Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

WanaBimulo wengi ni kabila la Wasubi, hawa ni jamii ya Wahaya wenye sura za majonzi
Hell Noo.....basubi ni tofauti na wahaya hata lugha ni tofauti na wahaya na tabia tofauti sana....huwezi kusema ni jamii ya wahaya....

miili ya shidashida na mtazamo wa humble na down to earth, Wahaya wakawaida walio wengi, wana sura laini laini na miili ya neema inayoashiria wanakula vizuri, ila pia kwenye mazungumzo yao, kuna elements za kujisikia, nshomile mentality na majigambo mengi.
mkuu usitie chumvi sana utaharibu......sehemu gani vijijini utakuta wananchi wana furaha?......alafu nani kakuambia wasubi wanakula vibaya? mkuu habarisha unalolijua kuhusu Basubi usipotoshe.....hao wahaya kula mono dayate ndizi maharage na ntula ndio wanakula vizuri?
 
Mji wa Biharamulo, ni vumbi vumbi vumbi tupu mpaka nyumba na majengo yamepaushwa na vumbi. Kuna hoteli mbili za maana, zilizobaki zote ni gesti. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ni choka mbaya, hata kiofisi cha serikali yangu ya mtaa ni afadhali mara mia. Huruma ya Mkurugenzi wa Halmashauri, angalau imemuondolea aibu kwa Mkuu wa Wilaya kuhifadhiwa ndani ya jengo la Halmashauri ambalo lina hadhi,
Mji mzima hakuna hoteli ya maana hata ya kupata chakula.
Siku ya kwanza tulilazimika kwenda kilomita zaidi ya 50, Akanazi kupata mlo na kujihifadhi kwenye vigesti vilivyojazana huku dada zetu wa Kihaya si haba.
Tumelazimika kufanya shughuli zetu Biharamulo na kulala Chato, kilomita 70 toka Biharamulo tena sisi ndio afadhali, Maofisa wa Tume ya Uchaguzi maisha ya Biharamulo yamewashinda kabisa, wao wanajilalia Geita, kilomita karibu 200!
huo ni ubadhirifu wa fedha.....nyie mlitegemea kukuta sheraton b'mulo? acheni hizo.....b'mulo una guest nzuri tu tena zinalalika.....
 
.
Naomba tumtambue kwa utambulisho rasmi uliokubalika kisheria na pepar work na sio huo unaodhaniwa, hata kama ukweli halisi ni vinginevyo.
Kijani ni Mhaya!.

Mkuu, binafsi siwezi mtambua na siku zote nitalaani kwa nguvu zangu zote uharamia na uhuni uliofanywa katika jambo hili!
Na Kibaya zaidi I know these people in person! sasa nitaidanganyaje nafsi yangu?

Mtu mzima unaye heshimika kuamua kuuficha ukweli kwa sababu yoyote ile unakuwa umejipunguzia heshima kubwa mbele ya jamii, Wana B'mlo nawaombea kwa Mungu, awape ujasiri wakutoa adhabu stahiki kwa waongo hawa! Kwani ninyi mnajua fika ukweli ni upi.

Asante mkuu
 
Mji wa Biharamulo, ni vumbi vumbi vumbi tupu mpaka nyumba na majengo yamepaushwa na vumbi. Kuna hoteli mbili za maana, zilizobaki zote ni gesti. Ofisi ya Mkuu wa Wilaya, ni choka mbaya, hata kiofisi cha serikali yangu ya mtaa ni afadhali mara mia. Huruma ya Mkurugenzi wa Halmashauri, angalau imemuondolea aibu kwa Mkuu wa Wilaya kuhifadhiwa ndani ya jengo la Halmashauri ambalo lina hadhi,
Mji mzima hakuna hoteli ya maana hata ya kupata chakula.
Siku ya kwanza tulilazimika kwenda kilomita zaidi ya 50, Akanazi kupata mlo na kujihifadhi kwenye vigesti vilivyojazana huku dada zetu wa Kihaya si haba.
Tumelazimika kufanya shughuli zetu Biharamulo na kulala Chato, kilomita 70 toka Biharamulo tena sisi ndio afadhali, Maofisa wa Tume ya Uchaguzi maisha ya Biharamulo yamewashinda kabisa, wao wanajilalia Geita, kilomita karibu 200!

Maisha yamewashinda duuuu??
Bado wanataka wasiwatendee haki masikini hawa?, umaskini muwatie kwa zaidi ya myaka 40 ya uhuru hata haki yao ya kuchagua wanaye mpenda?
Mara muwakate mapanga, mara muwapige kanisani? jamani?
 
Hell Noo.....basubi ni tofauti na wahaya hata lugha ni tofauti na wahaya na tabia tofauti sana....huwezi kusema ni jamii ya wahaya....

mkuu usitie chumvi sana utaharibu......sehemu gani vijijini utakuta wananchi wana furaha?......alafu nani kakuambia wasubi wanakula vibaya? mkuu habarisha unalolijua kuhusu Basubi usipotoshe.....hao wahaya kula mono dayate ndizi maharage na ntula ndio wanakula vizuri?
Yoyo, haya ninayoyaeleza ndiyo ninayoyaona, naomba kuwaomba radhi wale wote nitakaowagusa, don't take it personal, ni mtazamo tuu.
Hivi kuna ubishi kuwa Uzaramoni kuna njaa, wavivu na maendeleo hasi, hivi unawaona Wazaramo na sura za huzuni?. Nenda Kimanzichana na Chole samvula kashuhudie mama hajui nyumbani watakula nini, na hajala kitu, ukipita mdundika, huyoo.. na anajirusha kama aliyeshiba.
Nadhani Wahaya kula ndizi, kunafanya sura zao zinakuwa soft miili minene ya shibe sambamba na Wanyakyusa, lakini nenda Rwanda, Wahutu na Watusi wote wanakula ndizi, Watusi sura laini, Wahutu sura ngumu.
Sura za Shibe au za njaanjaa hazi uhusiano wa moja kwa moja, watu wanakula nini, mbona wasomali na waethiopia wote kwao njaa kali, pata picha ya binti wa Kihabeshi na njaa yake bado anatisha, Wakisudani ya Kusini hata na shibe yao wakoje?.
Nadhani Biharamulo lazima kuna matatizo fulani ndio maana pako nyuma kimaendeleo, ila ni afadhali kuliko baadhi ya maeneo ya kwetu Usukumani, sio kuna matatizo, bali kuna umasikini wa kutupwa na watu wasio na matumaini kabisa ya maisha bora. BiMulo wanaonyesha wana uchungu na maendeleo, kwetu hawana uchungu, because "yuo can.t miss what you never had"
 
Kwenye ramani yangu ya Logmans pocket, Chato haipo, its no where to be seen, Biharamulo ni mji mkongwe, picha ya mwaka 61 wakati wa uhuru, mji ulipendeza, ulikuwa na barabaza ya lami, leo Chato ya juzijuzi ni lami na BiMulo kongwe ni vumbi tupu, lazima kuna tatizo mahali "there must be a problem somehow,somewhere"
Inawezekana vipi, Chato ya juzi, kuna majumba ya ghorofa, modern housing estates, makao makuu ya vilaya, majengo mapya ya ghorofa ya kisasa, huku mji mkongwe Biharamulo, unaendelea kudumaa, hivi fedha za Tulawaka zimefanyia nini?. au tumbo street, hayo matumbo si tungeyaona, mbona naona kama ni njaa tupu left right and centre?!.
Ukweli nilivyoiona Chato, kama kweli ni kazi ya John Pombe, then, jamaa ni mbunge wa maisha wa Chato mpaka mwenyewe aseme basi kama Kingyemisi alivyofanya pale Mvumi. Bado najiuliza contast btn Chato na Bimulo is so huge, mpaka sasa napata maswali mengi bila majibu.
 
huo ni ubadhirifu wa fedha.....nyie mlitegemea kukuta sheraton b'mulo? acheni hizo.....b'mulo una guest nzuri tu tena zinalalika.....

Pasco,
Hapo karibu na stand kuna Guest inaitwa Ngono Lodge ya Ta Edward Bitegera ni nzuri tu.
 
Kwenye ramani yangu ya Logmans pocket, Chato haipo, its no where to be seen, Biharamulo ni mji mkongwe, picha ya mwaka 61 wakati wa uhuru, mji ulipendeza, ulikuwa na barabaza ya lami, leo Chato ya juzijuzi ni lami na BiMulo kongwe ni vumbi tupu, lazima kuna tatizo mahali "there must be a problem somehow,somewhere"
Inawezekana vipi, Chato ya juzi, kuna majumba ya ghorofa, modern housing estates, makao makuu ya vilaya, majengo mapya ya ghorofa ya kisasa, huku mji mkongwe Biharamulo, unaendelea kudumaa, hivi fedha za Tulawaka zimefanyia nini?. au tumbo street, hayo matumbo si tungeyaona, mbona naona kama ni njaa tupu left right and centre?!.
Ukweli nilivyoiona Chato, kama kweli ni kazi ya John Pombe, then, jamaa ni mbunge wa maisha wa Chato mpaka mwenyewe aseme basi kama Kingyemisi alivyofanya pale Mvumi. Bado najiuliza contast btn Chato na Bimulo is so huge, mpaka sasa napata maswali mengi bila majibu.

Usishangae mkuu, nchi hii inaendelea kwa kwenda nyuma!! Hushangai kuna sehemu nyingi tu unakuta kuna mabaki ya lami ya zamani? Ni swali zuri wanabiharamulo walipaswa kuwauliza watawala wanaokuja kuwaahidi maisha bora kwa kila mtu.
 
huo ni ubadhirifu wa fedha.....nyie mlitegemea kukuta sheraton b'mulo? acheni hizo.....b'mulo una guest nzuri tu tena zinalalika.....
Sijasema hakuna gest, wala sijasema zilizopo hazilaliki, hapa napo ni mambo ya mtazamo, nimeona hoteli mbili, gest za kumwaga, ukifika mahali ukakuta wenyeji wako wanasubiri giza liingie ndipo waoge nje na wanatakata, ukijiona huwezi .kuogea nje, utalala bila kuoga na kesho yake utatafuta pa kuogea, kwani wanaooga nje hawatakati?, kwani usafi ni kazi ya bafu?.
Biharamulo kuna sehemu kibao za .kupata chakula cha maana, lakini bado sili silali BI'Mulo kuko full, hata wakati wa Busanda, nililala Geita, Katoro gest kibao. Sasa nalala Chato. Its only a matter of choice, not of need, na kwa taarifa tuu, mimi ni mgumu,. nimeshalala mpaka ..street London wakati wa winter, chips vumbi ndio. msosi wangu, ma-ntilie hoteli yangu.
mpaka sasa naishi kwenye kibanda size ya 20ft container.
Ubadhirifu ni ubadhirifu tuu pale unapotapanya mali ya umma, bahati mbaya au nzuri, mimi sio mtumishi wa umma, not paid by taxpayers money, Imake my own money and use them as I please, Busanda sikutumwa, na Bi'Mulo sijatumwa, ni mapenzi binafsi kushuhudia harakati za kisiasa katika ujenzi wa demokrasia ya kweli.
 
Yoyo, haya ninayoyaeleza ndiyo ninayoyaona, naomba kuwaomba radhi wale wote nitakaowagusa, don't take it personal, ni mtazamo tuu.
Hivi kuna ubishi kuwa Uzaramoni kuna njaa, wavivu na maendeleo hasi, hivi unawaona Wazaramo na sura za huzuni?. Nenda Kimanzichana na Chole samvula kashuhudie mama hajui nyumbani watakula nini, na hajala kitu, ukipita mdundika, huyoo.. na anajirusha kama aliyeshiba.
Nadhani Wahaya kula ndizi, kunafanya sura zao zinakuwa soft miili minene ya shibe sambamba na Wanyakyusa, lakini nenda Rwanda, Wahutu na Watusi wote wanakula ndizi, Watusi sura laini, Wahutu sura ngumu.
Sura za Shibe au za njaanjaa hazi uhusiano wa moja kwa moja, watu wanakula nini, mbona wasomali na waethiopia wote kwao njaa kali, pata picha ya binti wa Kihabeshi na njaa yake bado anatisha, Wakisudani ya Kusini hata na shibe yao wakoje?.
Nadhani Biharamulo lazima kuna matatizo fulani ndio maana pako nyuma kimaendeleo, ila ni afadhali kuliko baadhi ya maeneo ya kwetu Usukumani, sio kuna matatizo, bali kuna umasikini wa kutupwa na watu wasio na matumaini kabisa ya maisha bora. BiMulo wanaonyesha wana uchungu na maendeleo, kwetu hawana uchungu, because "yuo can.t miss what you never had"
Wewe umezoea umbeya, na kusikiliza ububusa ...popote Tanzania utaona wenye njaa, umsakni, uduni wa miundo mbinu nk...unakutana na jamii ya watu waliopauka kwa kukosa maji...iwe pwani, kigoma, biharamulo, butiama singida ---acha umbeya wako streotype tumechoka na generalization of things, people and places without clues!!!!
 
Tunaomba Updates kwa walioko Biharamulo.

Mkuu,ukiona kimya ujue CHADEMA maji yako shingoni.
Niko mbali sana na eneo la uchaguzi lakini kwa uzoefu wangu hapa jamvini mambo si mazuri huko Biharamulo.
 
Sijasema hakuna gest, wala sijasema zilizopo hazilaliki, hapa napo ni mambo ya mtazamo, nimeona hoteli mbili, gest za kumwaga, ukifika mahali ukakuta wenyeji wako wanasubiri giza liingie ndipo waoge nje na wanatakata, ukijiona huwezi .kuogea nje, utalala bila kuoga na kesho yake utatafuta pa kuogea, kwani wanaooga nje hawatakati?, kwani usafi ni kazi ya bafu?.
Biharamulo kuna sehemu kibao za .kupata chakula cha maana, lakini bado sili silali BI'Mulo kuko full, hata wakati wa Busanda, nililala Geita, Katoro gest kibao. Sasa nalala Chato. Its only a matter of choice, not of need, na kwa taarifa tuu, mimi ni mgumu,. nimeshalala mpaka ..street London wakati wa winter, chips vumbi ndio. msosi wangu, ma-ntilie hoteli yangu.
mpaka sasa naishi kwenye kibanda size ya 20ft container
.
Ubadhirifu ni ubadhirifu tuu pale unapotapanya mali ya umma, bahati mbaya au nzuri, mimi sio mtumishi wa umma, not paid by taxpayers money, Imake my own money and use them as I please, Busanda sikutumwa, na Bi'Mulo sijatumwa, ni mapenzi binafsi kushuhudia harakati za kisiasa katika ujenzi wa demokrasia ya kweli.
una spin huna lolote mkuu......nilijua utaleta stori zakzo za majuu zisizo an tija.....kama umelala street london sio b'mulo mkuu unapotosha unayasema tunayajua......hotel gani hio ya 20 ft?
hata ukiamua kulala dar unamkia b'mulo ni juu yako lakini usiseme kuwa b'mulo hakulaliki.....wewe tuletee matokeo sio kuponda eti wasubi wamechoka choka.....na habari za kizushi kibao....
 
Zoezi la upigaji kura uchaguzi mdogo jimbo la Biharamulo Magharibi, limeanza vizuri tuu asubuhi ya leo kwa vituo kufunguliwa saa moja kamili.
Hata hivyo mpaka sasa ninapoandika, vituo vingi wameshamaliza upigaji kura hivyo kusubiri saa kumi ifike zoezi la kuhesabu kura lianze.
Hii inamaanisha turn out ni ndogo kama kawaida ya by-elections.
 
Zoezi la upigaji kura limeendelea kwa utulivu na amani ukiondoa matatizo madogo madogo ya hapa na pale.
Baadhi ya wapiga kura imekutwa picha jina limekosewa, au jina lipo picha imekosewa.
Idadi ya wasiojua kusoma na kuandika miongoni mwa wenye
Wazee ni wengi na hawakuja na watu wanaowaamini kuwapigia kura, matokeo yake wanazoa wasaidizi hapo hapo hali iliyopelekea yule msaidizi kumpigia kura mgombea tofauti na uliyemtaka. Nimeshuhudia bibi kizee mmoja ameweka kidole kwenye picha ya mgombea wa chama fulani, halafu anayempigia kura akatia tick kwa mgombea tofauti, bibi hajui kitu, kura hiyo ikakunjwa na kuishia sandukuni. Hiyo ni single incident, hali halisi ikoje kwa vituo zaidi ya 200.
 
Hapo ndipo sisiemu wanapochukua chao mapemaaaaa???? Kina TLP na wenzao walie tu
 
Nimeshuhudia bibi kizee mmoja ameweka kidole kwenye picha ya mgombea wa chama fulani, halafu anayempigia kura akatia tick kwa mgombea tofauti, bibi hajui kitu, kura hiyo ikakunjwa na kuishia sandukuni. Hiyo ni single incident, hali halisi ikoje kwa vituo zaidi ya 200.
Mimi nilisdhani upigaji kura ni siri... kumbe mlioko huko mnaruhusiwa kuchungulia mtu anampigia nani! hayo ni mapya kwangu
 
Zoezi la upigaji kura limeendelea kwa utulivu na amani ukiondoa matatizo madogo madogo ya hapa na pale.
Baadhi ya wapiga kura imekutwa picha jina limekosewa, au jina lipo picha imekosewa.
Idadi ya wasiojua kusoma na kuandika miongoni mwa wenye
Wazee ni wengi na hawakuja na watu wanaowaamini kuwapigia kura, matokeo yake wanazoa wasaidizi hapo hapo hali iliyopelekea yule msaidizi kumpigia kura mgombea tofauti na uliyemtaka. Nimeshuhudia bibi kizee mmoja ameweka kidole kwenye picha ya mgombea wa chama fulani, halafu anayempigia kura akatia tick kwa mgombea tofauti, bibi hajui kitu, kura hiyo ikakunjwa na kuishia sandukuni. Hiyo ni single incident, hali halisi ikoje kwa vituo zaidi ya 200.

Huu ndo mtaji wa... chama cha.., kuhakikisha wananchi wako choka mbaya, ili hata wakihongwa miatano inatosha, na hata kuwanyima elimu kama huyu bibi.., it is so sad karne ya 21 kutojua kusoma bado ni kwingi nchini kwetu!
 
Mimi nilisdhani upigaji kura ni siri... kumbe mlioko huko mnaruhusiwa kuchungulia mtu anampigia nani! hayo ni mapya kwangu

Kama sikosei, Watazamaji wa ndani na wa Kimataifa na waandishi wa habari huweza kuingia ndani.
 
Back
Top Bottom