Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

We mzee Makamba usidhani wanachama wenzako wamesahau uliyoyafanya Tarime! Usijikoshe kwa kutoa kafara wenzako! Amini nakwambia hutasameheka lazima yatakufika hivi karibuni LAZIMA UKATIBU UPOKONYWE SOON!
 
Tunataka wakina RA, Lowassa, Chenge, Mramba, na kundi lote la mafisadi kutimuliwa wote kama kweli wanataka hivyo, lakini hivi ni danganya toto ya asubuhi bwana, kuna mafisadi kibao
 
Mgosi Makamba ama kweli nyani haoni kundule! wewe umefanya UYUDA mara ngapi humo kwenye chama chako ulikuwa unafanya nini uchaguzi wa 2005
 
Baba January hivi hii ndio demokrasia mnayowatangazia wadanganyika kwamba imejaa sisi M........!!!!????
 
Jamani habari kutoka huko hazijaanza kunoga.

Ila mambo makubwa ambayo yamejiri huko ni
  1. Makamba amemfukuza kazi Katibu wa Jumuia ya Wazazi wa Wilaya kwa maelezo kwamba amekuwa akipeleka siri za chama CHADEMA.
  2. Mrema amefika na lori lake na jana alikuwa mjini Biharamulo akicheza muziki hadharani. Katika hotuba yake Mrema alisema kuwa MWENYE NYUMBA amekuja WAPANGAJI waondoke.
  3. Makamba amtishia mkurugenzi wa Halmashauri ya Biharamulo kwamba akiitangaza CHADEMA kuwa washindi basi ajue kuwa hana kazi.
  4. Rushwa sasa inatolewa nje nje!! CCM hawawezi tena kununua shahada kwa hiyo wameamua sasa kugawa pesa hovyo.
 
CCM hakutatulia kamwe hata kama Makamba atafukuza wote na abaki yeye tu na Msekwa.
 
Mkuu hilo ulilo sema ni kweli ebu angalia alama hizi hapa kutoka Mwananchi


Wananchi 1000 wadai mahakamani uwanja wa Majimaji Songea

WANANCHI 1,000 wa Ruvuma wamefungua kesi dhidi ya Bodi ya Wadhamani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakipinga chama hicho kumiliki Uwanja wa Majimaji ulioko mjini Songea.

Kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi imeanza kusikilizwa na itaendelea leo.

Katika kesi hiyo, namba 2/2009 inayosikilizwa na Jaji Mfawidhi, Stella Longway, ilifunguliwa Januari Mosi mwaka huu, wadai wanataka umiliki wa uwanja huo uwekwe wazi.

Wananchi hao wanaitaka mahakama kutamka wazi mmiliki wa uwanja huo kama ni ama Halmashauri ya Manispaa ya Songea au Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo na si CCM.

Katika hati ya mashtaka, wananchi hao wamesema umiliki unaofanywa na CCM kwa sasa kwenye kiwanja hicho si wa kisheria kutokana na ujenzi wa uwanja huo ulitokana na nguvu ya wananchi.

Walidai kuwa wafanyakazi walikatwa sehemu ya mishahara yao, wafanyabiashara pamoja na watu binafsi kuchangia fedha taslimu wakati huo.

Pia, mahakama imeombwa iikataze CCM na watu wengine wakiwemo wanasiasa kufanya shughuli mbalimbali kwenye uwanja huo.

Katika kesi ya awali iliyosomwa Machi 5 na Aprili 4, mwaka huu, wakili wa walalamikaji, Edson Mbogoro aliitaka mahakama hiyo kuchukua hatua za haraka ili wananchi wa mkoa huo waweze kunufaika na kitegauchumi hicho ambacho kwa sasa kinainufaisha CCM pekee.

Hadi sasa, upande wa washtakiwa unaowakilishwa na wakili Sam Mapande haujawasilisha utetezi. Wakati huo huo, CCM ikishirikiana na wadau mbalimbali hivi karibuni wameanza mchakato wa kuukarabati uwanja huo.



Nani alitegemea kuna siku wadanganyika watajiunga pamoja kuanza kudai haki zao toka mikononi mwa dhulumati CCM?
Wacha wafanye haya waburuze mbele na nyuma wanyimie haki za watu, ila wajue tu kuna siku yana mwisho haya

Yeah, viwanja vyote vilivyojengwa kwa michango na nguvu za wananchi inatakiwa vikombolewe kutoka mikononi mwa CCM na virudi kwa wananchi.
 
Sasa wakimwaga pesa mwaka huu na ahadi lukuki ambazo hadi mwakani bila bila watakoma nakwambia.....watapigwa chini woote bahati yao wapinzani tu wana njaa na ubinafsi wangeungana wangepata viti vingi sana sana mwakani.....................
 
Au CCM wanafanya vyote; kwa nini hawawezi; kama hata mkrugenzi amepigwa mkwara kuna usalama kweli hapo?
Mrema ana n guvu kiasi gani hapo? Chadema je? CCM je?
 
Tunahitaji watu kutoka uwanjani kabisa maana kuna kila dadali za kuanza kama yake ya Busanda
 
Yeah, viwanja vyote vilivyojengwa kwa michango na nguvu za wananchi inatakiwa vikombolewe kutoka mikononi mwa CCM na virudi kwa wananchi.
Yatawezekana kama mahakama zetu zitatenda haki na kuondoa woga.
 
Wadau mnajua style ya siku hizi ya wageni hasa kutoka kenya???
wananunua vyeti vya kuzaliwa pale uzazi na vifo kisha wananunua mpaka jina la ukoo ionekane kana kwamba walikuwa nchini ila walitumia muda mwingi nje ya nchi...

Nina mashaka sana na Uhamiaji na hata Usalama wa Taifa kama wanafuatilia hizi ishu kwani ni hatari sana kwa usalama wetu humu ndani.

NINA MASHAKA kama maslahi ya nchi yanalindwa ipasavyo maana hawa walumendago wanaingia na kukamata sehemu nyeti kisha wakishavuna kiasi cha kutosha wanawekeza kwao. Gadem

Kuhusu Rwegasira najua Tume wamefunika Kombe tu. kuna jambo hapo linafichwa
 
Inashangaza sana kwa Msimamizi wa Uchaguzi, Jimbo la Biharamulo Magharibi kutamka kwamba Oscar Rwegasira ni Mgombea halali wa Ubunge kwa kueleza tu kwamba yeye Oscar alizaliwa Bukoba. Hakusema na hakuthibitisha kwamba wazazi wake hawakutoka Uganda!

Swali ni kwamba: Hivi mtalii akizalia mtoto hapa Tanzania, huyo mtoto anaweza kuwa Raia? Kama jibu ni HAPANA, basi endapo William Mukasa alikuja kufanya kazi hapa kwetu akitokea Uganda, mtoto aliyemzaa akiwa hapa hawezi kuwa Raia. Na kama huyu mtoto Oscar amepewa passport ya Tanzania kwa makosa kabla hajaomba Uraia na kuukana ule wa Uganda aliozaliwa nao, basi hastahili kugombea Ubunge.
 
Makamba amtishia mkurugenzi wa Halmashauri ya Biharamulo kwamba akiitangaza CHADEMA kuwa washindi basi ajue kuwa hana kazi.

Rushwa sasa inatolewa nje nje!! CCM hawawezi tena kununua shahada kwa hiyo wameamua sasa kugawa pesa hovyo.

Wanaharakati na hususan wanasheria mko wapi? Inawezekanaje Makamba anaropoka na kutimua watu kazi bila kuchukuliwa hatua za kisheira kama vile Tanzania iko mfukoni mwake!!!

Tunahitaji watu kama Mtikila wa enzi zile wanaoweza kuthubutu kuchallenge pumba za huyu mzee ili apate kujiheshimu. Msiangalie maslahi yenu tu tafadhali, watanzania watawaheshimu sana iwapo mtageukia pia maslahi ya Taifa hili yanyozidi kuyoyoma.

Pamoja na Obama kuwakumbusha hivi karibuni, CCM wanaendelea kugeuza ushindi wowote ule wa kura kuwa ni demokrasia!!!!!

 
Inashangaza sana kwa Msimamizi wa Uchaguzi, Jimbo la Biharamulo Magharibi kutamka kwamba Oscar Rwegasira ni Mgombea halali wa Ubunge kwa kueleza tu kwamba yeye Oscar alizaliwa Bukoba. Hakusema na hakuthibitisha kwamba wazazi wake hawakutoka Uganda!

Swali ni kwamba: Hivi mtalii akizalia mtoto hapa Tanzania, huyo mtoto anaweza kuwa Raia? Kama jibu ni HAPANA, basi endapo William Mukasa alikuja kufanya kazi hapa kwetu akitokea Uganda, mtoto aliyemzaa akiwa hapa hawezi kuwa Raia. Na kama huyu mtoto Oscar amepewa passport ya Tanzania kwa makosa kabla hajaomba Uraia na kuukana ule wa Uganda aliozaliwa nao, basi hastahili kugombea Ubunge.

Mkuu huo ndio ukweli na sheria yetu ndivo inavo sema, lakini haya hayawezi kutekelezwa chini ya himaya ya mkoloni CCM, kwao wao ushindi wa kutawala uko juu ya kila kitu, wako radhi wamlinde mtu fisadi asiye raia kwa garama yoyte ile, alimradi anawapa hela ya kuhonga na kukwapua ushindi! nazidi tu kuwa na imani kwamba lakini yana mwisho haya! ipo siku tu..
 
Ipo siku mkakati wa wageni kutawala nchi hii utatimia ..wanaanzia na kupenyeza wabunge,inasikitisha sana chama cha mapinduzi kupitisha mganda kugombea urais wakati wagombea walikuwa wengi tu..kwa ninni huyu akapita machujio yote ya usalama hadi afike kaamati kuu...inaelekea kuna watu ngazi za chini na kati ambao tayari wanatumikia nchi jirani nyuma ya mpango huu.....

ule ushujaa uliooneshwa kwa kufutia uaia kina balozi bandora,mwenyekiti wa ccm bukoba..etc na kina azim premji ? au kila uamuzi hufanyika tu kama una sababu za kidola[ccm]?
 
Back
Top Bottom