Bila kadi sasa hupandi Mwendokasi. Waziri Mchengerwa awataka DART kutoa fursa Kwa Watanzania kuwekeza kwenye Mwendokasi

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi ) Mohamed Mchengerwa amewataka watendaji wa mradi wa mabasi yaendayo haraka ,Dar es Salaam (DART) kutoa fursa kwa watanzania wenye uwezo kuwekeza katika mradi huo ili kupunguza changamoto na kero zinazolalamikiwa hasa msongsmano wa watu katika vituo kwa muda mrefu .

Aidha amewaagiza watendaji hao kutokaa maofisini na kwenda katika vituo hivyo kutatua changamoto za wananchi.

Mchengerwa ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa kadi janja na mageti ya mfumo wa kielektroniki ulioanza kutumika kuanzia leo katika vituo mbalimbali hapa jijini.
Uzinduzi huo umefanyika katika kituo kikuu Cha mabasi hayo Kimara Mwisho na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo wananchi wa maeneo mbalimbali.

"Masuala ya kubishana bishana hatuyataki watanzania wanataka huduma ili kuepusha usumbufu mkubwa uliopo katika usafiri huu kila siku michakato isiyomalizika sitaki kuisikia na kuanzia Leo msikae maofini tokeni nendeni mkawahudumie Watanzania,"amesema Mchengerwa.

Amesema wapo watanzania wanaweza hivyo washirikishwe wawekeze kwani kama Mtanzania ana mabasi yanayokwenda Mwanza, Arusha na sehemu nyingine hawezi kushindwa kuhudumia mabasi kama haya na sio kuwaangalia wazabuni wa nje tu,.

Amewataka DART na UDART kuhakikisha mabasi yanakamilika katika maeneo yote yenye barabara hizo ikiwemo Mbagala kabla ya Desemba mwaka huu ili watanzania wafurahie matunda ya Serikali yao.

"Sisi tumeaminiwa kuhakikisha Watanzania wanapata huduma nzuri naamini mtatoa elimu zaidi kuhusu tandao wa Mwendokasi App ili Watanzania wawe na uelewa mpana katika ukataji tiketi ili kuepuka kero zilizokuwepo awali," amesema.

Amesema anaimani huduma ikiwa nzuri hata watu wenye magari yao binafsi wanaweza kuegesha magari yao na kutumia usafiri huo wenye haraka zaidi.

Mchengerwa amewataka warendaji wote katika Wizara hiyo wabadilike na kuhakikisha wanafuata muda wa mabasi kufika vituoni ili kupunguza msongamano usiokuwa na tija kwa abiria.

Amewataka watendaji kusitisha mara moja matumizi ya tiketi za karatasi na kuanza kutumia kadi janja ambazo pia amewataka kuziweka katika mfumo rafiki ili kupunguza wingi wa kadi kwa wananchi.

Mchengerwa amesisitiza kuhakikisha wanatatua na kumaliza kero ili wakifika katika majiji mengine ikiwemo Arusha, Mwanza na Mbeya hapa Dar es Salaam kusiwe na changamoto yoyote ile.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa DART Othman Kihamia amesema mfumo huo utakuwa bora na kuondoa changamoto mbalimbali zilizokuwepo mfano chenchi, foleni kwa wananchi waliokiwa wakikutana nazo huko nyuma.

"Kadi hizo zina ubora wa hali ya juu na tumejipanga kuhakikisha watanzania hawakutani na changamoto kama zilizokuwepo huko nyuma,"alisema.



=============================

Mchengerwa: Kuna uhaba wa mabasi zaidi ya 600 ya Mwendokasi, watanzania wanaweza wakaribishwe kuwekeza

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema kuwa kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ambao utumia usafiri wa Mwendokasi, ikiwemo abiria kukaa kituoni muda mrefu, kutopatiwa chenji na vitendo vibaya vinavyofanywa na baadhi madereva.

Amesema kuwa mwendokasi awali wakati mradi ulipozinduliwa waliweka utaratibu wa magari kupisha kila baada ya muda fulani ili kufanya abiria wasikae sana kwenye vituo, lakini amesema kuwa kwa sasa kuna malalamiko ya abiria kukaa muda mrefu kwenye vituo.

"Tunatambua kwamba hapo awali kabla ya kuanza mfumo huu tunaoenda kuzindua siku ya leo wananchi walipata changamoto nyingi, ukisoma kwenye mitandao ya kijamii kila Mtanzania analamika, wapo ambao walikuwa wanalalamika kuhusu nauli zao, wapo ambao walikuwa wakitoa pesa ikiwa nyingi chenji yake ilikuwa inachukua muda mrefu wakati mwingine wanakosa chenji zao"amesema

Akizungumza katika uzinduzi mfumo wa ukataji tiketi kwa njia ya Kadi kidigtali leo September 1, 2024 amesema " Kwahiyo mfumo huu unaenda kujibu hoja, unaenda kujibu maswali ya watanzania ambayo kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamikia"

Pia ameelekeza DART pamoja na UDART kuongeza ufanisi wa huduma kwa kutatua kero zilizopo pamoja na kuhakikisha mfumo uliozinduliwa unatoa huduma kama ilivyokusudiwa.

"Nendeni mkaongeze ufanisi ili kila mtanzanita anayetumia mwendokasi afurahie kuishi Dar es salaam"amesema Mchengerwa

Aidha amebainisha kuwa kuna uhitaji wa magari zaidi ya 600 ya mwendokasi kwenye njia ya 'Morogoro road' ambayo tayari inatumika kwa sasa, ambapo amesema katika njia hiyo mabasi zaidi ya 170 yanahitajika lakini pia kwenye njia ya Mbagala amesema mabasi takiribani 500 yanahitajika.

"Watanzania wa Dar es salaam wanasubiri mabasi ya Mwendokasi kwa kuwa Mabasi yaliyopo hayatoshi. Changamoto hizi watanzania wa Dar es salaam wamezizungumza muda mrefu wanataka kuona mabasi ili huduma hii ya mwendokasi ijitosheleze katika Jiji zima la Dar es salaam"amesema Mchengerwa

Ameongeza "Nimeambiwa uhitaji wa mabasi katika barabara hii zaidi ya 170 kwa barabara ya Mbagala kwa kuanzia nimeambiwa ni mabasi na watanzania kule wamesubiri kwa kuwa barabara zimekamilika, Maelekezo yangu kwa DART hakikisheni mabasi haya yanapatikana kabla ya Desemba."

Kufuatia uhaba huo ameelekeza mamlaka husika DART na UDART kukamilisha mpango wa kuleta wawekezaji, ambapo amesema kuwa sio mpaka wangojee wawekezaji kutoa nje badala yake amewaelekeza kuzungumza na wawekezaji wa kitanzania ili waweze kuwekeza kwa lengo la kuongeza ufanisi wa huduma.

"Ongezeni ubunifu wakaribisheni watanzania kushiriki kwenye zabuni za kuhudumia mabasi katika mwendokasi hapa Dar es salaam, wakaribisheni watanzania wanaweza, kuna kampuni ambazo zina magari zaidi ya 200"amesema Mchengerwa

Pia, soma:
*Nakerwa na tabia ya wakata tiketi wa Mabasi ya Mwendokasi kudai hawana chenji kila siku

*Mabasi ya Mwendokasi: Hili suala la mimi nakudai chenji wewe unanipa vocha ya VODA, kuna nini hapa?
 
[emoji2956][emoji2956]
 
Miradi ikiendeshwa kwa usimamizi wa Serikali haina tija kwakuwa hakuna watu wenye weledi na dhamira thabiti katika utendaji wa majukumu yao ,badala yake ni kuendekeza ubinafsi ambao matokeo yake ni kufuja Mali na kujilimbikizia kipato.

Wapewe watu binafsi uone mabasi ya mwendokasi yatakavyoboreshwa na kutoa huduma nzuri kwa wananchi.

Hata huu mradi wa treni ya mwendokasi ikiwa Serikali watajiroga kishupaza vichwa kuwa eti wataendesha chini ya Serikali hautodumu muda mrefu utakufa kifo cha panzi
 
Wanaweza uza hisa 49% Kwa watu binafsi na kuwapa fursa ya kuweka uongozi. Au kuleta uongozi wa watu WA nchi zingine hasa kwenye idara ya uendeshaji , manunuzi , au ukaguzi , ili kuondoa upungufu wa uthubutu,na nidhamu
 
Upuuzi upuuzi tu.hizo kadi wanazindua mara ngapi?kadi zilikuwepo baadae wakazitoa Leo Tena wanazizindua ili iweje?mradi huu wa kihuni unatakiwa ufutwe na hizo barabara zilizotumia Kodi zetu zipite gari zote
Waliona Max Malipo wanafaidi sana wakawanyima tender, nchi ngumu sana hii.

Sijui kama Max Malipo bado wana-operate Tz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…