
Kwenye hiyo clip, kajamaa kalikuwa kameanza kumwingia Gerry kwa mara ya pili ndipo Gerry akawa anamwambia kwamba hakumtendea vyema Mzamo na kwamba alimtumia na kum-dump. Leo anajitetea kwamba waliongea na kuubaliana kufikia mwisho na ndipo Mzamo akaingia ku-clarify.

Kwa kifupi Moz Boy (Leo) ni mjinga sana, yaani alitaka kuwachanganya wakiwa ndani ya Jumba na alitarajia Gerry amkubali wakati aliwaona na alisikia kwamba wamefanya kabisa.

Mkuu asante sana, yaani hadithi imekuwa tamu sana, yaani katika ujinga watu wanafanya ni pamoja na huu wa Leo, sio rahisi hata siku moja ukachovya kwenye chungu hiki alafu wakati hata hakijaoshwa unataka kuchovya kingine ha ha yaani hapo ni buti tena buti la jeshi. Sasa mzamo sasa hivi ananafsi na nani? nimejaribu kufuatilia clips sioni maendeleo?
 
Sasa mzamo sasa hivi ananafsi na nani? nimejaribu kufuatilia clips sioni maendeleo?

Mzamo siku hizi ana "emotional husband" ambaye ni Eddie, lakini sio kivile ila wako close sana. Eddie kama angemtaka Mzamo angemchukua siku nyingi sana kwa kuwa Mzamo alishajilengesha mara kibao.

Pia Mzamo hakuonyesha kuwa consistent alikuwa confused. Hakujua awe na nani na alipoona Hanninton na Quinn wameingia mitini na akajitokeza Moza Boy akaona ngoja atii kiu yake kwa Leo ambaye kumbe aliingia hapo kwa bahati mbaya na Leo nae alikuwa na kiu na akaamua uitii.
 
Leonel ameondoka ... kilichonisikitisha sana ni kwamba hata nchi yake haikumpa kura. Nchi pekee zilizompa kura ni pamoja na Malawi, Zimbabwe, Namibia na Uganda. Hizi nchi zimekuwa consistent katika kupiga kura kila Kelvin anapokuwa up for eviction.
 
Hivi wale wapiga debe wakubwa wa sadc (P-hole, sadc president, Lailla nk) watakuwa wanatoka nchi gani? mimi nilidhani SA au ni Namibia hawa. Kwakweli hao wanajiita sadc kampeni zao zimepata pigo kubwa sana, i hope wataachana na upuuzi wao sasa.

Sasa tusubiri kesho, nahisi Itai anaweza kumpandisha Emma kizimbani kama hatakuwa nominated. Kevin anaweza kuwa up for eviction tena. Huenda siku za Emma zikawa zinafika ukingoni mjengoni.

Hata hivyo, huenda Biggie akabadilisha wiki hii kwani umebakia mwezi mmoja tu na housemate wapo 7. Labda mwaka huu wiki ya mwisho wantabakia hm 5.
 
Hata hivyo, huenda Biggie akabadilisha wiki hii kwani umebakia mwezi mmoja tu na housemate wapo 7. Labda mwaka huu wiki ya mwisho wantabakia hm 5.

Yacob kabla hajatoka alidai kwamba aliambiwa na BB kuwa finals mwaka huu ni washiriki 5, siyo watatu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma. Lakini Yacob angeweza kusema chochote na hasa linapokuja swala la strategies, kwa hiyo tumsubiri BB atasema nini wiki hii.
 
Lolote lilotokea huko BBA, nina imani kuwa Betty alikuwa mwakilishi mzuri wa kike kutoka Tanzania. Watoto wetu wa kike wengi wamekuwa ni aibu tu, hasa wanapochanganyikana na vijana wa kiume kutokea nchi za nje; Betty was none of them.
 
Leonel ameondoka ... kilichonisikitisha sana ni kwamba hata nchi yake haikumpa kura. Nchi pekee zilizompa kura ni pamoja na Malawi, Zimbabwe, Namibia na Uganda. Hizi nchi zimekuwa consistent katika kupiga kura kila Kelvin anapokuwa up for eviction.

Hata mwenyewe hakushtuka alijua anatoka,wiki hii huenda Emma akaondoka maana kama Itai asingekuwa HOH yeye ilikuwa ndiye wa kuondoka
 
Nominations za leo:

Itai: Emma & Geraldine
Emma: Nkenna & Mzamo
Edward: Emma & Itai
Geraldine: Itai & Emma
Nkenna: Itai & Emma
Kevin: Edward & Mzamo
Mzamo: Itai & Emma

Preliminary Results

Emma - 5
Itai - 4
Mzamo - 2
Nkenna - 1
Geraldine - 1
Edward - 1

Tusubiri maamuzi ya Itai, ambaye atajiokoa mwenyewe na sijui atampandisha nani hapo juu.
 
Alliance ya Emma imesambaratika kabisa na kila mmoja anatafuta kulipa kisasi wabaya wake. Emma na Kevin wangeweza kukubaliana wawa-nominate Eddie na Mzamo tatizo Emma naye anataka kulipa kisasi kwa Nkenna. Matokeo yake hawawezi kuwapeleka kwenye eviction list.

Bila shaka Itai anajiokoa mwenyewe na kumpachika Gerra, na Africa itamuokoa Emma kwa upenzi na strategy. Nchi zinazompenda Kevin zita mpigia kura Emma (maybe isipokuwa Naigeria). Tanzania licha ya kwamba Angola hawakumpigia kura Elizabeth bado nadhani tutampa kura yetu Emma.

Wale wa kambi ya Eddie (sadc camp) watampigia kura Emma ili aingie best 5 kuzigawa kura za Kevin. Sadc wameshatambua kuwa Kevin anamashabiki wengi, hivyo kilichobaki ni kuzigawa kura zake kwa kumuacha Emma na Nkenna. Next week ataondolewa Itai. Hivyo final itakuwa ngumu sana, kutokana na ukweli kwamba Kevin/Emma/Nkenna watagawana kura upande mwingine Edward/Mzamo watagawana kura pia. Tusubiri tuone.
 
Back
Top Bottom