Mkuu wangu Mbogela,
Nilisema wiki hii tutaona alliances zikienda na maji na ninaona kila mtu hamwamini mwenzake. Kama Paloma na Liz wasingekuwa nominated, basi trust ingeendelea kuwepo. Tatizo vinara wa Girl Power walipokuwa nominated wakajua lazima kuna nyoka kwenye alliance yao, maana kila wakipiga hesabu za kura zinagoma.
Non-smokers alliance walikuwa wanamlaumu Itai kwamba kura yake ya nomination ilikuwa na madhara kwa Paloma na Liz na ndiyo maana wamekuwa nominated. Lakini ni nani yuko tayari kusikia kwamba alliance hii wanataka kuku-nominate na yeye akakaa kimya bila ku-retaliate? Tit for tat ndio mwendo wa game.
So far kuna Players kama 6 hivi ambao wameishasema ama hawataki tena alliance ama wako kwenye alliance lakini hawaziamini tena. Players hao ni pamoja na Kevin, Liz, Elizabeth, K1, Itai, Kristal na Hannington. Msingi wa any alliance ni trust; if there is NO TRUST then NO ALLIANCE.
Kiama kitakuwa siku ya Jumapili. Kama Paloma ataondoka, basi jumba zima na hasa kwa upande wa akina dada wataishiwa nguvu kwa kuwa wana amini kwamba Paloma is the strongest player kwa hiyo hawezi kutoka, na huo ndiyo utakuwa mwisho wa Girl Power. Nina hakika members wa Girl Power watakaobaki watajipachika ama kwa wavuta sigara ama kwa non-smokers kwa kuwa wao wenyewe kwanza hawaaminiani.
Kama Namibians wote 3 wataondoka, next victims watakuwa Yacob na Itai na baadaye watafuata Mzamo na Hannington na huo ndio utakuwa mwisho wa smokers alliance.
Kama Paloma atatoka na Ed akabaki, angalau Ed anaweza kuwaongezea nguvu smokers na hivyo wakajikongoja na kufika mbali iwapo tu Girl Power itasambaratika ama ikiendelea kukosa imani na non-smokers alliance.
Sijajua kwanini Paloma ameanza kumganda Yacob na pia Liz ameanza kumganda Hannington. Hiyo nayo ni dalili mbaya, may be kuna kitu wanakitaka kutoka kwa hao jamaa 2, ama inaweza kuwa wanataka kuwavuta ili waungane na kummaliza Kevin na K1, maana sijasikia msichana yeyote akiwasema Quinn au Jeremy kwa ubaya, wanaosemwa ni K1 na Kevin kutoka kwenye hilo kundi la non-smokers.
Inawezekana Quinn haguswi kwa anatoka nchi moja na Liz ambaye ni kinara wa Girl Power na pia Jeremy haguswi kwa kuwa bado hawana imani sana kama JEMMA imekufa kikweli ama ni usanii tu. Kama Paloma atatoka nina hakika JEMMA inaweza kuibuka upya kwa kasi ya kuua mtu, kwa sasa Emma ana negative influence ya Paloma na ndio maana ame back off.
Paloma jana alikuwa anawahoji JEMMA kuhusu future, nadhani alikuwa anataka kupata uhakika kama Emma anaweza kuwa tayari kumchinjilia mbali Jeremy. Na wao kwa ujinga wanajibu na kujieleza utadhani wako kwa Discipline Mistress. Pia alimhoji Geraldine kuhusu K1 na Lionel. Kwanini mtu atake kujua undani wa mahusiano ya watu? Bahati nzuri Paloma amekutana na watu wastaarab sana na wanamjibu sincerely utadhani ni mzazi wao.
Any player anapotoa details kama hizo ni sawa na kuji-expose na hivyo anakuwa more vulnerable. Maana tayari Paloma ana inside info ya mahusiano yao, kama alikuwa na sumu ya kumwaga kwa Jeremy ama Emma anaweza kuimwaga at any time na isiwe na madhara kwa Paloma. Kama wasingeji-expose atachukua muda mrefu kuchunguza na kupata uhakika na anaweza kufanya decision at a wrong time ana akawa na incomplete info na hivyo outcome ya decision yake ikawa na madhara kwake kama ilivyokuwa kwenye nominations za Jumatatu iliyopita.
Kilichofanya Paloma na Liz wawe nominated last time ni vitu kama hivi, walianza ku-discuss nominations tangu Jumanne na wakawa wanawa-target Mzamo na Itai, walipopata info nyingine wakabailisha mawazo na tayari majadiliano ya nominations yalishaanza ku-leak matokeo yake unajiongezea maadui wa ndani unnecessarily. Halafu anashangaa kwanini amekuwa nominated!