Kwa upande wangu sijui lolote kuhusu Oscar zaidi ya kinachosemwa. Kabla ya kusikia juu ya pingamizi la Chadema jina la Mukasa tu lilinidokeza kwa namna fulani kuwa huyo ndugu ana uhusiano na Uganda. Siikuwa na matatizo ya uraia wake kwani Mtu wa Uganda anaweza kuhamia Tanzania na akawa raia wa Tanzania.
Kama vile watu waliotoka Nyasa na wako Tanzania na ambao majina yao tunayajua ni ya Kichewa kina (Banda, n.k) na wapo ambao wametoka Uarabuni au asili yao ni uarabuni na ukakuta majina yao mengi tu Zenji, Dar, Tanga n.k So, kuwa na jina la "Mukasa" siyo sababu ya kusema si raia wala sababu ya kushuku kuwa si raia.
Tatizo:
a. Kwamba kulikuwa na mjadala wa jina la "Mukasa" kunamfanya mtu aulize "kwanini" ukizingatia hayo niliyoyasema hapo juu. CCM au Oscar mwenyewe hakuwa na sababu yoyote ya kukana jina lake isipokuwa kama hakutaka watu wahusishe na "kitu fulani" yaani Uganda.
b. W/alipoamua kutumia jina la Rwegasira ambalo kwa Watanzania wengine linawakubusha ya kina "Paul Rwegasira" na wahaya waliowazoea Oscar amefanywa awe na jina la "kitanzania", it begs the question "why"? Ukifirikia sana hakuna jina la Kitanzania per se, kwani "Patel, Dewji, Nyoni/Nyuni, Simba, Tembo, n.k" ni majina ambayo unaweza kuyakuta nchi nyingine vile vile lakini yanatumiwa na watanzania. Kwanini hili la Oscar libadilishwe? Isipokuwa pale penye ishara ya matatizo?
Ninaamini waliovurunda hili siyo Chadema kwa kuchallenge uraia wa Oscar bali CCM kwa kuufanya uwe issue. Kama Chadema wana info zile zile ambazo CCM ziliwafanya waone kutumia "Mukasa" ni kukaribisha udadisi usio wa lazima kwanini wasihoji?
Hivyo utaona kuwa kama Oscar yuko (na inaonekeana hivyo) comfortable na jina lake kama Mtanzania na hakuna chochote cha kuficha asione haya aseme "Kutumia jina langu la Rwegasira naona kumezua maneno mengi, na nimeamua kutumia jina langu la kawaida la Mukasa, kwani mimi ni Mtanzania na sina hofu na asili yangu". Na kuanzia hapo hayo ya Rwegasira wayarudishe huko huko kwenye vikao vyao na Oscar aendelee kuwa Oscar Mukasa kama anavyo/alivyo fahamika kwa wengi.
Inasikitisha kuwa CCM kwa kuamua kumbadili Oscar Mukasa kuwa Oscar Rwegasira wamekaribisha wenyewe utafiti katika maisha ya kijana huyu na hivyo kututoa kwenye kuangalia ni nani anafaa kuwa mbunge wa Biharamulo.
Hata hivyo, kama kuna sababu ya msingi ya kuhoji uraia wake (kama ilivyodokezwa na CCM katika kubadilisha majina) ni haki ya kila Mtanzania kuona sheria inafuatwa. Kama tumeweza kuhoji uraia wa Rostam tuweze kutumia hilo hilo katika kuhoji uraia wa mtu mwingine yoyote pale inapotokea sababu ya msingi (kama mtu kutaka kuwa muwakilishi wa watu).
Tatizo kubwa ni kuwa bila kumaliza huu mjadala, itakuwa ni yale yale ya RA ambapo tangu alipoibuka 1994 akiwa kijana wa kama miaka 25 maswali yameendelea kuulizwa juu ya uraia wake na hayajakoma. Sitaki Oscar ajikute anahojiwa tena juu ya uraia 2010 au huko mbeleni endapo maswali ya msingi hayatojibiwa.
Tunaposema sheria ni kipofu maana yake ni hiyo. Haiangalii mtu ana utajiri kiasi gani, amesoma kiasi gani, amefanya vitu gani n.k swali ni JE AMEFUATA SHERIA? Wenzetu katika hili wanajitahidi sana ndio mwaana hapa in the "D" wamemfunga Meya wao jela, na sehemu nyingine wamewatia pingu wabunge wao (maseneta na wawakiilishi) bila kuwaonea haya.