Bila connection hupati kazi

Bila connection hupati kazi

miyanga

Member
Joined
Dec 24, 2015
Posts
38
Reaction score
55
Wanajamvi nawasalim,

Katika vitu nimejifunza tujitahidi sana kama vijana kufanya kazi kwa bidii huku tukiwaandalia watoto wetu mazingira mazuri ya biashara, kama umemsomesha aje kuajiriwa basi fanya juu chini tengenza connection.

Vijana wengi baada ya kumaliza vyuo na kutofanikiwa kupata ajira permanent huamua kujitolea katika taasisi mbalimbali za serikali wengine kwa juhudi nidham na weledi wanaouonesha kazini hupandishwa hadi vyeo, changamoto kubwa inayowapata hawa watu ni kutokuwa na mzizi wenye connection nini namanisha ni hivi.

Unamkuta huyo mtu ni mtu mwenye cheo katika taasisi kutokana na uimara wake nidham na weledi inatokea serikali kupitia utumishi wanatangazi nafasi za kazi katika hiyo taasisi.

Kijana anaomba nafasi hiyo pamoja na wengine wanaitwa kwenye udahili kijana anajikuta hajapita au kuchaguliwa kwenye udahili anachaguliwa mtu mwingine kabisa anapata ile nafasi kijana anarudi kwenye nafasi yake ya kujitolea na kauongozi alikoteuliwa.

Waajiriwa wapya wanaripoti kazini na anapangiwa kwenye kitengo aliyopo yule kijana anaejitolea ambae hakuchaguliwa kijana anae jitolea anapewa majukumu ya kumfundisha kazi muajiriwa mpya na kumpa uzoefu wa kazi ambayo yeye aliiomba na hakuchaguliwa kwa kuambiwa hana vigezo hajafaulu interview (DUNIA HAIKO FAIR)

Kijana anaejitolea anafundisha kazi muajiriwa mpya na kumsimamia katika kazi.

Huyu kijana anaejitolea maumivu anayoyapata ni sawa na kumwagiwa pilipili na chumvi kwenye kidonda kibichi.

Kama mdau nashauri wazazi tuwatengenezee vinana connection wanafanya vizuri lakini hawapati nafasi.
 
Oyiiii nimewai mfundisha mtu kazi TANESCO ten alikuwa hajui hata kushika mouth ya computer nimemuelekeza kila kitu jamaa alikuwa msoma mita mm shule nimekwenda na Kaz nafanya vzr San wale vijana nilowaelekeza bila kinyonga huku boss akiniahid kuwa atafanya mpango nibaki pale kipindi kile hakukuwa na mambo ya interview za tume

Siku Moja wale vijana wamesha juwa Kaz kila kitu nashanga wakaletewa cheque namba kutoka makao makuu taayari wameajiriwa kipind hcho feliscni mramba ndio director mkuu wa tanesco yetu ..jmn baada ya muda nikaambiwa niondoke kwani Kaz ninayo fanya hapo wamepatikana watu wakufanya nilihudhunishwa sana Kisha nikarudi kijij kupambana na msoto na msongo wa mawazo

Nalaani hicho kitendo mkp leo na siajwai kanyaga tanesco mpk dakika hii nikiwa na shida namtuma mtu

Ila mungu akanipigani kipata kibarua sehemu fln ila Ni baada ya msoto mrefu mno

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Imenikumbusha mbali nliwah fanya kazi asasi moja ya kimataifa muda wa miaka 2 badae mkataba ulivoisha nkaanza kjuishi kwa mkataba wa miezi 6 cha ajabu nafasi niliokuwa naitumikia ikatangazwa nikaomba interview ikaitwa nkahudhuria sikuchaguliwa kaja mtu mpyaaa nkapewa nimtrain muajiriwa mpya ndo ikaww mwisho wangu pale aisseee inauma na inachoma kama pasi
 
Waajiriwa wapya wanaripoti kazini na anapangiwa kwenye kitengo aliyopo yule kijana anaejitolea ambae hakuchaguliwa kijana anae jitolea anapewa majukumu ya kumfundisha kazi muajiriwa mpya na kumpa uzoefu wa kazi ambayo yeye aliiomba na hakuchaguliwa kwa kuambiwa hana vigezo hajafaulu interview (DUNIA HAIKO FAIR)
 
Back
Top Bottom