Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Biharamulo: Kampeni, kura na matokeo!

Chama makini kama CCM kinaweza vipi kumteua mtu ambaye si raia? So nadhani hili haliendi mbali. CCM haiwezi kumpendekeza mtu awe Mbunge wakati si Raia
Ina maana wakati ule Jenerali Ulimwengu anateuliwa kwenye nafasi zile zote chama hakikuwa makini?
 
- Mkuu kama ikithibitika kwamba Oscar sio raia na aliwahi kuwa mwanachama wa Chadema huko nyuma kama Masanilo alivyosema, unasema politically Chadema hawatakuwa na kesi ya kujibu pia kama CCM?

FMEs!

KWA TAARIFA ZA SASA:
Pingamizi hilo la Chadema limetupwa nje na msimamizi wa uchaguzi, lakini kuna vitu katika ujazaji wa fomu vinatia shaka. Nafuatilia zaidi ila kwa anayeweza ampigie Msimamizi wa uchaguzi 0784 750019 Bw. Mbyana. Natarajia kupata barua ya kutupwa kwa pingamizi hilo na maelezo ya msimamizi muda si mrefu.
 
- Kama umeamua kujifanya mbumbu ni tatizo lako sio langu, yaani mimi ninaandika hoja wewe unajiona mbumbumbu halafu unataka kunilaumu mimi? Nitakusaidia vipi hapo?

- what do you have kuhusu uraia wa Ulimwengu? Weka hapa tuchambue ila na angalia usije ukajiona mbu mbumbu, Bwa! ha! ha! ah! haya weka hapa ya uraia wa Ulimwengu tuone!

- Halafu wewe si ulisema unamjua sana huyu jamaa Oscar, sasa weka hapa je ni raia au sio raia?

Repect.

FMEs!

DO we always think before typing; or we type because we have time; resource etc; Mie nimemwelewa vema mhusika; uliongea contradiction FMES na ulisahihishwa kuwa Kuna akina ULIMWENGU walishakumbwa na mambo haya; why dont you like to understand!!

My take: As per now uraia bado una utata mpaka hapo atakapothibitisha otherwise ndio maana kawekewa pingamizi; they have proof; he has to prove that their prove is wrong; otherwise huenda uchaguzi huu ukose mvuto au CCM watawekeza TLP ili Chadema washindwe; nalo ni zoezi gumu pia
 
KWA TAARIFA ZA SASA:
Pingamizi hilo la Chadema limetupwa nje na msimamizi wa uchaguzi, lakini kuna vitu katika ujazaji wa fomu vinatia shaka. Nafuatilia zaidi ila kwa anayeweza ampigie Msimamizi wa uchaguzi 0784 750019 Bw. Mbyana. Natarajia kupata barua ya kutupwa kwa pingamizi hilo na maelezo ya msimamizi muda si mrefu.

tunasubiri kwa hamu!
 
Chama makini kama CCM kinaweza vipi kumteua mtu ambaye si raia? So nadhani hili haliendi mbali. CCM haiwezi kumpendekeza mtu awe Mbunge wakati si Raia

Mzee MM hivi ni uzee au nini? Unashangaa hili wakati kuna mmoja alifikia ngazi ya mweka hazina mkuu na mpaka sasa ni mjumbe wa halmshauri kuu na NEC na si raia? Ukiwa na pesa bila kujali umezipata vp ndugu zetu wa ccm watakukumbatia tu hayo mengine ya uraia na nini sijuwi ni baadaye haisumbui.
 
Kuna watu walinotisi mara moja mabadiliko ya kutoka kutumia jina la "Mukasa" kwenda kwa "Rwegasira"... well

“Baada ya kubaini hilo na kufuatilia uhamiaji na kwingineko, wamebaini kwamba wazazi wake mgombea huyo walingia nchini mwaka 1971 wakitokea Bunyoro nchini Uganda na kuishi eneo la Misenyi,” alidai Mrema.

Alidai kuwa mgombea huyo wa CCM, alizaliwa Uganda mwaka 1970 na si katika kijiji cha Rukalagata Biharamulo kama anavyodai.

Natumaini hili eneo watakuwa wamelifanyia kazi vyema na wanayo makabrasha ya ushahidi mkononi kwani nani asiye wajua mafya wa CCM? wanaweza chonga uhamiaji document zote.. but kama wameisha wawahi na kuwa nazo hapo mzee mzima kavutwa sharubu
 
Kinachonisikitisha mimi ni elimu yake nzurri kabisa anaenda kuimalizia kwenye siasa.
 
JAMANI nadhani swala la uraia watu tumeshaliongelea hapa mpaka sheria na misahafu ikatundikwa humu. Kikubwa hapa naomba tujue kwamba..kila mtu anayo haki ya kubadilisha jina lake na kuitwa anavyotaka. Hata kama angeamua kuitwa Chungwa au embe...its him! Unless proved otherwise.

Nategemea watu humu JF tulijadili swala hili objectively. Kwanza, lazima tujue kabisa watu wengi wa Tanzania especially wa mikoa iliyo pembezoni mwa nchi kama Kagera, Kigoma, Mara nk..wengi wa wananchi wana connection na nchi jirani either kwa lugha au undugu. NA HILI ni purely geographical accident halikwepeki. Mtu wa Kigoma au Ngara definitely yuko closer na mtu wa Burundi kuliko mtu wa Rukwa kwa sababu ambazo ziko wazi kabisa. Wanaongea lugha moja! So is mtu wa Mara na mtu wa Kenya. But kasumba ambayo tunaiendekeza especially wabongo wengi..ni kuwaona raia wa hizi sehemu kama warwanda au warundi..simply because they speak similar language..same ukija Msoma..Mkurya ataambiwa..wewe kwanza ni mkenya..and on and on.. Hili lazima tulikubali kama legacy ya mipaka iliyowekwa blindly na mkoloni na kuhalalishwa na nchi zetu baada ya uhuru. Na hawa watu wameingiliana maana ndo wanasaidiana katika shida na raha..Its purely geographical accident.

Pili, lazima tujue kwamba Tanzania yetu sheria nyingi ziko kwenye mashelf wananchi waliowengi hawazijui na viongozi ambao wanapaswa kuzitekeleza wanafumba macho..zinaibuliwa pale kunapokuwa na maslahi ya watu fulani. Kwa hiyo usishangae kuona kuna warwanda, wakenya, waganda..name them..wameishi tanzania wakaoa watanzania..watoto wao wamezaliwa Tanzania..wamekulia tanzania kifupi they have known no other homeland than Tanzania. Na wamefanya yote haya bila kuulizwa na mtu. Sasa inapofika watoto kama hawa waliohangaika kama watanzania, ingawa wazazi wao either hawakuwa raia au hawakuhalalisha uraia wao.. wengine wanataka ku-participate kwenye shughuli pevu kama hizi za kisiasa..ndo sheria zinaibuliwa. Sasa huyu mtu aende wapi? mtu kazaliwa kijijini hata hiyo birth certificate hana! Yes, ni rahisi kusema kwamba watu wahalalishe uraia wao..lakini do you think..hii fursa ni wangapi wanaijua? Na swali langu kubwa..why should we punish a child kwa sababu ya makosa ya wazazi wake? Huyu hata ungemrudisha Uganda kwanza atajulikana kama Mtanzania..na at the end of the day..atakuwa Stateless. Maana hata huko hatakubalika!

Kama alivyouliza FMES..iweje kama baba siyo raia afikie level kubwa ya utumishi katika jamhuri yetu? Jibu wote tunalijua..swala la uraia ni kadi ya maslahi especially siasa. na si Tanzania tuu..its all over Africa.

Mi nadhani issue kama hizi za uraia..ni vema ku-raise legitimate questions, lakini tusiwahukumu watoto ambao wamepigana kama sisi..simply because their parents did this or that. Ni kuwanyima fursa...simply because baba au mama hakufanya kitu fulani..ni kama kumuita mtoto wa nje ya ndoa..illegitimate..its damn unfair..maana mtoto hakuhusika na maelewano ya wazazi wake..sasa kwa nini leo anyimwe haki sawa..simply because alizaliwa kwa baba aliyekimbia mimba? Think about it. NA KUNA SHERIA KAMA HIZI ARCHAIC NYINGI..BADO ZIMO KWENYE VITABU VYETU!

Ndo maana governance inatushinda, maana jiulize..ni lini hawa wanaomuwekea pingamizi walijua kwamba jamaa siyo raia? mbona hawakusema hilo mapema? Ofcourse Chadema wana haki ya kuuliza maswali kama haya..lakini..sisi kama wasomi humu JF..we should go beyond these cheap talk..tupeane ideas namna ya kuli-address hili tatizo maana kuna silent majorities wengi sana kwenye hii dilemma. Yaani baba ni wa kuja lakini mtu kazaliwa Tanzania na ameishi TZ miaka yote..leo amemaliza Chuo kikuu..amepata scholarship ya kwenda PHD nje..ananyimwa passport kwamba siyo raia..it doesnt add up..mtu kama huyo..anakuwa frustrated sana...yuko radhi kutoa rushwa yoyote apate hiyo passport.

My suggestion: Tufanye kama USA with some modifications kiasi..kila mtu ahukumiwe kama yeye! Kama umezaliwa ndani ya mipaka yetu basi wewe ni raia (with few exceptions kama wakimbizi walio chini ya uangalizi wa sheria za kimataifa..etc).... Hii itawasaidia watoto wengi..especially wanaozaliwa vijijini. Otherwise hii ni political witch hunt..ambayo inamuumiza kijana wa watu kwa kosa ambalo hakulifanya. Angalia hata CV yake..kijana ni mpiganaji..leo anaambiwa eti siyo raia..duh!

Masanja,
 
Tumeifungulia wenyewe hii sumu ya ubaguzi na itakuja kutumaliza. Badala ya kuuliza ametumikia vipi taifa hili na ana mipango gani ya baadae kwa jimbo lake sisi tunabaki kung'ang'ania ati amezaliwa upande upi wa mpaka ? Mipaka tuliyowekewa na wakoloni wetu wakati wakifyonza mvinyo Berlin bila kujali sisi wenyewe tunaishije! Kuna jamaa walisema, " rangi ya paka si muhimu, ili mradi anakamata panya." Sisi tunakazania kutafuta paka mweusi wakati panya wanatutafuna vidole! Pathetic.

Obama, Powell wangezaliwa bongo wala wasingeona ndani!

Amandla.........
 
Mimi naitwa Makoye2009 ndiyo kwanza najiunga na Jamiiforums.

Napenda kuchangia kidogo kuhusu hii habari ya mgombea wa CCM Biharamulo kubadilisha jina ghafla baada ya kuteuliwa na chama chake cha CCM kugombea ubunge. Ni dhahiri hapa kuna walakini maana kama babake mzazi alikuwa mtumishi wa umma na akiwa na majina ya William Mukasa basi tulitegema kuwa majina ya mgombea huyu yafuatane na majina ya ukoo yaani babake mzazi kama ifuatavyo: Oscar William Mukasa.

Lakini hapa tuna Oscar Rwegasira!!!Haya majina ya ukoo William Mukasa ameyaficha wapi????Kama huyu mzee William Mukasa alikuwa na jina jingine la ukoo la Rwegasira huko nyuma tunaweza kushawishika kuwa Osca kaamua kutumia jina la babu wa babu yake.

Nje ya hapo hatumwelewi huyu jamaa. Is very likely huyu jamaa anaweza kuwa na asili ya Baganda au Banyankole. Hii ya kusema kuwa baba yake alikuwa mtumishi wa umma wa siku nyingi hapa Tanzania si sababu ya kuthibitisha uraia wake.

Mara nyingi imetokea kwamba majimbo mengi yanayopakana na nchi jirani ya maingiliano ya kijamii ikiwamo kuoana na kuishi kati ya nchi mbili zinazopakana. Yawezekana kabisa kuwa kuna akina Mukasa wa Uganda na Mukasa wa Tanzania.

Uthibitisho wa hili ni vyeti vya kuzaliwa kwa familia hii ya kina Mukasa kama kweli tangu enzi za mababu walikuwa ni wazaliwa wa Biharamulo au ni wahamiaji. Kama hatakuwa na huo uthibitisho basi CCM safari hii tutawaambia WAMEFULIA HUKO BIHARAMULO.

Makoye.
 
Last edited:
Hata kama kiongozi wao atakuwa jambazi wao waachie tu ili mradi eti anayajua majhitaji na matatizo ya eneo ? Vipi usalama wa eneo na Nchi yangu Tanzania ?Kwenye chaguzi za wenzetu haya huyasikii kwa kuwa hayako hakuna mtu katoka Mexico akataka kuwa Rais wa USA so huwezi kusikia issues na sisi tuna make progress we need to clean it all .

Lunyungu,
Pitia mchakato wa wamarekani wanaodai kuwa Obama sio Raia wa Marekani.
Michakato ya namna hii ipo duniani kote, lakini kuna mazingira fulani huwa inakuwa bayana kuwa walalamikaji hawana mantiki. Ndio maana kesi ya Obama ilikataliwa na mahakama. Hii nayo ni vilevile inaelekea hukohuko, kwa sababu mchakato wa kuthibitisha kuwa mtu mwenye passport ya Tanzania sio mtanzania unahitaji ''nguvu ya ziada''.Sidhani kama CHADEMA wanayo ''nguvu ya ziada'', na kama wanayo sidhani kama ni cost effective kuitumia nguvu hiyo kwenye mchakato huu badala ya masuala muhimu zaidi kama kujitangaza kwa wananchi ambao hawawezi kutofautisha bendera ya CUF na CHADEMA.
 
Lakini jambo lililo wazi ni kuwa huyu angekuwa mgombea wa CHADEMA huu ndo ungekuwa mwisho wa safari yake kwa kuwa CCM wanayo hiyo nguvu ya ziada unayozungumzia hapa. Na hii ndo hatari ambayo wote tunaiona. Kuna watu mambo haya yanaendelea kuwatesa hadi kesho, tatizo lao ni kuwa wamekataa kukiri na kusujudia katika madhabahu ya CCM.
 
CCM wanaweza kumchagua hata Jesse Jackson na akagombea... CCM wameshika mpini na wengine wote Makali.
 
Tumeifungulia wenyewe hii sumu ya ubaguzi na itakuja kutumaliza. Badala ya kuuliza ametumikia vipi taifa hili na ana mipango gani ya baadae kwa jimbo lake sisi tunabaki kung'ang'ania ati amezaliwa upande upi wa mpaka ? Mipaka tuliyowekewa na wakoloni wetu wakati wakifyonza mvinyo Berlin bila kujali sisi wenyewe tunaishije! Kuna jamaa walisema, " rangi ya paka si muhimu, ili mradi anakamata panya." Sisi tunakazania kutafuta paka mweusi wakati panya wanatutafuna vidole! Pathetic.

Obama, Powell wangezaliwa bongo wala wasingeona ndani!

Amandla.........
Kwani Katiba inasemaje? Kama katiba imeonyesha dhahili nani anae qualify kuwa Mtanzania kwa nini tuipinge?
 
Hivi kwa Mfano mimi naitwa Ndumilakuili Kipepe na katika Documents zangu zote za shule, za kuzaliwa na Hata Passport ina hizo info, sasa naamua kugombea Ubunge naiambia tume ya Uchaguzi jina langu ni Ndumilakuili Pimbi Betina, Je kuna kosa la kisheria kwamba nimetoa taarifa za Uongo? Je ni kosa watu kunihoji imekuaje nikadanganya Majina? Wajuvi wa Sheria tuambie legal implication ya hiyo Scenario.

Asanteni
 
Tumeifungulia wenyewe hii sumu ya ubaguzi na itakuja kutumaliza. Badala ya kuuliza ametumikia vipi taifa hili na ana mipango gani ya baadae kwa jimbo lake sisi tunabaki kung'ang'ania ati amezaliwa upande upi wa mpaka ? Mipaka tuliyowekewa na wakoloni wetu wakati wakifyonza mvinyo Berlin bila kujali sisi wenyewe tunaishije! Kuna jamaa walisema, " rangi ya paka si muhimu, ili mradi anakamata panya." Sisi tunakazania kutafuta paka mweusi wakati panya wanatutafuna vidole! Pathetic.

Obama, Powell wangezaliwa bongo wala wasingeona ndani!

Amandla.........
Lazima tugeuze mawe na vyungu ili tujue kutufanyia au kufanya mambo mazuri hilo hatuna shida nalo je sheria zimefuatwa na sheria zetu zinasemaje?? Ikithibitika sio raia wala hatumfukuzi nchi yetu ni nzuri sana ataletewa form nyumbani ataomba uraia kama wengine, na tutampa na ataendelea kuwa mtanzania halali. Sheria haimpendelei mtu wala haiogopi vyeti. na tusipokuwa wakali kwa hawa wanaokwenda kutunga sheria na kutumikia wananchi na kushika ofisi zetu nyeti nchi hii itakufa. Lazima wajue muda wa kutubeza na kujichukulia nchi wanavyo taka unakaribia mwisho. Hii tabia inakuwa na kukomaa ndio maana Rostam anatesa na wengine wengi.Wapenzi wa Mukasa tulieni subirieni majibu ya pingamizi.
 
Hivi kwa Mfano mimi naitwa Ndumilakuili Kipepe na katika Documents zangu zote za shule, za kuzaliwa na Hata Passport ina hizo info, sasa naamua kugombea Ubunge naiambia tume ya Uchaguzi jina langu ni Ndumilakuili Pimbi Betina, Je kuna kosa la kisheria kwamba nimetoa taarifa za Uongo? Je ni kosa watu kunihoji imekuaje nikadanganya Majina? Wajuvi wa Sheria tuambie legal implication ya hiyo Scenario.

Asanteni
Jina lako ndiyo utambulsiho wako (identity). Unapoficha jina lako halisi na kujipachika jina lisilo lako unakuwa unaficha utambulisho wako. Na hapo si bure, kuna jambo. Ni kosa! Lazima watu wahoji. Ndiyo maana mtu akitaka kubadilisha jina lake lazima aende mahakamani
 
Chama makini kama CCM kinaweza vipi kumteua mtu ambaye si raia? So nadhani hili haliendi mbali. CCM haiwezi kumpendekeza mtu awe Mbunge wakati si Raia

mwanakijiji juzi tu ulikuwa na hoja ya RA sio raia leo unasema CCM hawawezi kuchagua mtu ambae sio Raia?hebu angalia hawa na walishika madaraka-Rostam Azizi-Iran-Iddi Simba-Burundi-J. ulimwengu mwisho alikuwa BMT kwa kuteuliwa na raisi-Burundi-Mwamedi Musa alikuwa iliyokuwa FAT-Kenya-L Masha-Americanina wasiwasi pia na mbunge wa mufindi Mh. Mungai
 
CCM wanaweza kumchagua hata Jesse Jackson na akagombea... CCM wameshika mpini na wengine wote Makali.

Huu upuuzi wa CCM wa kujifanya wao ndio wameshika makali na wao ndo wenye hati miliki ya kutawala Wadanganyika milele ndo tunaotaka kuukomesha hapa.

Angalia kule Bussanda walichofanya! Ilikuwa ni wizi mtupu! Tulisikia juu wa,wizi wa kura, ununuzi wa vitambulisho vya wapiga kura,kuwapiga wanachama na viongozi wa CHADEMA yote hayo yakifanywa na CCM na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya CCM. Hii haiwezekani kwenye nchi ambayo tunasema tunaheshimu utawala wa sheria!!!

Kama kuna ukweli hapa kuhusu uraia wa mgombea wa CCM Biharamulo tunaomba uwekwe wazi. Mbona wao waliweka pingamizi la mgombea wa CHADEMA kule Mbeya kwa kipengele cha kuhusu wapi fomu za mgombea wa CHADEMA zilisainiwa?

CCM hapa lazima kula nao sahani moja kama kweli wameweka mgombea ambaye hana sifa za uraia wa nchi yetu Tanzania na aondolowe haraka sana ili vyama vyenye sifa za wagombea viingie uringoni.
 
Last edited:
Masanilo
FMES huwa ananifurahisha sana CCM ikiwekwa angle mbaya.This time wanalo,Mukasa hebu tueleze,kulikoni gafla bin vuu ukawa Rwegasira?
 
Back
Top Bottom