JENERALI kinachomkera ni namna watu walivyomiminika kumlilia JPM, alitegemea watu wasimzike vizuri shujaa wao.
Eti JPM alijiona IMMORTAL yaani mwenye kuweza kuishi milele, matusi mabaya hayo JENERALI. Ungemtendea haki JPM ungetafuta hata hotuba zake uka'quote' kama kweli alijimwamba kiasi hicho. JPM kwa taarifa yako alitamka mara nyingi mno kwamba maisha ni 'temporal' yanapita na ndo maana alijitahidi kutumia kila dakika ya maisha yake kuleta mabadiliko.
Hata hivyo kiuhalisia JPM wa macho ya rohoni ni 'IMMORTAL'. Mawazo yake bado yanaishi, kazi zake nzuri bado zinatunufaisha na misimamo yake bado inalitegemeza taifa hili.
JPM hajaishi kizembe na wala hajafa kizembe. Amekufa akiwa kazini, wewe ndugu yangu JENERALI ni LOOSER ndo maana G55 iliishia hivyo hivyo, huna legacy. Hata kumwandika JPM ili usomwe ni kwasababu ana jambo bado, he is BIG MAN. Kumbe hata akilini mwako hajafa na huenda unaogopa what if he comes back.
Tahadhari, unapoandika baya juu ya JPM kuwa na ubinadamu maana unawatia huzuni mke n.k.