ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,040
- 7,303
Kwenye siasa, chama au mgombea hujitahidi kuonyesha tabia njema zaidi wakati wa uchaguzi. Kwa hiyo kama tukichora grafu ya tabia njema za wanasiasa au vyama vya siasa basi kilele cha grafu hiyo kitakuwa siku ambazo kulikuwa na uchaguzi.
Aina ya mijadala inayochukua kipaumbele katika chaguzi zetu inanifanya nijiulize, je, ni kweli wanasiasa wetu wanatambua mahitaji ya jamii?
Chaguzi zimejaa malumbano ya kuzomeana, kurushiana mawe, kuchimbachimba mgombea gani hajakamilisha nakala gani ili awekewe pingamizi, kulumbana juu ya nani amuachie nani kugombea n.k
Nilitegemea kipindi hiki kiwe fursa kwa wananchi wote wa Tanzania kuielewa kwa ukaribu jiografia ya Biharamulo, matatizo yanayowakabili watu wake na jinsi kila chama/mgombea kilivyojidhatiti kuyatatua matatizo hayo. Badala yake, kwa mara nyingine tena, wananchi wanaanza kusikia malumbano kama ya Mbeya,Tarime,Busanda n.k
Je, katika siasa za Tanzania kuvutanavutana bila kuzungumzia sera ndio inaonekana tabia njema zaidi? Na kama hivyo ndivyo ilivyo, je, tunategemea maendeleo yaje kama mikate inayoanguka toka mbinguni?
Ni vyema mijadala mingi ikazunguka kwenye sera na mikakati endelevu.