Kama mlivyosikia nchi yetu Kwa mwezi Sasa tunasakata la kuuzwa Kwa BANDARI zetu huko nyuma rasilimali nyingi zimeuzwa lakini tumewaachia watu wachache watusemee hawa watu wachache nao wamechoka ,Sasa Ombi langu watanzania Kwa makundi yenu tuokoe nchi yetu ,maana kuanzia kuvuja Kwa mkataba huu Rais amekaa kimya,Bunge limekwenda kuwasaliti wananchi ,mahakama ndio hiyo ambayo jaji anaongezewa muda kanakwamba wasomi wamekwisha ,
Shime watanzania dawa iliyobaki ni kuandamana popote ulipo Kwa kufunga,kuzungumza Kwa vijiwe vyote na maeneo mengine niwashukuru chama cha wanasheria TLS Kwa kuonesha hasira zao ,niwaombe walimu,manesi,wauguzi,mabaharia,wachumi,machinga wote tupaze sauti zetu Kwa nguvu zote ,kila siku wafanyakazi wanalalama mishahara midogo ,manesi na wauguzi fanyeni kweli ,katiba yetu inatutaka tulinde rasilimali zetu muda wa kulinda ni sasa yaani kama ni nafasi ni sasa.Tujiulize swali mbona wenzetu Zanzibar wanakatiba Yao ya 2010 Sisi tunashangaa nini!!! Kwa nini watanzania ni wabinafsi sana yaani watoto wetu wataishi vipi?Kwa nini hatuwazi kesho?
Mimi wiki hii nimesambaza vipeperushi vingi maeneo ya Lindi na mtwara juu ya BANDARI zetu kuuzwa