Big Brother Africa 2009: The Revolution

Big Brother Africa 2009: The Revolution

duuu mazee mtoto ni mkali, yaani fikiria inakuwa mkeo hivi, yaani kitu kimewaka mno, Lakini wanapsycholojia wanasema watoto waliokuwa bila baba huwa wanakuwa hivi na pia huwa hawana aibu kuwaconfront wanaume sijui huyu kama anaangukia kwenye hizi stastics, ameishi na baba yake mpaka lini? Pia nahisi inawezekana huyo BF wake ni Mume wa mtu kwa hiyo hataki jina lake litajwe au kuna sababu nyingine ya kumficha asifahamike, kwani aliyevujisha hii siri ya kuwa ana BF nadhani alikuwa Emma ambaye alimwamini, na Kama mtakumbuka wakati anaingia alisema kuwa hatajiingiza kwenye mahusiano hata iweje nadhani anataka kusimamia kile alichokuwa amekisema. Mimi nililalamika kuwa ile statement sio nzuri itakuja kumhukumu, na ndiyo inayomdrive sana saa hizi. Hili la BF wake kutajwa leo mara ya Pili anagomba.
 
Yacob alishasema kwamba huyo dada anahitaji mwanaume strong, akiolewa na mwanaume legelege lazima apelekeshwe puta. Kevin na kelele zake zote, pale ni mwisho wa maneno, huwa hafurukuti.

Swala la yeye kuwa na bf pia alishalisema mwenyewe, alimwambia Kevin na akamwambia wazi kwamba ana bf mzungu, na tangu aanze kujua mambo ya wanaume, hajawahi ku-date mweusi. Ndio ile siku Kevin akasema hawawezi kufika popote kwa kuwa preference ya mtoto ni wazungu. Mtoto aliangua kilio utadhani kapigwa, sasa sijui alikuwa analia nini? Maana hiyo kauli ya Kevin ilikuwa inamtoa kwenye kitanzi kwamba kajamaa kamekata tamaa na kanajikata.

Leo Kevin kasema anashindwa kumwacha peke yake, maana hana mtu mwingine aliye-close nae zaidi ya Kevin. So Kevin akisema amtose, Eliza atabaki mwenyewe of which maisha yanaweza kuwa magumu. But again, Kevin nae ni mjinga ama ni mtoto, kwa mazingira ya humo ndani nina hakika Kevin akikaa mbali na Eliza, Eliza atamfuata after few days na hawezi kuwa na huo ujinga anaomfanyia.

Ninahisi kilichomfanya Eliza awake sana leo, ni pale Itai aliposema kwamba Kevin huwa anapata "some extra" kutoka kwa Eliza. Eliza inawezekana ali-interpret vibaya hiyo kauli, akahisi labda watazamaji wanaweza kuhisi kwamba Kevin alishafika mbali. Jamani BB huwezi kujificha, kila kitu kiko hewani, wakiamua kula denda tutaona, wakijifunika kwenye covers tutaona kila kitu.

Itai anaweza kuwa na makosa ama alikuwa right, "getting some extra" can mean several things from conversation, kissing, cuddling, making love, etc. Yote hayo yanaangukia hapo. Wakati mwingine hata kuongea na mtu wa opposite sex kwenye mazingira kama yale means a lot, achana na mambo ya kuvuana chvpi.

Kama Itai alifanya makosa, Eliza alitakiwa kwenda kumwambia/kuongea nae kwa upole. Kwamba Itai ninakuheshimu, nimesikia hiki na kile mkiongea na Kevin, naomba swala la mimi na Kevin usijiweke kati yetu. Tutali-handle sisi wenyewe na hakuna haja ya kulisema mbele ya kadamnasi. Kama Itai angerudia hapo angekuwa na haki ya kumuwakia, ila leo kwa kifupi aliwaka sana (over reaction). Kitu ambacho kinaweza kutafsiriwa vibaya kwamba dada yetu ana mawazo mabaya.
 
lakini tukiyangalia maisha yake binafsi familia anayotokea na huyo Boy friend wake na hao wengine aliowahi kudate nao ili tuweze kuona kama hakuna tatizo la kisaikolojia pale, tutakuwa tunaenda mbali mno? au mnadhani ni maisha yake binafsi? actually nitaendelea kumsuport sana ameonyesha msimamo, LAKINI ningekuwa mwajiri anakuja kuomba kazi baada ya BBA, kwa kweli siwezi kumpa, huyo kazini itakuwa balaa, imagine yupo kwenye open office alafu mfanyakazi mwezie mmoja anamboa kidogo tu, duu moto utakao waka hapo usiombe
 
Ili kumsaidia Elizabeth na kutufanya tuendelee kumjua zaidi basi ni kumwondoa Mzamo this week. Haters wakubwa wa Elizabeth mle ndani ni Mzamo (Malawi) na Leonel (Mozambique). Kwasasa nadhami atakuwa ameongezeka Itai japo hata huko nyuma Itai hakuwa upande wa Elizabeth na kura ya Zimbabwe tulishaikosa siku nyingi.

Kibaya zaidi mmoja kati ya rafiki zake (Jeremy au Emma) anaondoka jpili hii. Itakuwa vibaya sana kama Mzamo atabaki Jemma wakaondoka. Rafiki wa Elizabeth atakuwa Kevin tu, labda amsogelee Geraldine. Hali ilivyo hawezi kufanya urafiki na Eddie wala Itai, wakati huo huo Nkenna na Leonel ndo wabaya wake. Akipata akili amwombe radhi Itai.
 
Mkuu Nemesis.

Siyo kwamba ninakukatisha tamaa, lakini ukweli unabaki pale pale, kumtoa Mzamo ni kazi ngumu sana, ana fans wengi kuliko hata Emma. Maadui wa nje (nchi) wa Mzamo ni wachache ukilinganisha na nchi ambazo representatives wao wametendwa na JEMMA.

JEMMA ina disadvantage, nchi ambazo zinaunga mkono JEMMA lazima wata-split kura zao. Waki-split kura wanampa advantage Mzamo. Nkenna amecheza kete yake kwa ufundi wa kutosha, maana angemwacha Itai, JEMMA ingepona.

Pattern ya Kura inaweza kuwa hivi:
Uganda hawawezi kuwapa kura JEMMA, kwa sababu alliance yao ndio aliyowatosa Phil na Hannington. Nigeria wamegawanyika baada ya kusikia Emma, Eliza na Jeremy wakipanga mkakati wa kuwa-nominate Nkenna na Geraldine wiki ijayo. Kwa hiyo ili kupunguza madhara kwa Nigerian housemates, majority of Nigerians wame-settle for Mzamo, japo kuna wengine wanaitaka JEMMA ila hawajui wampe nani kura.

Namibia hawajasahau mkakati wa Emma kuhakikisha mapacha wanapandishwa wote kwa kum-nominate mmoja na then wa pili anachomekwa na HoH. South Africa bado wanauguza jeraha la Quinn kuondoka, na aliyesababisha akawa nominated ni Emma alipokuwa analipa kisasi.

Zimbabwe bado wanaona JEMMA ni threat kwa Itai na walikuwa na mkono kwenye eviction ya Kristal/Quinn. Issue ya jana Eliza kumjia juu Itai nayo imeongeza mafuta kwenye moto kwa kuwa Eliza na JEMMA lao ni moja. Mozambique they will be behind Mzamo kwa sababu ya Leo. Nchi zilizobakia with exception of Angola na Kenya, kura zake zinaweza kwenda either way. Chances za JEMMA kupona ni ndogo mno, Jeremy lazima ataondoka Jumapili.

Kwa hesabu za haraka haraka Mzamo anaweza kupata kura za Uganda, Malawi, Zimbabwe, Namibia, Mozambique na South Africa. Akishapata kura za nchi 5, basi anapeta, unaless wawe wanatoka housemates 2.

As you said we need to support our representative kwa kuwapa kura JEMMA, ninaungana na wewe japo vita ni ngumu. Sample ya polls za BB kule kwenye site yao zinaonyesha mchuano mkali kati ya Mzamo na Emma, Jeremy kaachwa mbali.
 
Nadhani anayasikia mnayosema

ELIZABETH APOLOGISES TO ITAI
They had a talk in the garden so Itai could understand where all the anger was coming from and etc etc etc. It was cool in the end and they started talking about the task. So, all is well that ends well. These HMs are human. Well done Elizabeth and Itai
 
Today's Nominations

Jana nilisema kwamba kwa jinsi mambo yalivyo, uwezekano wa kuwa-nominate Nigerians ni mdogo sana. Nominations za leo Nigerians wamepona na sasa kama Nkenna ni smart, it is time to do her thing strategically kwa kumuweka Emma up for eviction, move hiyo itaisambaratisha alliance ya akina Emma.

Summary ya nominations:

Nkenna - Jeremy + Emma
Mzamo - Jeremy + Elizabeth
Eddie - Itai + Jeremy
Itai - Jeremy + Mzamo
Elizabeth - Itai + Mzamo
Kevin - Leonel + Mzamo
Emma - Itai + Mzamo
Leonel - Jeremy + Elizabeth
Geraldine - Nkenna + Mzamo
Jeremy - Itai + Mzamo

Waliopata kura nyingi ni:
Mzamo = 6
Jeremy = 5
Itai = 4

Iwapo Big Brother atachukua wawili wa juu, basi ni Mzamo na Jeremy. Iwapo itakuwa hivyo na kama Nkenna ni strategist mzuri atamuokoa Mzamo na kumuweka Emma ili mmoja kati yao aondoke. Iwapo BB ataamua watatu wawe nominated basi Nkenna, for obvious reasons, atamuokoa Itai na kumuweka Emma. Bado Jeremy anaweza kuwa na kibarua kigumu mbele ya Emma na Mzamo, in the end alliance ya akina Emma itasambaratishwa. Ngoja tusubiri baadaye tuone maamuzi ya Nkenna yakoje.

Wiki hii itakuwa ni mbaya sana kwa JEMMA na pia hata Elizabeth, kwa kuwa lazima Emma na Elizabeth watakuwa hawana imani kama wamepona au la.

NOTE: Hakuna housemate aliyem-nominate m-Nigeria yeyote, zaidi ya Geraldine ambaye kasema ndivyo walivyokubaliana na Nkenna. Jana nilisema watabaki untouched.

The whole thing is fvcked up kwa sababu ya alliance ya kijinga ya akina Emma ambayo automatically inawagusa other two Nigerians, kwa hiyo akina Emma hawawezi ku-introduce subject ya wingi wa Nigerians mbele ya Kevin unless wamtumie Eliza. Eliza angekuwa na "mahusiano" na Kevin ya JEMMA style, angweza kuifanya hiyo kazi kwa urahisi na mafanikio ili amshawishi Kevin awatose ma-'wifi' zake. Sasa dada yetu haeleweki, kwanini Kevin a-take risk ya kuwatosa dada zake na ilhali hana attachment yoyote na Eliza.

Sasa wasubiri non-Nigerian ashinde HoH labda akiwa-swap ndipo wanaweza kuwa up for eviction. Lakini kwa mwendo huu wa nominations ni ngumu sana na leakage ya strategies ni kubwa, Kevin hawezi kukaa kimya akisikia Emma na wenzake wanataka kuwa-nominate dada zake, lazima ataenda kuwaambia na hivyo hao akina dada watatafuta numbers ili ku-counter hiyo strategy.

kwa kweli keil wewe ni analyst mzuri sana, nimekua nikukufatilia toka hii revolution ilivyoanza, kikubwa zaidi una predict vitu vingi ambavyo huja kutokea kweli.....naona mwakani uwepo kwenye jopo la wanaochagua watu wakutuwakilisha uko...wakupe tu ilo dili na hakika tutafika mbali sana...Hongera ndugu.
 
Mkuu Nemesis.

Siyo kwamba ninakukatisha tamaa, lakini ukweli unabaki pale pale, kumtoa Mzamo ni kazi ngumu sana, ana fans wengi kuliko hata Emma. Maadui wa nje (nchi) wa Mzamo ni wachache ukilinganisha na nchi ambazo representatives wao wametendwa na JEMMA.

JEMMA ina disadvantage, nchi ambazo zinaunga mkono JEMMA lazima wata-split kura zao. Waki-split kura wanampa advantage Mzamo. Nkenna amecheza kete yake kwa ufundi wa kutosha, maana angemwacha Itai, JEMMA ingepona.

Pattern ya Kura inaweza kuwa hivi:
Uganda hawawezi kuwapa kura JEMMA, kwa sababu alliance yao ndio aliyowatosa Phil na Hannington. Nigeria wamegawanyika baada ya kusikia Emma, Eliza na Jeremy wakipanga mkakati wa kuwa-nominate Nkenna na Geraldine wiki ijayo. Kwa hiyo ili kupunguza madhara kwa Nigerian housemates, majority of Nigerians wame-settle for Mzamo, japo kuna wengine wanaitaka JEMMA ila hawajui wampe nani kura.

Namibia hawajasahau mkakati wa Emma kuhakikisha mapacha wanapandishwa wote kwa kum-nominate mmoja na then wa pili anachomekwa na HoH. South Africa bado wanauguza jeraha la Quinn kuondoka, na aliyesababisha akawa nominated ni Emma alipokuwa analipa kisasi.

Zimbabwe bado wanaona JEMMA ni threat kwa Itai na walikuwa na mkono kwenye eviction ya Kristal/Quinn. Issue ya jana Eliza kumjia juu Itai nayo imeongeza mafuta kwenye moto kwa kuwa Eliza na JEMMA lao ni moja. Mozambique they will be behind Mzamo kwa sababu ya Leo. Nchi zilizobakia with exception of Angola na Kenya, kura zake zinaweza kwenda either way. Chances za JEMMA kupona ni ndogo mno, Jeremy lazima ataondoka Jumapili.

Kwa hesabu za haraka haraka Mzamo anaweza kupata kura za Uganda, Malawi, Zimbabwe, Namibia, Mozambique na South Africa. Akishapata kura za nchi 5, basi anapeta, unaless wawe wanatoka housemates 2.

As you said we need to support our representative kwa kuwapa kura JEMMA, ninaungana na wewe japo vita ni ngumu. Sample ya polls za BB kule kwenye site yao zinaonyesha mchuano mkali kati ya Mzamo na Emma, Jeremy kaachwa mbali.

Mkuu Keil, ninakubaliana na wewe, wish zangu ni ngumu kutimia. Bila shaka mshiriki wetu atakuwa ktk wakati mgumu sana wiki ijayo. Amekuwa akipoteza marafiki kadri siku zinavyokwenda. Tatizo yupo serious mno. Elizabeth amefanya vizuri kuomba msamaha kwa Itai.
 
http://beta.mnet.co.za/mnetvideo/browseVideo.aspx?vid=20420
News: Keliz Get Physical

icon_date.gif
28/10/2009
icon_comm.gif
94 comments

It all starts off with Kevin teasing Elizabeth with some strokes and pokes while she lies on the couch. When Elizabeth tells him to stop, Kevin takes it up a notch!

A tipsy Kevin tells Elizabeth that his being there for her is like her winning the lottery. Kevin persists to touch and poke Elizabeth who clearly does not like it. Elizabeth hits back hard with a pillow but Kevin keeps at it. Elizabeth cries but Kevin does not seem to take the tears seriously.

Eventually Elizabeth starts slapping him but Kevin keeps laughing and asks why Elizabeth is getting violent. Elizabeth tells Kevin: "You should be lucky that you don't hit women otherwise I would have hit you hard!"

Kevin tells Elizabeth that when she fights with other Housemates, like Itai, he defends her so she should calm down. After a lot of struggling between the two, Elizabeth leaves the couch and storms off.

Kevin and Elizabeth, former Comrades in Arms, have fought a couple of times. Kevin has repeatedly confessed his love to Elizabeth who has rejected him.
 
Kwa hali anayoenda nayo "psycobeth" she will be out sooner than we anticipated.....alionekana kufanya vizuri mwanzoni lakini nadhani ni kwa vile she was keeping a low profile...sasa what we are seeing now is the real Elizabeth and i must say iam very very dissapointed!!!! Watanzania tunajulikana sana kwa ukarimu wetu na how charmingly we interact with people lakini huyu mdada has a major problem!!!i pity the guy she is dating!!!!kwanza she is a control freak yaani hii huhitaji kuanalyze sana, secondly ana lugha kali, she is rude, worse is that she has a violent behaviour im sure kusingekuwa na policy ya not fighting in the house siku nyingi angekuwa ameshapigana. Simlaumu coz i don't know her..and how she became who she is...yawezekana upbringing yake ndo sasa inajireflect kwenye tabia anayodisplay. Naangalia sana BB lakini i think i have had enough...nothing and no one can save this woman from being evicted next week and she only has herself to blame....My advice to fellow Tanzanians...lets put country loyalty aside and vote for the best person....which sadly in my opinion is not Elizabeth.
 
Lakini mkuu si unaona kuwa hivyo vituko ndio entertainment yenyewe, watu tuna kitu cha kuangalia na kujadili
 
Lakini mkuu si unaona kuwa hivyo vituko ndio entertainment yenyewe, watu tuna kitu cha kuangalia na kujadili

Sina hakika kama ni entertainment, ingekuwa ni entertainment iwapo wangekuwa wanatubadilishia, mara ugomvi, arguments, vicheko, maongezi mazuri na mengine, lakini ni ugomvi non-stop. Richard na Tatiana walikuwa wanagombana sana, lakini baada ya dakika chache utawakuta wamepatana na wako kwenye kiota chao cha maraha.

Hakuna kitu kibaya kama mtu kuonekana na mahasira all the time ama hawawezi kukaa waongee mpaka mwisho bila Eliza kukasirika. Watu wanasema Eliza is irritating, na siku zote yeye ndo mwenye kukasirika.

Siwezi kumlaumu Eliza kwa kitu hicho, Kelvin anachangia kwa kiasi kikubwa sana na huyo ndio adui wake mkubwa kwa kuwa ndio anamfanya Eliza aonekane mbaya. Asingekuwa Kelvin watu wasingejua Eliza ni nani na ana tabia gani. Alishasema kwamba siku akiwa hajisikii kuongea huwa anaweza kushinda kutwa nzima yuko alone na hasemi. Kelvin hawezi kumpa nafasi hiyo na ndio maana huwa wanaishia kugombana kila mara, maana Kelvin hajui amvae saa ngapi na wakati gani amwache kama alivyo.

Watu wa jamii ya Eliza unatakiwa kuwa-avoid unapoona wako kimya, subiri mpaka yeye mwenyewe akiwa anajisikia kuongea na wewe ndipo atakufuata lakini siyo umfuate. Sasa kijana hajui hilo ama utoto unamsumbua.

Tunachohitaji ni yeye kutokuonyesha upande mmoja tu wa shilingi,ajitahidi kutuonyesha pia mazuri yake. Task za kucheza hapo utampenda lakini social interaction (which is very important ndani ya jumba) ni ZERO.
 
Is Elizabeth in Danger?

Sure! She is in danger of being nominated next week and may be being up for eviction. If she will be up for eviction, her survival will depend on who she will be against on a chopping board. She stands a 50 - 50 chances if she will be up against Moza boy (Leonel) or Itai. She may have advantage if she will be against one of the Nigerian Gals (iff viewers will decide vote out one Nigerian regardless of whether she is better than Eliza or otherwise). The rest of housemates are too tough for her, and if she will be up against any of the rest of housemates, chances of being evicted is 75%.

Kitakachomuokoa ni kama ata-win HoH. Lakini akikosa HoH ajue kwamba anaondoka kwa kuwa kama Emma atashinda basi unorganized alliance (Itai, Eddie, Mzamo, Leonel, Geraldine, na Nkenna) wanaweza kumuweka Emma na Eliza ili Emma ajiokoe mwenyewe. Ikitokea Kelvin aka-win HoH, chances za Eliza kuokolewa ni 50-50 na esp iwapo the unorganized alliance wataamua kum-nominate Eliza na one of Nigerian gals, hoping that Kelvin will save a Nigerian gal.

Mpaka sasa Eliza ndio anaonekana kuwa common target ya unorganized alliance, ana beef na Itai, ana kisasi cha kimya kimya na Eddie, haivi na Nkenna, haivi na Leonel na impliedly Mzamo nae anaingia ndani. Hao wote wakim-nominate tayari atakuwa na kura nyingi kuliko wengine.

End of the Road for JEMMA + KELIZ?
JEMMA + KELIZ wako kwenye edge ya kupotea ndani ya Jumba, the only person ambaye bado ana advantage ni Kelvin kwa kuwa bado ana number za dada zake na pia bado he can count on Eliza and Emma for Monday's nominations. The future of the group will be clear tomorrow baada ya task ya HoH, kama mmoja wao atashinda basi wanaweza ku-survive. Lakini unorganized alliance inaweza kuwaweka Emma na Eliza kwenye nominations ili atakayekuwa kashinda ajiokoe mwenyewe na kumwacha mwenzake, na itategemeana ni nani atakuwa up against who. So the whole picture will be clear on Monday.

Jeremy akiondoka, Emma will be frustrated na atawachukia housemates wote na esp Nkenna, na hapo ndipo visasi vitakapoanza. Nkenna anafahamu na alikuwa anaombea sana Jeremy atoke ili am-destabilize Emma apoteze focus kwenye game na hivyo ku-pave way. Kwa hiyo umaarufu wa Emma unaweza kupotea ghafla baada ya Jeremy kuondoka. Kama nominations zilimtoa machozi, Jeremy akiondoka msichana anaweza kuchanganyikiwa sana na itategemeana na jinsi atakavyo-handle hiyo situation na pia atakavyoweza ku-cope na the rest of housemates.

Kuna mambo mengi tutayaona wiki ijayo. The game has just started, na hautasikia tena Emma akisema kwamba, "It is just a game". Ni rahisi kusema hivyo ukiona hauko kwenye target na alliance yako haishambuliwi, lakini ukishakuwa kwenye target ndipo utagundua kwamba sasa ni vita.
 
Nimekupata vizuri sana mkuu Keil, kwa kusema ukweli Elizabeth si entertainer kabisa. Housemates wote wameshamchoka vibaya. Jana akina Leonel, Itai, Nkenna na Geraldine walikuwa wanajadili kwamba Elizabeth ame-survive nominations zilizopita kwasababu ya Kevin. Sababu yao ni kwamba Eliza si intertainer hivyo wapiga kura wasingempa kura. Baada ya kuendelea kugombana na Kevin, Jeremy na Emma pia wakawa wanajadiliana juu yake na wakasema anachukizwa na Kevin. Elizabeth mwenyewe akamwambia Kevin kwamba watu wanamuona psycho.

Hali ilivyo hakuna housemate aliyetayari kuwa karibu na Elizabeth kutokana na tabia yake ya ugomvi na chuki. Kevin akiamua kumtosa basi atabaki hana mtu wa karibu. Kwa hali ilivyo ni dhahiri gemu limemshinda na limekuwa mzigo kwake na wiki ijayo anarudi Dar.

Elizabeth ameshajanga uadui mkubwa na Mzamo, Leonel, Itai, Eddie na Nkenna. Endapo Emma na Jeremy wataondoka jpili itakuwa mbaya zaidi kwake. Binafsi nime-give up na sitampigia kura tena, msaada ninaoweza kuutoa ni kusaidia arudi nyumbani haraka.
 
Mkuu Nemesis,

Yaani ulichokisema ndiyo kile nilichokuwa nacho mawazoni, na ukisoma post yangu pale juu kuna mambo mengi ambayo tumeyaongelea kila mmoja kwa wakati wake.

Hali ilivyo hakuna housemate aliyetayari kuwa karibu na Elizabeth kutokana na tabia yake ya ugomvi na chuki.

Leo asubuhi walipokuwa wanagombana Itai hakujua kinachoendelea akawa ameenda kuwa-join kwenye garden, aliposikia kinachoongelewa ni ujinga wao, aliondoka haraka sana na kwenda kuendelea na hamsini zake. Jana wakati wanagombana Eddie alikuwa around akawa anasema fight fight fight, kitu ambacho kwa Eddie ni cha kawaida sana na hata kwa mtu yeyote na ni sehemu ya jokes. Lakini dada yetu alijibu kwa ukali mpaka nikawa ninashangaa, Is it your business? Kweli mtu kama huyo hata kama una nia njema unaweza kumsogelea?

Dada yetu yuko too moody, hata marafiki zake wa karibu (JEMMA) wanaogopa kumshauri, maana unaweza kumshauri kwa nia njema akakugeuzia kibao, sasa nao wanaanza kuwateta na huku wako kwenye alliance moja. Ukifikia hiyo stage ya kukwepwa na mabest wako basi wewe ni mzigo usiobebeka.

Elizabeth ameshajenga uadui mkubwa na Mzamo, Leonel, Itai, Eddie na Nkenna.

Na hawa wote wanaisubiri Jumatatu kwa shauku kubwa ili waende kummaliza. Already wameisha wa-out number akina JEMMA + KELIZ, na wanaonekana wana common goal. Emma akienda kuwaomba kura, hawatamwelewa, lazima kwanza waondokane na kisirani ndipo wataanza kuhangaika na wa-Nigeria.

Endapo Emma na Jeremy wataondoka jpili itakuwa mbaya zaidi kwake.

Hivi anaondoka mmoja ama wanaondoka 2? Kama wanaondoka 2 hiyo itakuwa big blow maana wanaoipenda JEMMA watashindwa kujua wampe nani kura. Ndivyo ilivyokuwa kwa Namibians 3, Paloma aliwapelekesha puta sana, maana watu hawakujua wampe pacha yupi ama m-Namibia gani kati ya wale 3. Eddie alipona kwa kuwa hakuwa na nchi isiyompenda.

Binafsi nime-give up na sitampigia kura tena, msaada ninaoweza kuutoa ni kusaidia arudi nyumbani haraka.

Mkuu ni mapema sana, labda tuendelee kumpigia debe anaweza kuongeza japo wiki moja, maana ukimnyima kura ndo utakuwa umempa msaada mkubwa wa kumuwahisha kwa bf wake.

Ninahisi huyu mtoto ana matatizo ya maruhani ya hisia za mapenzi (huwa anasisimka kirahisi sana), kwanini huwa anaogopa kuguswa? Ukichunguza sehemu nyingi wanazogombana, chanzo kinaweza kuwa Kelvin kutaka kuongea na mtoto huku akiwa ana mshika mshika ama akiwa anamsogelea, kitu ambacho kwa marafiki wa opposite sex na kwenye jumba kama hilo ni cha kawaida sana, hata kama hakuna mahusiano ya kimapenzi. Kweli ukiwa kwenye hayo mazingira unaweza ku-avoid kuguswa completely na rafiki yako?

JEMMA wanasema ana "sexual tension" (whatever that phrase means), nahisi mtoto mambo yake huwa yako jirani sana na ndio maana anaogopa sana kuguswa guswa kwa kuwa anaweza kuanguka kirahisi sana.
 
Keil nimekubaliana na wewe mkuu wangu. Nadhani niendelee kutoa support.

Kinachoshangaza zaidi, yeye anapoongea na mtu kirafiki (mfano Kevin) anapenda kumshika shika na kumpiga piga, akigeuziwa kibao unakuwa ugomvi mmh!.

Jioni hii mida ya saa moja hivi, ameongea kwa hisia na kulia sana. Anadai anayosiri kubwa. Kuna kitu kimemtokea siku chache kabla hajaingia big brother. Anadai kitu hicho anajua kilivyofanyika (how) na muda (when) lakini hajui ni nani waliofanya (who), wapi (where) na kwa nini hajui.

Nimeanza kuhisi huenda alitekwa na kubakwa siku chache kabla ya kuiingia big brother. Ndiyo maana siku za mwanzoni Biggie alimpatia daktari. Hivyo, ameathirika kisaikolojia, plan zake na strategy za game zimevurugika na ndo maana anahasira siku zote.

Amemwambia Kevin kwamba akimwambia hiyo siri, Kevin atashindwa hata kumwangalia usoni. Kuna kubwa hapa, pole sana Elizabeth.
 
Back
Top Bottom