Mkuu Jenipher ni mtoto wa mwanasheria maarufu wa Msumbiji bwana Inácio Sebastião Mussanhane, Siku za karibuni amepewa nishani kutoka Marekani kwa kupigania haki za binadamu.
Huyu mzee Baba yake na Jeni inasemekena wakati anasoma SA aliwahi kusikia kuwa kuna jamaa anawachukua wadada wa msumbiji alafu anawaweka kwenye danguro,(anawafanyia biashra ya ukahaba, anauwauza). akaenda huko akijifanya mteja na baadaye kuwambia wale akina dada yeye sio mteja lakini angependa kuwasaidia watoke.
Akina dada hao walimshirikisha mzee issue zote na baadaye kamfuata huyo jamaa mwenye Danguro na kumtaka awaachie hao akina dada lakini huyo jamaa kataka kumuhonga kiasi kikubwa cha pesa, baba yake Jeni alikataa.
Baadaye jamaa wakamtishia kumuua, lakini akawatafuta Polisi wa SA, ubalozi wa msumbiji na wa Marekani wakasaidia kuwaokoa wanawake kadhaa.
Sasa inasemekana anaheshima kubwa sana huko kwao (Msmbiji na kimataifa) na anataka kuilinda hii heshima kwa gharama yoyote. Inaonekana wakati binti yake anaenda huko BB, mzee hakujua (au hakuwepo). Sasa mtoto anabwabwaja mno habari za familia ndani ya nyumba ya BB, na dingi ameshaona uwezekano wa binti kumegwa nao upo akiangalia heshima yake kwa jamii ameona khaaa bora lawama.
Nasikia amewataka wamtoe mtoto mara moja lasivyo atachukua hatua kali, baya zaidi ametishia kumwacha mke wake (mama yake Jen) kwa kosa la kumruhusu mtoto aende BBA.
Khaa mimi nimeishiwa maneno, lakini mtoto anatia huruma sana ukimsikiliza jinsi anavyowaaga wenzie. Anyaw wanazo tayari acha watu kama akina Elizabeth ambao hawakuweza kusoma hata Ngumbaro kwa kukosa ada wapate huto tuvijisenti tuwasaidie.