Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Ndio kawaida yao hao washari sana. Muda umeisha lakini wana lazimisha kuendelea na kampeni ili sheria ichukue mkondo wake halafu waanze kulalama.

Wamebanwa mbavu na wataangukia pua kesho wanacho tafuta sasa ni kuanzisha fuso na kuharibu uchaguzi.

Hivi hawawezi kujifunza japo kidogo kutoka kwa CCM? wao wamemaliza kampeni zao ndani muda na kutawanyika

Unayo mangapi hayo fuso?
 
Kampeni za mwisho za CCM zinafanyikia uwanja wa Stendi Kuu ulipofanyikia mkutano wa TLP jana.
CCM si wana uwanja wao kule juu karibia na shule ya msingi Umoja? hako kastendi kanabana sana au walijua hawataujaza ule uwanja?
 
Nimerejea mkutano wa CCM, saa 12 imepita, Makamba ndie anazungumza. Mgombea wao ameshazungumza.
Wakati naondoka mkutano wa Chadema, nimemuona RPC wa Kagera, Afande Salema akiwa na CO, FFU, afande Aneclet, nikasimamisha gari, na kushuka kuwasalimia, nikalipongeza jeshi la polisi kwa uvumilivu wa uvunjifu wa sheria ya uchaguzi kwa kuwastahimilia Chadema wakiendelea na kampeni huku saa kumi na mbili imepita.
RPC akasema ni kweli wameivumilia sana Chadema, ili ifikapo 12 na Nusu, uvumilivu, utawashinda.
CCM WAMEMALIZA KAMPENI 12:30 JUU YA ALAMA. Narejea Chadema kushuhudia Tifu!.
 
Hapa umechonganisha lolote baya tutakulaumu wewe. Ulikuwa na maana gani kumkumbusha RPC kazi yake?
 
Nimerudi Chadema, mkutano ndio unaisha 12:45 bila polisi kuingilia kati. Kama kawaida yao wanaondoka kwa maandamano yasiyo yakiongozwa na Mbowe, Polisi wanaendeleza ustahimilivu wao kwa kutoyatawanya maandamano.
Hata wana CCM wanazunguka mitaani wakiongozwa na gari zao za PA. Nawashuhudia makamanda wale wawili wamesimama njia panda kushuhudia maandamano yasiyo rasmi bila kuamrisha visago.
 
Ndio kawaida yao hao washari sana. Muda umeisha lakini wana lazimisha kuendelea na kampeni ili sheria ichukue mkondo wake halafu waanze kulalama.

Wamebanwa mbavu na wataangukia pua kesho wanacho tafuta sasa ni kuanzisha fuso na kuharibu uchaguzi.

Hivi hawawezi kujifunza japo kidogo kutoka kwa CCM? wao wamemaliza kampeni zao ndani muda na kutawanyika
w

Mozoawe,
Mukaruka wakati mwingine unapaswa kuona aibu. Wewe uko huko Kangunguli Pasco yuko Biharamulo anasema chama cha majambazi wamemaliza saa kumi na mbili na nusu wewe unasema wamemaliza kwa muda sahihi tukuelewe vipi? Hivi mshari ni yupi anayekata mapanga wenziye au yule anayepitiliza muda wa mkutano?
Halafu unasema wajifunze kutoka kwa wakora sisiemu, waifunze fujo na ufisadi?
 
Kampeni zimemalizika salama ila hali ya usalama BiMulo bado ni tete kidogo kwa sababu mashabiki wa Chadema na wa CCM wanazuka mitaani kwa michakamichaka, kama wakikutana mahali itakuwa shughuli pevu.
 
CCM si wana uwanja wao kule juu karibia na shule ya msingi Umoja? hako kastendi kanabana sana au walijua hawataujaza ule uwanja?
CCM ni wazuri kwenye mass mobilization, wangeweza kuujaza uwanja wao, tatizo wana B'iMulo, hawatabiriki.
 
Tunataka kujua kuwa nani atakuwa mshinda kutokana na kura za maoni za CCM au vipi??
 
Nimerudi Chadema, mkutano ndio unaisha 12:45 bila polisi kuingilia kati. Kama kawaida yao wanaondoka kwa maandamano yasiyo yakiongozwa na Mbowe, Polisi wanaendeleza ustahimilivu wao kwa kutoyatawanya maandamano.
Hata wana CCM wanazunguka mitaani wakiongozwa na gari zao za PA. Nawashuhudia makamanda wale wawili wamesimama njia panda kushuhudia maandamano yasiyo rasmi bila kuamrisha visago.
Hao polisi waangalie huo ustahimilivu wao usije ukawa ndio chanzo cha machafuko maana wanawalemaza watu. Kwa kuwaachia wavunje sheria wanaweza kudhani kuwa ni haki yao kuvunja sheria
 
Inawezekana kabisa kuwa CCM wakishirikiana na Tume ya Uchaguzi wanakuwa wanabaka Demokrasia na hivyo kuna uwezekano yale ya busanda kujirudia tena Biharamulo
 
Hicho ndicho ni nachosema. Kwa tume hii iliyopo, wasimamizi wa uchaguzi ambao huwa ni wakurugenzi wa wilaya jimbo lilimo na polisi wa TZ itasganza afrika kama sisiemu haitapewa ushindi.
 
Utabiri wa ushindi ni mgumu kwa sabababu Wanabimulo hawatabiriki, Kwanza ni wakmya, hawana ushabiki wa kisiasa. Kutokana na hayo, wao wanachagua mtu sio chama. Hii inamaana kati ya wagombea kama chaguo lao lipo, atachaguliwa hata bila kampeni.Nadhani hata ccm ilipopigwa chini it was a surprise, hivyo tusibiri surprise kesho jioni.
 
Pamoja na ugumu wa kutabiri mshindi, sio vibaya nikatoa tathmini yangu binafsi ya kitu ninachokiona Biharamulo, angalizo, hii ni tathmini ya nilichokiona kwa macho yangu na nilichikisikia kwa masikio yangu, yaani first hand information, sio second hand news wala hearsay.
Biharamulo ni masikini japo sio kama Busanda. Masikini wa Biharamulo, ni masini wenye wanaouchukia umasikini na wanamatumaini umasikini wao unaweza kupata ufumbuzi ukageuka utajiri. Hivyo kwa vile wana hasira na umasikini wao, ule utaratibu wa vizawadi vya kilo ya sukari, T-shirt, Kofia na fedha ya kubadili mboga, kwao ni kama dhihaki na kuwatukana. Hivyo T-shirt watavaa, kofia watajikingia jua na vumbi, sukari watapokea na mboga watabadili, lakini kura watapeleka pale moyo wao ulipowatuma.
Busanda ni masikini waliokata tamaa na hawana matumaini yoyote, hivyo mleta sukari, T-shirt na kofia, tutampatia chochote atakacho. Biharamulo sio Busanda!.
 
WanaBimulo wengi ni kabila la Wasubi, hawa ni jamii ya Wahaya wenye sura za majonzi, miili ya shidashida na mtazamo wa humble na down to earth, Wahaya wakawaida walio wengi, wana sura laini laini na miili ya neema inayoashiria wanakula vizuri, ila pia kwenye mazungumzo yao, kuna elements za kujisikia, nshomile mentality na majigambo mengi.
WanaBimulo ni wakimya sio kwa sababu hawa la kusema, bali ni wakya waliomua kukaa kimya lakini wanaonekana kujua vizuri kila kinachoendelea, yaani wakmya huku wanafikiri na kutafakari, Wahaya wa kawaida waliowengi ni boastiful na very vocal.
Hii maana yake, kama Wasubi, wanaukabila wa ndani ya damu, watanchagua mgombea wa Chadema ambaye ni Msubi mwenzao. CCM imemsimamisha Mhaya, kama Wasubi, wanawazimia Wahaya, basi watamtosa Msubi mwenzao wa Chadema na kumchagua Mhaya wa CCM.
Kutokana na tabia ya ukimya wa Wasubi, ni wagumu kutabirika, hata huyo Msubi mwenzao hawajamuonyesha matumaini ya kumpatia upendeleo wa ukabila. Hivyo kwa ukimya huo, kama wanaukabila mioyoni mwao, mgombea wa CCM hawezi kupita hata wamtakatisha kwa kumuogesha kwa pumba, na kumpaka manukato ya manemane ili aonekane vizuri machoni mwa Wasubi, na anukie vizuri puani mwao, kwao bado watasikia harufu ya uvundo, kwa sababu la kuvunda, halihitaji ubani.
 
Mji wa Biharamulo, ni vumbi vumbi vumbi tupu mpaka nyumba na majengo yamepaushwa na vumbi. Kuna hoteli mbili za maana, zilizobaki zote ni gesti. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ni choka mbaya, hata kiofisi cha serikali yangu ya mtaa ni afadhali mara mia. Huruma ya Mkurugenzi wa Halmashauri, angalau imemuondolea aibu kwa Mkuu wa Wilaya kuhifadhiwa ndani ya jengo la Halmashauri ambalo lina hadhi,
Mji mzima hakuna hoteli ya maana hata ya kupata chakula.
Siku ya kwanza tulilazimika kwenda kilomita zaidi ya 50, Akanazi kupata mlo na kujihifadhi kwenye vigesti vilivyojazana huku dada zetu wa Kihaya si haba.
Tumelazimika kufanya shughuli zetu Biharamulo na kulala Chato, kilomita 70 toka Biharamulo tena sisi ndio afadhali, Maofisa wa Tume ya Uchaguzi maisha ya Biharamulo yamewashinda kabisa, wao wanajilalia Geita, kilomita karibu 200!
 
WanaBimulo wengi ni kabila la Wasubi, hawa ni jamii ya Wahaya wenye sura za majonzi, miili ya shidashida na mtazamo wa humble na down to earth, Wahaya wakawaida walio wengi, wana sura laini laini na miili ya neema inayoashiria wanakula vizuri, ila pia kwenye mazungumzo yao, kuna elements za kujisikia, nshomile mentality na majigambo mengi.
WanaBimulo ni wakimya sio kwa sababu hawa la kusema, bali ni wakya waliomua kukaa kimya lakini wanaonekana kujua vizuri kila kinachoendelea, yaani wakmya huku wanafikiri na kutafakari, Wahaya wa kawaida waliowengi ni boastiful na very vocal.
Hii maana yake, kama Wasubi, wanaukabila wa ndani ya damu, watanchagua mgombea wa Chadema ambaye ni Msubi mwenzao. CCM imemsimamisha Mhaya, kama Wasubi, wanawazimia Wahaya, basi watamtosa Msubi mwenzao wa Chadema na kumchagua Mhaya wa CCM.
Kutokana na tabia ya ukimya wa Wasubi, ni wagumu kutabirika, hata huyo Msubi mwenzao hawajamuonyesha matumaini ya kumpatia upendeleo wa ukabila. Hivyo kwa ukimya huo, kama wanaukabila mioyoni mwao, mgombea wa CCM hawezi kupita hata wamtakatisha kwa kumuogesha kwa pumba, na kumpaka manukato ya manemane ili aonekane vizuri machoni mwa Wasubi, na anukie vizuri puani mwao, kwao bado watasikia harufu ya uvundo, kwa sababu la kuvunda, halihitaji ubani.

Si bora wangemsimamisha mhaya? mganda?

Anyway asante Pasco kwa info, majambazi wa kura tumeisha wazoea, Wenye mamlaka yaliyo tukuka walisha acha maagizo nani atangazwe mshindi, tunasubili saa na dakika itimie atangazwe!
 
.
Naomba tumtambue kwa utambulisho rasmi uliokubalika kisheria na pepar work na sio huo unaodhaniwa, hata kama ukweli halisi ni vinginevyo.
Kijani ni Mhaya!.
 
Back
Top Bottom