Mkuu Nemesis,
Yaani ulichokisema ndiyo kile nilichokuwa nacho mawazoni, na ukisoma post yangu pale juu kuna mambo mengi ambayo tumeyaongelea kila mmoja kwa wakati wake.
Hali ilivyo hakuna housemate aliyetayari kuwa karibu na Elizabeth kutokana na tabia yake ya ugomvi na chuki.
Leo asubuhi walipokuwa wanagombana Itai hakujua kinachoendelea akawa ameenda kuwa-join kwenye garden, aliposikia kinachoongelewa ni ujinga wao, aliondoka haraka sana na kwenda kuendelea na hamsini zake. Jana wakati wanagombana Eddie alikuwa around akawa anasema fight fight fight, kitu ambacho kwa Eddie ni cha kawaida sana na hata kwa mtu yeyote na ni sehemu ya jokes. Lakini dada yetu alijibu kwa ukali mpaka nikawa ninashangaa, Is it your business? Kweli mtu kama huyo hata kama una nia njema unaweza kumsogelea?
Dada yetu yuko too moody, hata marafiki zake wa karibu (JEMMA) wanaogopa kumshauri, maana unaweza kumshauri kwa nia njema akakugeuzia kibao, sasa nao wanaanza kuwateta na huku wako kwenye alliance moja. Ukifikia hiyo stage ya kukwepwa na mabest wako basi wewe ni mzigo usiobebeka.
Elizabeth ameshajenga uadui mkubwa na Mzamo, Leonel, Itai, Eddie na Nkenna.
Na hawa wote wanaisubiri Jumatatu kwa shauku kubwa ili waende kummaliza. Already wameisha wa-out number akina JEMMA + KELIZ, na wanaonekana wana common goal. Emma akienda kuwaomba kura, hawatamwelewa, lazima kwanza waondokane na kisirani ndipo wataanza kuhangaika na wa-Nigeria.
Endapo Emma na Jeremy wataondoka jpili itakuwa mbaya zaidi kwake.
Hivi anaondoka mmoja ama wanaondoka 2? Kama wanaondoka 2 hiyo itakuwa big blow maana wanaoipenda JEMMA watashindwa kujua wampe nani kura. Ndivyo ilivyokuwa kwa Namibians 3, Paloma aliwapelekesha puta sana, maana watu hawakujua wampe pacha yupi ama m-Namibia gani kati ya wale 3. Eddie alipona kwa kuwa hakuwa na nchi isiyompenda.
Binafsi nime-give up na sitampigia kura tena, msaada ninaoweza kuutoa ni kusaidia arudi nyumbani haraka.
Mkuu ni mapema sana, labda tuendelee kumpigia debe anaweza kuongeza japo wiki moja, maana ukimnyima kura ndo utakuwa umempa msaada mkubwa wa kumuwahisha kwa bf wake.
Ninahisi huyu mtoto ana matatizo ya maruhani ya hisia za mapenzi (huwa anasisimka kirahisi sana), kwanini huwa anaogopa kuguswa? Ukichunguza sehemu nyingi wanazogombana, chanzo kinaweza kuwa Kelvin kutaka kuongea na mtoto huku akiwa ana mshika mshika ama akiwa anamsogelea, kitu ambacho kwa marafiki wa opposite sex na kwenye jumba kama hilo ni cha kawaida sana, hata kama hakuna mahusiano ya kimapenzi. Kweli ukiwa kwenye hayo mazingira unaweza ku-avoid kuguswa completely na rafiki yako?
JEMMA wanasema ana "sexual tension" (whatever that phrase means), nahisi mtoto mambo yake huwa yako jirani sana na ndio maana anaogopa sana kuguswa guswa kwa kuwa anaweza kuanguka kirahisi sana.