Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

“Gari tayari tumelipata jana likiwa limefichwa ndani ya nyumba ya kulala wageni iitwayo Robert na baada ya hapo tuliwaweka askari wetu katika eneo hilo kulilinda na kumkamata dereva ama mtu yeyote ambaye atakwenda kulifungua. “Tunadhani kuna mapanga humo ndani na hata magobori, kwa sababu tuna taarifa kwamba baadhi ya vijana wa Chadema walioletwa hapa, wana magobori, mapanga na majambia,” alisema Kamanda. Aliongeza kuwa kama hadi jana watakuwa hawajaonekana, Polisi itawaita viongozi wa Chadema na CCM na kulivunja vioo gari hilo ili kubaini kilichomo ndani.

Asubuhi hiyo mkuu wa kamandi ya FFU Tanzania na RPC Kagera wakaamuru gari hiyo ya CHADEMA ikafanyiwe upekuzi.

Wakati huo viongozi wa CCM akiwepo Dr. Deodarus Kamala walikuwa katika Hotel iliyoko karibu kabisa (mita 50 hivi) iitwayo White House ili kupokea kwa shangwe taarifa za CHADEMA kupatikana na silaha katika gari yao.

Upekuzi ulisimamiwa na Inspector Omary kutoka makao Makuu ya Jeshi la Polisi na kushuhudiwa na Mashinda na Basil Lema kutoka CHADEMA na kijana mmoja Hamisi wa Roberts Hotel. Kilikuwepo kikosi cha askari wenye silaha na kuvalia kofia za kutuliza fujo wapatao 20 pamoja na wananchi wengi waliokuja kushanga kuna nini?

Hatimaye upekuzi umehitimishwa kwa kukuta kuwa gari hilo halikuwa na kitu chochote cha hatari
.


Nukuu ya kwanza inatoka katika katika gazeti- liliripoti kabla ya upekuzi kufanyika. Ya pili ni kutoka shuhuda wa upekuzi.
Kwa kuwa hakuna chochote cha hatari kilichopatikana, na kwa kuwa polisi wanakiri kulilinda gari hilo usiku kucha, basi kuna kauongo fulani ndani ya taarifa ya kufanyika vurugu huko rusahunga.
Waandishi wa habari mtusaidie sana sisi wananchi - nadhani ingekuwa vizuri kama gazeti liliporipoti kutokea kwa vurugu na kwamba polisi wanafuatilia, wangetupatia matokeo ya pilisi walichoona. Huo ndio uandishi mzuri, siyo mnatuacha hewani tu.
 
Kwa maana hiyo Jasusi unataka niamini habari unazotoa wewe tu? Ze Utamu amekamatwa kweli serikali ina mkono mrefu

Ipole,

Jasusi anataka uamini habari zilizoandikwa na Tanzania Daima kwi kwi kwi!!! Kazi kweli kweli; mwaka huu kweli mkulima atakula mbegu zake, baada ya hapo njaa tupu.
 
Je kama mtu akisema gari la CCM lina mabomu, je polisi hao watalikagua kama walivyofanya kwa gari la chadema?
 

Mtanzania,
Makosa ya ccm yachunguzwe kwa amri ya nani wakati ccm ndiyo dola?! umesahau Makamba alivyomtishia mkurugenzi wa Biharamulo kuwa akitangaza CHADEMA imeshinda ajue hana kazi!!! unataka polisi wasiwe na kazi?
 
Mtanzania,
Makosa ya ccm yachunguzwe kwa amri ya nani wakati ccm ndiyo dola?! umesahau Makamba alivyomtishia mkurugenzi wa Biharamulo kuwa akitangaza CHADEMA imeshinda ajue hana kazi!!! unataka polisi wasiwe na kazi?
Kauli za huyu babu zinatia kichefuchefu siku zote ni za OVYO OVYO
 
Wakuu nakumbuka mgombea ubunge kupitia Chadema aliweka pingamizi juu ya mgombea mwenza wa CCM huko biharamulo kuwa si raia.

Hivi hili sakata liliishia wapi wakuu naomba nisaidieni kwani naona kampeni zinaendelea kama kawaida huku Malecela akimnadi na kusema kuwa ni mtu safi hivyo mpigieni kura!!
 
mod muunganishe huyu eneo husika kuna majibu
 
Tume walikubali kuwa ni raia wa Tanzania na hivyo kuendelea kama kawaida tu
 
Mod, Thread ya Bi'Mulo kampeni za Mwisho imepotelea wapi?!.
Leo ndio kampeni za mwisho za Uchaguzi wa Biharamulo unaofanyika kesho zinahitimishwa.
TLP wao walihitimisha kampeni zao jana. Hawa wanajua kusoma dalili za nyakati, leo wamewapisha mafahali CCM na Chadema kuumana.
Nimehudhuria ufungaji wa kampeni ya CCM na sasa niko ufungaji kampeni ya Chadema.
 
Kama CCM wameanza kuchapa watu mapanga bila ya sababu yoyote ile unategemea nini?? Kama CCM wanatumia vyombo ya dola, Nashangaa sana kusikia kuwa hata Chiligati anasema kuwa Makanisa ni sehemu ya kampeni na hakuna sheria ya kufanyia ibada kwenye makanisa huko
 
Kampeni za mwisho za CCM zinafanyikia uwanja wa Stendi Kuu ulipofanyikia mkutano wa TLP jana. watu ni wengi, ila watu waliovalia sare za CCM za T-shirt na Cap ndio wengi zaidi kuliko wananchi wa kawaida.
Kikundi cha TOT kimefanya uhamasishaji wa hali ya juu, kwa eneo la stend, nilitegemea umati mkubwa zaidi wa wananchi kuliko mashabiki wa CCM wenye sare.
cCM imeleta safu yake ya viongozi wa juu, wakiongozwa na Makamo Mwenyekiti Msekwa.
Kama kawaida ya kampeni za mwisho ni vijembe vya piga ua garagaza.
Ushangiliaji wa WanaBimulo ni wa ajabu sana, jamaa hawashabikii vijembe, wanaBiharamulo nadhani sio wapenda shari, hivyo kampeni za kutukanana Biharamulo si mahala pake.
Nakatisha kuwaletea kampeni ya mwisho za Chadema.
 
Kwenye Kampeni ya Chadema, ndio nikuta Zitto akimwaga sera.
Leo kavalia Jeans na T-shirt nyeusi na Blazer la Brown na sio Combat kama kawa yao.
Watu ni wengi mkutano wa Chadema kuliko mkutano wa CCM, huu wingi wa watu sasa sio ushabiki tena wa helikopta ni ama hamasa kwa Chadema ama jusy curiosity ya kuwasikia kina Slaa na Zitto.
Wingi wa watu sio kigezo cha ushindi, kwani Busanda imetoa somo kuhusu makundi kwenye kampeni, CCM ilionekana hoi bin taabai na bado ikaibuka kidedea.
Zitto anaendelea kumwaga sera huku ushangiliaji wa wanaBimulo ukiwa duni vile vile kama kule CCM.
 
Mbona unasema mambo ya CCM tu mzee wangu?? Tunataka na CHADEMA
Nimeposti kuhusu Chadema, ila pia sijui imepotelea wapi. Jana nimeposti kuhusu kampeni za mwisho za TLP, thread ilikaa kidogo tuu sijui ikapotelea wapi.
Nimesaka thread za Biharamulo nikazipata mbili tuu.
Sina shaka na mamod bado naamini ni technical issues kwa sababu JF hainunuliki, japo hii go slow ya Bi'Mulo unanitia mashaka
 
Sasa hivi anaunguruma Mwenyekiti Mbowe na Combat yake. Anazungumzia umasikini wa Bi'Mulo ambao kweli maendeleo ni duni na umasikini upo japo sio kwa kiwango cha Busanda. Mji wa Biharamulo ni vumbi, vumbi vumbi kwa kwenda mbele, lami ya mwisho ni ile iliyotandikwa na mkoloni kabla ya uhuru.
Mbowe anawauliza WanaBi'Mulo kama wanafaidika na mgodi
Tulawaka.
Viongozi wa vyama vya upinzani wa CUF, NCCR na mamluki wa TLP
Wapo.
Mbowe anahitimisha kwa kusema wamejifunza kwa makosa ya Busanda, "Leo ni hakuna kulala mpaka kieleweke'.
 
Mie naona kama hali ngumu kwa chadema.au ndio wamebadili mbinu ya upiganaji?
 
Kumi na Mbili kamili imetimia, ndio muda rasmi wa mwisho wa kisheria kumalizika kwa kampeni, Mbowe bado anaunguruma na mgombea wa Chadema bado hajazungumza. Naishia hapa Chadema na kuacha mtu wa kunibrief kama watashushwa jukwaani, narejea mkutano wa CCM kuona kama nao walimaza kampeni Kuminambili juu ya alama.
 
Pasco, you do a great job, thanks mkuu, nakutegemea sana kesho na kesho kutwa pia. May God bless you.
 


Ndio kawaida yao hao washari sana. Muda umeisha lakini wana lazimisha kuendelea na kampeni ili sheria ichukue mkondo wake halafu waanze kulalama.

Wamebanwa mbavu na wataangukia pua kesho wanacho tafuta sasa ni kuanzisha fuso na kuharibu uchaguzi.

Hivi hawawezi kujifunza japo kidogo kutoka kwa CCM? wao wamemaliza kampeni zao ndani muda na kutawanyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…