Bila chakula mtu anaweza kuishi kwa mwka mmoja lakini bila maji ni siku tatu

Dr Akili

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Posts
5,313
Reaction score
4,751
Mtu anaweza kufunga kula chakula kwa mwaka mmoja na akabaki hai na salama. Mr Angus Barbiel, mwanaume wa Scotland, alifunga kula chakula (akiwa nyumbani kwake) kwa siku 382 kuanzia tarehe 14 June 1965 hadi tarehe 30 June 1966. Katika muda huo alikuwa anatumia tu maji, chai, kahawa na vitamins. Alikuwa na uwezo wa kutembea hadi kwenye hospitali yake ya karibu ya Maryfield Hospital for medical evaluation.

Muda wa kuishi bila kula chakula hutegemea wingi wa mafuta mtu aliyonayo mwilini mwake. Mafuta ni hifadhi ya chakula cha akiba. Kwa wanaume mengi ya haya mafuta huhifadhiwa kwenye tumbo (abdominal wall) na kuitwa kitambi. Kwa wanawake mengi ya mafuta haya huhifadhiwa kwenye makalio na chini ya ngozi (subcutaneous) na kuifanya ngozi kuwa laini yenye kuvutia. Akiba ya chakula ambayo mwili huwa inaihifadhi kwenye ini kama glycogen inatosha kwa siku tatu tu.

Hivyo mtu akifunga au kususa kula chakula mwili wake huanza kutumia hifadhi (stoke) yake ya akiba. Kwa siku takribani tatu za kwanza hutumia akiba yake ya glycogen iliyohifadhiwa kwenye ini lake. Baada ya hapo mwili huaza kutumia ile akiba yake ya mafuta (fat acids) kama chakula. Hii akiba ya mafuta ikimalizika mwili hugeukia protein zilizoko kwenye misuli (muscles) kwa kuzi deaminate na kuzitumia kama chakula. Misuli ndiyo akiba ya mwisho na baada ya hapo zikimalizika huwa hamna njia nyingine bali kurejea kwa Muumba. Huu mchakato hadi kurejea kwa Muumba huchukua miezi 3 kwa wengi lakini kwa wenye hifadhi ya kutosha kama huyo Mr Angus Barbiel wa Scotland unaweza kuchukua hata mwaka.

Asilimia 60% ya mwili wa binadamu ni maji ambayo hutumika kwenye processes mbali mbali (metabolism) ya cells za mwili. Maji haya yanahitaji constant and continuous refilling kutoka nje. Hivyo kususia kunywa maji ni suicidal attempt. Usipokunywa maji cells za mwili zitayatumia maji yaliyomo mwilini na mwili utapungukiwa maji. Hali hii inaitwa dehydration na ikiendelea ndani ya siku tatu cells zote hazitaweza kufanya kazi na utarejea kwa Muumba.

Kwa hiyo huyo jamaa aliyetishia kuanza kususa kula chakula, watu wala wasiwe na waswasi. Ameamua tu kupunguza akiba yake ya mafuta aka kitambi ambalo ni jambo jema kwa afya yake. Ila atakaposusia kunywa maji na kuwa severely dehydrated atundikwe dripu ya maji na kushitakiwa kwa kutaka kujiua (suicidal attempt).
 
Kama kuna kitu siwezi hapa duniani basi kitu hicho NI fasting .

Kufunga Kula ingekuwa NI kazi na Mshahara wake NI mnono Mimi ningekubali inipite .

Mambo gani haya ya kukaa bila Kula.
 
Akili za ki CCM hizi
 
Chaguzi alilofanya lissu si sahihi, mijitu inayotaka UKWENDEZAKO, we unasusia kula.. si wanachekelea kimtimdo
 
Sio kweli mkuu

Attachments

  • Screenshot_20250505_080552_Google.jpg
    Screenshot_20250505_080552_Google.jpg
    407.9 KB · Views: 39
Binadamu awaye yote, anapofikia kiwango chq kuushurutisha au kuutiisha mwili wake kwa kidhibiti chakula. Anakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuhimili jambo lolote linalomkabili.

Waliosema adui yako muombee njaa walijua udhaifu ulioko kwenye chakula.

Tizama watu mashuhuri, huwa hawali hovyo hata wanapoalikwa mahala. Ukifatilia hata maji hawanyi.

Chakula kina siri...

Maji ni uhai...

Imeandikwa, hatutaishi kwa mkate tuu...

Bali....

Bi. Kasinde.
 
Kama kuna kitu siwezi hapa duniani basi kitu hicho NI fasting .

Kufunga Kula ingekuwa NI kazi na Mshahara wake NI mnono Mimi ningekubali inipite .

Mambo gani haya ya kukaa bila Kula.
hayajakukuta tu, kuna watu wana vinono, wana kila kitu, ila wanafunga hadi siku tatu kavu,wengine 21 nusu kavu na wengine 7 ya maji tu, ili watafute uso wa Mungu. haujaijua dunia bado.
 
Back
Top Bottom