Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,903
- 1,360
Gari tayari tumelipata jana likiwa limefichwa ndani ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Robert na baada ya hapo tuliwaweka askari wetu katika eneo hilo kulilinda na kumkamata dereva ama mtu yeyote ambaye atakwenda kulifungua. Tunadhani kuna mapanga humo ndani na hata magobori, kwa sababu tuna taarifa kwamba baadhi ya vijana wa Chadema walioletwa hapa, wana magobori, mapanga na majambia, alisema Kamanda. Aliongeza kuwa kama hadi jana watakuwa hawajaonekana, Polisi itawaita viongozi wa Chadema na CCM na kulivunja vioo gari hilo ili kubaini kilichomo ndani.
Asubuhi hiyo mkuu wa kamandi ya FFU Tanzania na RPC Kagera wakaamuru gari hiyo ya CHADEMA ikafanyiwe upekuzi.
Wakati huo viongozi wa CCM akiwepo Dr. Deodarus Kamala walikuwa katika Hotel iliyoko karibu kabisa (mita 50 hivi) iitwayo White House ili kupokea kwa shangwe taarifa za CHADEMA kupatikana na silaha katika gari yao.
Upekuzi ulisimamiwa na Inspector Omary kutoka makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kushuhudiwa na Mashinda na Basil Lema kutoka CHADEMA na kijana mmoja Hamisi wa Roberts Hotel. Kilikuwepo kikosi cha askari wenye silaha na kuvalia kofia za kutuliza fujo wapatao 20 pamoja na wananchi wengi waliokuja kushanga kuna nini?
Hatimaye upekuzi umehitimishwa kwa kukuta kuwa gari hilo halikuwa na kitu chochote cha hatari.
Nukuu ya kwanza inatoka katika katika gazeti- liliripoti kabla ya upekuzi kufanyika. Ya pili ni kutoka shuhuda wa upekuzi.
Kwa kuwa hakuna chochote cha hatari kilichopatikana, na kwa kuwa polisi wanakiri kulilinda gari hilo usiku kucha, basi kuna kauongo fulani ndani ya taarifa ya kufanyika vurugu huko rusahunga.
Waandishi wa habari mtusaidie sana sisi wananchi - nadhani ingekuwa vizuri kama gazeti liliporipoti kutokea kwa vurugu na kwamba polisi wanafuatilia, wangetupatia matokeo ya pilisi walichoona. Huo ndio uandishi mzuri, siyo mnatuacha hewani tu.