Bila Katiba Mpya hakuna mwekezaji atakuja kuwekeza Tanzania, Kenya waula

Uwekezaji kwenye hii nchi ni mgumu sana, hata yale mabilioni ya IFAD kwaajili ya miradi ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba yako kwenye hati hati ya KULIWA na mchwa waliomzunguka Mama.
 


Ni kweli bila demokrasia kwa hapa EA hatutamfikia kenya. UN yote ipo Kenya
 
Chawa katika ubora wake rubbish
 
Ndioooooo
 
Kiroho Tanzania ilipaswa kuwa marekani ya Afrika ila sera za kipuuzi za kijamaa zimeidumaza. Hakuna mwekezaji anayeweza kuwa jasiri kuweka mtaji kwenye nchi isiyotabirika. Imagine ile administration ya JIWE!!
 
Uwekezaji na demokrasia havina uhusiano wowote, hapa unatufunga kamba.

Uwekezaji unahitaji mazingira mazuri ya kufanya biashara.
Mazingira mazuri ni sera nzuri za kibiashara, sera Kodi, Sera za fedha, uhakika wa soko la ndani na nje.

Qatar, UAE, Oman, Saudia, hata Rwanda hamna demokrasia kama yetu.
Ila wana mazingira mazuri ya uwekezaji.

Rwanda in a day (wao wanajinasibu 3hrs) unapata all the necessary docs za kampuni kufunguliwa, kupata leseni na tax docx ili ufungue akaunti ya bank.

Wazungu wasiwadanye sana mkadhani kila kitu ni demokrasia.

Na kuna mazingira ya vita (hostile environment) pia utawakuta hao hao wawekezaji.

Congo DR, mazingira ya vita, bado utawakuta Barrick na kampuni kibao za madini.

Wanajua kwenye vita na hali tete, wanavuna kila kitu bila kulipa Kodi stahiki na bila kuwa na ufuatiliaji.

Mnapoandika kwenye wall, vema kuwa na broad unaweka hoja yako kwenye context ipi??
 
Ni Kweli huku hapatabiriki Kwa sasa,

Wasubiri moto wa KATIBA mpya na Tume huru ya Uchaguzi ukolee, vikipatikana ndo waje kuwekeza.

Muda huo CCM kitakuwa chama Cha upinzani kama TADEA na NLD.πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…