WanaBimulo wengi ni kabila la Wasubi, hawa ni jamii ya Wahaya wenye sura za majonzi, miili ya shidashida na mtazamo wa humble na down to earth, Wahaya wakawaida walio wengi, wana sura laini laini na miili ya neema inayoashiria wanakula vizuri, ila pia kwenye mazungumzo yao, kuna elements za kujisikia, nshomile mentality na majigambo mengi.
WanaBimulo ni wakimya sio kwa sababu hawa la kusema, bali ni wakya waliomua kukaa kimya lakini wanaonekana kujua vizuri kila kinachoendelea, yaani wakmya huku wanafikiri na kutafakari, Wahaya wa kawaida waliowengi ni boastiful na very vocal.
Hii maana yake, kama Wasubi, wanaukabila wa ndani ya damu, watanchagua mgombea wa Chadema ambaye ni Msubi mwenzao. CCM imemsimamisha Mhaya, kama Wasubi, wanawazimia Wahaya, basi watamtosa Msubi mwenzao wa Chadema na kumchagua Mhaya wa CCM.
Kutokana na tabia ya ukimya wa Wasubi, ni wagumu kutabirika, hata huyo Msubi mwenzao hawajamuonyesha matumaini ya kumpatia upendeleo wa ukabila. Hivyo kwa ukimya huo, kama wanaukabila mioyoni mwao, mgombea wa CCM hawezi kupita hata wamtakatisha kwa kumuogesha kwa pumba, na kumpaka manukato ya manemane ili aonekane vizuri machoni mwa Wasubi, na anukie vizuri puani mwao, kwao bado watasikia harufu ya uvundo, kwa sababu la kuvunda, halihitaji ubani.