Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

 
Kwa hiyo swali la kujiuliza kwanini amebadilisha jina mara baada ya kuteuliwa kuwa mgombea wa CCM? Ana umri wa miaka 39 sasa, kwanini hakubadilisha alipokuwa O-Level, A-Level ama Mlimani au wakati akifanya graduate program?
Mkuu, imeshasemwa kuwa hajabadili jina, isipokuwa ameongeza la katikati ambalo alokuwa halitumii. Mchezo umekwisha, tusubiri kampeni na ushindi wa kishindo
 

- Mkuu kama nimekupata vizuri ni kwamba ni haki ya kila mwananchi kuhoji ni sawa kabisa, lakini nimesikitishwa sana kwamba katika habari nzima umeshindwa hata mara moja ku-mention haki za Oscar kisheria pia kujitetea na attacts zisizokuwa na legal facts at hand,

- Sheria ni kweli inatakiwa kuwa kipofu, lakini only inapokuwa imeshiba yaani all legal facts at hand ambazo kwenye hi ishu ya Oscar, so far either hazipo au zipo ila hatujawekewa, sasa kwa mantiki ya kutokuwa na all the facts mezani bado sheria ianatakiwa kuwa kipofu na kusema otherwise ni kumhukumu Oscar kwamba tayari ana utata na sheria that is unfair kwa civil society kama tuliyonayo hapa JF.

Otherwise, baada ya kuisoma sana na betweeen the lines hii article yako, sasa I am convinced than ever before kwamba ushahidi wa ishu bado uko mbali sana na tuendelee kuusubiri.

Respect.

FMEs!
 


Haki za Oscar hazitegemei mimi kuzitaja. Yeye kama msomi anajua haki zake na anajua ni wapi anatakiwa aziite kumtetea. Lakini zaidi ni kuwa Oscar hajanyang'wanya haki hizo.


Ili kuweza kushiba facts zote sheria inahitaji kuhoji maswali. Kinachofanyika hapa na kwa muda tangu ianze post hii ni maswali ambayo yanalengo la kuchochea kutafuta facts. Mahali pa uhakika pa kupata facts siyo JF bali mahakamani au kwenye chombo ambacho kinasimamia. Sisi tunachofanya hapa ni kudodosa tu na kuchokoza lakini tusijifikirie kwa namna yoyote sisi ni sehemu ya utafutwaji haki au utoaji haki au hukumu.

Hili ni baraza la mijadala, maswali yanaulizwa, hoja zinatolewa na hupanguliwa, na mitazamo huundwa na fikra hubadilishwa au kudumishwa. So, tuendelee kutafuta facts ndio maana hadi hivi sasa sijasema lolote kwa upande wangu kuhusu kama Oscar ni raia au si raia. Niko katika kuuliza maswali.


Otherwise, baada ya kuisoma sana na betweeen the lines hii article yako, sasa I am convinced than ever before kwamba ushahidi wa ishu bado uko mbali sana na tuendelee kuusubiri.

Haitoshi kusubiri tu bali pia kuchokonoa na kuuliza maswali, kuchokoza na kuibua hoja, ni katika kufanya hivyo ndivyo ambavyo tunaupekua ukweli na hatimaye kufikia mahali kusema kuwa "tunajua". Tuendelee kuuliza maswali na kutafuta majibu.
 
Lakini Oscar si alikuwa Chameda? Iweje hawakuweka pingamizi kabla wanaweka sasa when they are expecting to run against him? Basi na Chadema ina makosa kama likuwa inajua mtu si raia na waka nyamamza. Kama iki gundulika Oscar siyo raia na Chadema walikuwa wanajua na wakati alikua mwanachama wao basi they have to be held responsible to a certain degree. If this is all true basi Chadema napo kuna unafiki.
 

- Sawa sawa, hapa tupo pamoja sana.

Respect.

FMEs!
 
Pingamizi la chadema lilikuwa na sehemu mbili. Kwanza, Oscar sio raia wa Tanzania na pili hana sifa za kugombea kwasababu hakuchaza fomu sawasawa. Kwenye fomu yake kipengele cha tatu kinauliza ulizaliwa wapi yeye akajibu "Bukoba". Kipengele cha nne kinauliza ni halmashauri/wilaya/mji/manispaa gani na yeye hakujaza kitu. Chadema wanadai "Bukoba" haitoshi kumtambulisha mtu amezaliwa wapi na vilevile unaporudisha fomu kila kipengele kinatakiwa kiwe kimejazwa tena kwa Herufi kubwa.

Oscar katika utetezi wake amewasilisha copy ya passport yake, copy ya birth certificate (ambayo tarakimu ya kwanza kwenye serial number haisomeki) pamoja barua ya mafao ya kustaafu kazi ya baba yake Biharamulo. Aidha, kwenye barua yake ya utetezi amesema bado anafuatilia vielelezo viwili, barua kutoka uhamiaji (hakusema itakuwa na nini) pamoja na cheti cha ndoa cha wazazi wake.

Mkurugenzi amesema vielelezo vilivyo kwisha wasilishwa vinatosha kuthibitisha kwamba Oscar ni raia wa Tanzania. Na kuhusu kujaza fomu sawasawa, Mkurugenzi pamoja na Oscar wamekiri kwamba fomu iliyobandikwa nje ya ofisi ilikuwa na makosa lakini fomu mbili ambazo mkurugenzi anazo zilikuwa zimejazwa kwamba anatoka mji wa bukoba. Hivyo kujazwa fomu moja kimakosa hakuwezi kumtengua Oscar kwenye kinyang'anyiro (ingawa hiyo fomu yenye makosa ndiyo ilikuwa available to the public for scrutiny).

Chadema wamekata rufaa leo mchana. Jaji makame na wenzake wanaingia Biharamulo kesho kuijadili rufaa ya chadema. Wana masaa 48 kuja na jibu.
 

Sasa hiyo kopi ya passport ni Mukasa ama Rwegasira?
 

Naam!


Kwanini kuna suala la Uhamiaji wakati yeye ni Mtanzania?



Naam
Chadema wamekata rufaa leo mchana. Jaji makame na wenzake wanaingia Biharamulo kesho kuijadili rufaa ya chadema. Wana masaa 48 kuja na jibu.

naam!
 
Naam!



Kwanini kuna suala la Uhamiaji wakati yeye ni Mtanzania?






naam!

Harafu kingine nachotaka kufahamu kuna mdau hapo juu amesema Oscar ana PHD.Ni kweli??

Jamani kama anayo na pamoja mambo yote yanawezekana lakini kwa umri huo naanza kupatwa nawasisi wasiwasi hata kwa umri wake. Jamani miaka 29 una PHD bongo aahhh teh teh teh teh.
 
....... Jamani miaka 29 una PHD bongo aahhh teh teh teh teh.


Umefulia kweli huko ughaibuni, kwa taarifa yako wenye PhD kuanzia miaka 25 hadi 33 ni wa kumwaga siku hizi. Kuwa na PhD sio kitu cha ajabu bongo, kama huna bachelor or master degree usirudi bongo mwanawane...
 
Last edited by a moderator:
Sasa hiyo kopi ya passport ni Mukasa ama Rwegasira?

MkamaP,

Hilo la jina huenda lisiwe issue sana maana kule kwetu hatujali sana majina.

Kikawaida majina ya Watanzania yanakuwa matatu, jina lako, la baba na jina la ukoo. Kuna watu wengi sana wanapoandishwa shule wazazi walikuwa wanatumia majina mawili tu yaani jina la kijana na jina la baba.

Lakini kwenye siasa za Tanzania ni muhimu sana kuweka jina ukoo ili wananchi wajue wewe ni mmoja wao. Huenda hiki ndicho kinatokea sasa kwa kijana Oscar.

Pia sehemu yoyote kubadili jina kunakubalika. Kijana Oscar anaweza tu kusema ameamua kutumia jina la ukoo badala ya jina la babake.

Of course pia kunaweza kuwa na sababu nyingine ambayo ni tofauti kabisa na hii. Pia kunaweza kuwa na udanganyifu, nafikiri CHADEMA wamepitia taarifa zake zote.
 
Umefulia kwenye huko ughaibuni, kwa taarifa yako wenye PhD kuanzia miaka 25 hadi 33 ni wa kumwaga siku hizi. Kuwa na PhD sio kitu cha ajabu bongo, kama huna master degree usirudi bongo mwanawane...

Teh teh teh
Maprof wa udsm wanavyokamata kweli wanaweza kukuruhusu kijana miaka 25 utoke na na phd.? wale jamaa soo walimkamata jamaa yangu kasoma miaka 8 PHD pale udsm,kwa kweli duuuu.

Bag'heshi Narudi huku niliko kila mtu ana phd hata mfagizi nikimuuliza anasema ana phd ,bora home wenye nazo wachache.
 
MkamaP,

Oscar ana miaka 39 na wala sio 29 kama ulivyoandika hapo juu. Taarifa zake zinasema alizaliwa 1970.

Kwa miaka ya nyuma ilikuwa ngumu sana kwa Mtanzania wa miaka 29 kuwa na Ph.D. Kwa siku hizi inawezekana. Kwa wale ambao hawajaenda JKT na pia hawakuhitaji kusubiri mwaka baada ya kumaliza A-level kwenda university inawezekana kabisa.
 

Mtanzania
Asante unajuwa kwa kweli nilichanganya mambo.
Sasa jamaa hata kama kahamia miaka 38 kaishi nchini ,mimi nafikiri hakuna haja ya kuhoji uraia wake tena.Labda wamkabe huko kwenye kujaza fomu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…