Mkuu hilo ulilo sema ni kweli ebu angalia alama hizi hapa kutoka Mwananchi
Wananchi 1000 wadai mahakamani uwanja wa Majimaji Songea
WANANCHI 1,000 wa Ruvuma wamefungua kesi dhidi ya Bodi ya Wadhamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakipinga chama hicho kumiliki Uwanja wa Majimaji ulioko mjini Songea.
Kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi imeanza kusikilizwa na itaendelea leo.
Katika kesi hiyo, namba 2/2009 inayosikilizwa na Jaji Mfawidhi, Stella Longway, ilifunguliwa Januari Mosi mwaka huu, wadai wanataka umiliki wa uwanja huo uwekwe wazi.
Wananchi hao wanaitaka mahakama kutamka wazi mmiliki wa uwanja huo kama ni ama Halmashauri ya Manispaa ya Songea au Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na si CCM.
Katika hati ya mashtaka, wananchi hao wamesema umiliki unaofanywa na CCM kwa sasa kwenye kiwanja hicho si wa kisheria kutokana na ujenzi wa uwanja huo ulitokana na nguvu ya wananchi.
Walidai kuwa wafanyakazi walikatwa sehemu ya mishahara yao, wafanyabiashara pamoja na watu binafsi kuchangia fedha taslimu wakati huo.
Pia, mahakama imeombwa iikataze CCM na watu wengine wakiwemo wanasiasa kufanya shughuli mbalimbali kwenye uwanja huo.
Katika kesi ya awali iliyosomwa Machi 5 na Aprili 4, mwaka huu, wakili wa walalamikaji, Edson Mbogoro aliitaka mahakama hiyo kuchukua hatua za haraka ili wananchi wa mkoa huo waweze kunufaika na kitegauchumi hicho ambacho kwa sasa kinainufaisha CCM pekee.
Hadi sasa, upande wa washtakiwa unaowakilishwa na wakili Sam Mapande haujawasilisha utetezi. Wakati huo huo, CCM ikishirikiana na wadau mbalimbali hivi karibuni wameanza mchakato wa kuukarabati uwanja huo.
Nani alitegemea kuna siku wadanganyika watajiunga pamoja kuanza kudai haki zao toka mikononi mwa dhulumati CCM?
Wacha wafanye haya waburuze mbele na nyuma wanyimie haki za watu, ila wajue tu kuna siku yana mwisho haya