Bila Katiba Mpya hakuna mwekezaji atakuja kuwekeza Tanzania, Kenya waula

Amka usingizini wewe, kwa Sasa Tanzania chini ya mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani ndio chaguo la kwanza kwa wawekezaji katika ukanda huu wa Afrika mashariki na Kati na kusini mwa Afrika, Tanzania ndio kituo Cha kwanza kwa watalii, watalii na wawekezaji kwa Sasa macho na akili zao Ni Tanzania pekee hasa baada ya juhudi kubwa zilizofanywa na mh Rais wetu mpendwa kupitia royal Tour pamoja na kuimarisha diplomasia yetu
Mkuu, wawekezaji makini wanapenda sera zinazotabirika na utawala wa sheria siyo utashi wa mtu.
 
Nchi zilizoendelea zina demokrasia. Amani na haki ndani ya katiba ndio mpango mzima. Nani awekeze Zimbabwe au South Sudan?
Rais mpya wa Kenya amesema nchi yake inakimbiliwa na waekezji kwasababu kuna demokrasia na hivyo mustakabali wake unatabilika.

Uchaguzi uliyopita umeithubitishia dunia kwamba Kenya Ina misingi imara ya kidemokrasia na hivyo haitayumbishwa na yeyote.

View attachment 2363937

Hapa Tanzania kwa katiba ya sasa ambayo imeweka nguvu na mamlaka makubwa kwa mtu (Rais), mwekezaji gani atakuja kuwekeza?

Tutaendelea kutegemea tozo kama chanzo cha mapato mpaka hapo tutakapopata katiba bora.
 
Kinachovutia wawekezaji sio katiba mpya bali ni factors nyingine kabisa ikiwemo predictability ya policies na taxes.
 
Mkuu, wawekezaji makini wanapenda sera zinazotabirika na utawala wa sheria siyo utashi wa mtu.
Uongozi wa mh mama yetu mh Samia suluhu Hassani Ni uongozi unaozingatia misingi ya Sheria na utawala Bora, Ni uongozi unaofuata taratibu zote za kisheria na kisera, Ndio sababu ya kuongezeka kwa wawekezaji hapa nchini katika kipindi hiki Cha mh Rais wetu mpendwa mama Samia suluhu Hassani
 
Nakuelewa, lakini kama akija mwingine kuna guarantee kuwa hatafanya kwa utashi wake? Historia ya hivi karibuni ya TZ inajitosheleza kwa point yangu.
 
Bwana Sexless kama tatizo ni demokrasia kwanini nchi kama Congo, Rwanda, Uchina na Mexico ambazo hazina demokrasia na utawala wa sheria ziendelee kuvutia wawekezaji wakubwa tu ???
 
Congo nafikiri unamaanisha DRC/RDC is a failed state kinachendelea kule ni looting, virtually sio uwekezaji - tangu enzi za mfalme Leopold II.

Huko kwingine ni suala la kuwa na kiongozi dikteta mwenye maono, utashi na uelewa wa mikakati thabiti ya kuiletea nchi yake maendeleo. Mfano mzuri kabisa ni wa Lee Kuan Yew wa Singapore. Bila shaka unajua habari yake. Ndiye aliyehamasisha usemi wa “benevolent dictator”. Kagame anajitahidi kufuata hilo. Tatizo la madikteta ni ile tamaa ya kutohojiwa wakijinufaisha kibinafsi.

Mexico ni demokrasia ingawa ieelemewa sana na wauza madawa ya kulevya.

China ni mfano wa kipekee wa utawala wa kundi la kidikteta lenye maono, mbinu na mikakati ya hali ya juu ya maendeleo na nguvu ya taifa. Heshima ya kipekee inamuendea Deng Xiaoping aliyepindua na kutawala China tangu 1978-1989 baada ya Mao. Huyu ndiye aliyeijenga China Mpya - the architect of Modern China kwa kuifungua na kuingiza uchumi wa soko. Ndio wakati mamia ya wawekezaji toka US na Ulaya walipovamia China na kusisimua utajiri tunaouona leo hii. Alitaka China iwe ya kidemokrasia kama Marekani na Ulaya. Lakini wahafidhina akina Xi wakaweka Breki na kurejesha enzi za kutukuza mtu mmoja - lakini bila kutibua mwelekeo wa uchumi.

TANZANIA SASA … Ni udikteta usio na vision wala utashi wa maendeleo ya nchi. Hakuna mikakati, miongozo wala taasisi imara za kuelekeza maendeleo. Mfumo wa uongozi umegubikwa na upendeleo (patronage), undugu (nepotism), uchawa (sycophancy), ufisadi (graft), wizi wa dola (kleptocracy) na kila takataka ya hujuma. Nchi imegeuzwa mgodi wa kujichotea. Hakuna mwenye uchungu na nchi. Kama vile sote ni wageni tunasaka fursa za kusanya na kusepa!

Kipaji kinachopewa uzito ni uchawa na na namna kupiga propaganda za hali ya juu kuhakikisha wananchi (mazuzu) wanatulia kwa amani huku mchezo ukiendelea.

US na Ulaya walijua kuwa hulka kuu ya binadamu ni UBINAFSI. Hivyo socialism haiwezekani (msome George Orwell katika Animal Farm) na udikteta hauna UTU. Hivyo walipambana kwa damu na jasho kutengua nguvu za wafalme na madikteta na kujiletea katiba imara zinazowahakikishia demokrasia ya kweli, haki za binadamu, uhuru wa mtu binafsi, fursa sawa, miongozo makini na uwezo wa kutekeleza mikakati thabiti ya maendeleo.

Hivyo mnapokana demokrasia na haki za binadamu na kutarajia maendeleo chini ya udikteta - eti kama China, Rwanda au Morocco jiulizeni kama kweli mnakielewa mnachojiombea. Bila kusahau kuwa kuna tyranny, despotism, dictatorship, benevolent dictatorship, petty dictatorship (udikteta uchwara), socialism, communism, democracy, socia democracy, liberal democracy, capitalism, etc. 😁 BE HONEST because only the truth will set you free.
 
Mpaka sasa, ukiacha hadithi za majukwaani, mazingira ya uwekezaji ya Tanzania bado ni ovyo sana. Hakuna kilichobadilika.
 
Congo nafikiri unamaanisha DRC/RDC is a failed state kinachendelea kule ni looting, virtually sio uwekezaji - tangu enzi za mfalme Leopold II.

Huko kwingine ni suala la kuwa na kiongozi dikteta mwenye maono, utashi na uelewa wa mikakati thabiti ya kuiletea nchi yake maendeleo. Mfano mzuri kabisa ni wa Lee Kuan Yew wa Singapore. Bila shaka unajua habari yake. Ndiye aliyehamasisha usemi wa “benevolent dictator”. Kagame anajitahidi kufuata hilo. Tatizo la madikteta ni ile tamaa ya kutohojiwa wakijinufaisha kibinafsi.

Mexico ni demokrasia ingawa ieelemewa sana na wauza madawa ya kulevya.

China ni mfano wa kipekee wa utawala wa kundi la kidikteta lenye maono, mbinu na mikakati ya hali ya juu ya maendeleo na nguvu ya taifa. Heshima ya kipekee inamuendea Deng Xiaoping aliyepindua na kutawala China tangu 1978-1989 baada ya Mao. Huyu ndiye aliyeijenga China Mpya - the architect of Modern China kwa kuifungua na kuingiza uchumi wa soko. Ndio wakati mamia ya wawekezaji toka US na Ulaya walipovamia China na kusisimua utajiri tunaouona leo hii. Alitaka China iwe ya kidemokrasia kama Marekani na Ulaya. Lakini wahafidhina akina Xi wakaweka Breki na kurejesha enzi za kutukuza mtu mmoja - lakini bila kutibua mwelekeo wa uchumi.

TANZANIA SASA … Ni udikteta usio na vision wala utashi wa maendeleo ya nchi. Hakuna mikakakati, miongozo wala taasisi imara za kuelekeza maendeleo. Mfumo wa uongozi umegubikwa na upendeleo (patronage), undugu (nepotism), uchawa (sycophancy), ufisadi (graft), wizi wa dola (kleptocracy) na kila takataka ya hujuma. Nchi imegeuzwa mgodi wa kujichotea. Hakuna mwenye uchungu na nchi. Kama vile sote ni wageni tunasaka fursa za kusanya na kusepa!

Kipaji kinachopewa uzito ni uchawa na na namna kupiga propaganda za hali ya juu kuhakikisha wananchi (mazuzu) wanatulia kwa amani huku mchezo ukiendelea.

US na Ulaya walijua kuwa hulka kuu ya binadamu ni UBINAFSI. Hivyo socialism haiwezekani (msome George Orwell katika Animal Farm) na udikteta hauna UTU. Hivyo walipambana kwa damu na jasho kutengua nguvu za wafalme na madikteta na kujiletea katiba imara zinazowahakikishia demokrasia ya kweli, haki za binadamu, uhuru wa mtu binafsi, fursa sawa, miongozo makini na uwezo wa kutekeleza na mikakati thabiti ya maendeleo.

Hivyo mnapokana demokrasia na haki za binadamu na kutarajia maendeleo chini ya udikteta - eti kama China, Rwanda au Morocco jiulizeni kama kweli mnakielewa mnachojiombea. Bila kusahau kuwa kuna tyranny, despotism, dictatorship, benevolent dictatorship, petty dictatorship (udikteta uchwara), socialism, communism, democracy, socia democracy, liberal democracy, capitalism, etc. 😁 BE HONEST because only the truth will set you free.
Bwana Drifter, umeandika mambo mengi sana muhimu, ambayo machache nakubaliana nayo kabisa. Demokrasia ni muhimu kwasababu mwanadamu anahitaji kuwa huru ili aweze kukua na kujiendeleza, japo uhalisia kuhusu suala la uwekezaji lina taswira tofauti. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya uwekezaji na demokrasia. Hili la Demokrasia na Uwekezaji ni wimbo ambao wengi hupenda kuuimba japo uhalisia wake ni mdogo, kwasababu uwekezaji unategemea zaidi ubepari uliokomaa (Imperialism) kuliko demokrasia.

Tangu kuzaliwa kwa ubepari mnamo karne ya 18, uwekezaji umekuwa ukisukumwa zaidi na haja ya kukuza faida (Maximization of Profit), eneo la uwekezaji (Area for Investment) , masoko (Market), malighafi (Natural Resources), soko nafuu la ajira (Cheap Labour) na ulinzi (Strategic Security). Hilo la demokrasia ni ziada tu, japo lina umuhimu wake ambao hauwezi kupuuzwa. Sasa hebu turudi kuchambua mifano yako mizuri kabisa uliyoitoa kuhusu Uchina na Singapore:

UCHINA: Marekani alienza kujenga mazingira ya uwekezaji nchini Uchina kuanzia mwaka 1972 kipindi Uchina iko chini ya Mao Zedong na Zhou Enlai. Japo nakubali kabisa kwamba aliyefungua Uchina alikuwa ni Deng Xiaoping. Mataifa ya Magharibi yalifanya uwekezaji nchini Uchina kwasababu ya uwepo wa soko kubwa (robust market), eneo la uwekezaji (area for investment), uwepo wa rasilimali ( available resources), soko nafuu la ajira (cheap labour) na uwezekano mkubwa wa kukuza faida (Maximization of profit). Suala la demokrasia halikuwa kipaumbele cha makampuni ya Marekani.

Mpaka sasa Uchina ndiyo taifa lenye soko nafuu la ajira dunia nzima, tena lina wataalamu wengi. Mpaka kufika mwaka 1971, mataifa ya Magharibi yalikuwa na tabaka la kati kubwa sana (The Largest Middle-Class), ambalo lilikuwa linataka mishahara mikubwa, huku serikali nayo ikiwa inatoza kodi kubwa kwa wazalishaji. Takwimu zinasema hivi, fundi Mchundo anayetengeneza gari kule Marekani kwa mwaka 1970's alilipwa $9,180 (Average Wage) kwa mwaka, pamoja na marupurupu mengine, ilhali fundi mchundo wa Uchina alilipwa asilimia 3% ya huu mshahara wa mfanyakazi wa Marekani.

Kimahesabu, kwanini ukomae kuzalisha nchini Marekani kwenye gharama wakati unaweza kupeleka viwanda vyako kule Uchina ambapo gharama za uzalishaji zipo chini, halafu kuna soko kubwa pia ??? Nadhani hili tuliangalie vizuri, tunaposema kwamba Demokrasia ndiyo iliwavutia Wamarekani kwenda kuwekeza nchini Uchina. Binafsi, nadhani maslahi na pesa rahisi ndizo zinapeleka uwekezaji nchini Uchina.

SINGAPORE: Lee Kuan Yew, ndiye aliyemshauri Deng Xiaoping kuruhusu uwekezaji kutoka nchi za Magharibi. Wachina walikuwa wanaisoma Singapore kwa miaka mingi sana na kutambua kwamba soko nafuu la ajira (Cheap Labour) ndiyo silaha kubwa ambayo wangeweza kuitumia, hasahasa ukizingatia kwamba wao ndiyo wenye taifa lenye watu wengi. Hizi mbinu za kibepari zilianza kutumika nchini Singapore, kabla ya kuigwa na Uchina. Singapore kama Uchina, ilikuwa na soko nafuu la ajira ambalo lilijaa wasomi, ndiyo maana unaona miaka ya 60's kulijaa viwanda.

Lakini mbali na hapo sababu za kijiografia, ziliwafanya wazungu wawekeze nchini Singapore, ambazo binafsi naweza kusema ndiyo eneo la uwekezaji (area for investment). Mfereji wa Malacca (The Malacca Strait) ndiyo njia kubwa ya biashara ya majini duniani kote, zaidi ya meli 60,000 zinapita pale kwa mwaka. Hivyo kuwekeza Singapore mbali na sababu za kiuchumi, pia ni sababu za kiulinzi na kimkakati (Strategic Security). Ule mfereji ukifungwa, nchi za Asia kama Uchina, Korea, Australia, Japan, Vietnam ndiyo mwisho wa habari yake.

Marekani analifahamu hivi vizuri, Uchina analifahamu hili vizuri. Kuna Jenerali wa Marekani aliwahi kunukuliwa akisema hivi "If the Chinese start a war in the Pacific, we will F*cking sail those waters and choke them at Malacca" . Hili ninalolisema hapa Raisi wa Uchina, Hu Juntao aliwahi kuliita THE MALACCA DILEMNA, ambalo ndiyo moja ya sababu kubwa iliyopelekea kutaka kujengwa kwa bandaria Bagamoyo (Bagamoyo Mega Project) na bandari ya Gwaddar (Gwaddar Port) kule nchini Pakistan. Hivyo kuwekeza Singapore na zaidi ya faida za kiuchumi tu.

MWISHO: Nakubaliana na wewe kwamba demokrasia ni muhimu, japo siyo kichocheo kikubwa cha uwekezaji. Hapa siongelei swala la maadili (Morality), bali uhalisia. Nchi za Magharibi zimeanza kuwekeza duniani kote miaka 150 hata kabla ya kuanza kueneza hii injili ya demokrasia. Sababu za kipindi hicho ndiyo sababu za kipindi hiki, hazijabadilika. Marekani amewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye Ghuba ya Uajemi (The Persian Gulf), siyo kwasababu ya Demokrasia bali maslahi ya kiuchumi na kiusalama. Uhai wa sarafu ya Marekani (The Petro-Dollar) unategemea usalama wa nchi za Ghuba ya Uajemi.

Hivyo tusijidanganye kwamba, demokrasia pekee ndiyo huleta uwekezaji. HAPANA. Hii siyo njia ya moja kwa moja (One Way Road). Kuna sababu nyingine zinazosababisha wawekezaji kufika kwenye nchi fulani. Hata huko Kenya, uwekezaji wa nchi za Magharibi ulikuwepo hata kipindi cha dikteta Daniel Arap Moi, hivyo kuna sababu za kuangalia kila nchi kivyake (Treat every case by its own merit), kuliko kuja jibu la pamoja (General Answer) kuhusu uwekezaji na demokrasi, ukilinganisha nchi za Kenya na Tanzania.

Kiujumla mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania ni MABOVU SANA, na hili halitokani na kukosa demokrasia peke yake au kuwepo kwa udikteta. Kuna masuala kedekede yanayochangia mazingira kuwa mabovu, umuhimu wa uwekezaji kwa muwekezaji (The Strategic Importance of the Investment to the investor, both financially and security-wise). Nina mengi ya kusema, pamoja na takwimu, japo sina muda wa kufanya hivyo.......
 
Uwekezaji na demokrasia havina uhusiano wowote, hapa unatufunga kamba.

Uwekezaji unahitaji mazingira mazuri ya kufanya biashara.
Mazingira mazuri ni sera nzuri za kibiashara, sera Kodi, Sera za fedha, uhakika wa soko la ndani na nje.

Qatar, UAE, Oman, Saudia, hata Rwanda hamna demokrasia kama yetu.
Ila wana mazingira mazuri ya uwekezaji.

Rwanda in a day (wao wanajinasibu 3hrs) unapata all the necessary docs za kampuni kufunguliwa, kupata leseni na tax docx ili ufungue akaunti ya bank.

Wazungu wasiwadanye sana mkadhani kila kitu ni demokrasia.

Na kuna mazingira ya vita (hostile environment) pia utawakuta hao hao wawekezaji.

Congo DR, mazingira ya vita, bado utawakuta Barrick na kampuni kibao za madini.

Wanajua kwenye vita na hali tete, wanavuna kila kitu bila kulipa Kodi stahiki na bila kuwa na ufuatiliaji.

Mnapoandika kwenye wall, vema kuwa na broad unaweka hoja yako kwenye context ipi??
Tatizo la Tanzania hatuna mfumo wa kiutawala unaoelezeka. Tuko katikati ya udikteta na demokrasia. Hivyo kesho ya nchi yetu kisera na kisheria haitabiriki , ndiyo maana wawekezaji wanatukimbia.

Nchi hizo ulizozitaja zenyewe zimejipambanua kuwa za kidikteta. Kesho (future) ya nchi hizo iko mikononi mwa madikteta kama akina Kagame na inatabirika.

Hata biblia inasema ni bora kuwa moto (demokrasia) ama baridi (dikteta), kuliko kuwa vuguvugu maana nitakutapika
 
Nadhani udikteta ni (moto), na demokrasia ni viguvugu. Maana kwenye demokrasia unaweza kuwa na wengi wajinga wajinga tu, kwa wingi wao wanafanya maamuzi ni inaonekana ni sawa kumbe wanawaingiza watu chaka.

Kama waikumbuka story ya Musa akipokea repoti ya wapelelezi nchi ya ahadi, watu wawili walikuwa relevant Kwa kuwa na Imani ya kuingia; wakijenga msingi wa kuyakabili majitu ili kuingia nchi ya ahadi.
Watu 10 walikuwa vilaza na waoga na kuwapa waliowaacha habari mbaya.

Nchi nyingi zilizofuata udikteta wakati wa transition kwenda kwenye uchumi mkubwa zilitoboza.

Wale waliobaki wanabishana, wanajadili, jambo la kuamuliwa na mtu mmoja inachukua mwaka au miaka.
Kama JPM angejadiliana na wana-CCM ua Cabinet kuhusu serikali yote kuhamia Dodoma, angepewa sound za 'feasubility study' michakato, et al.

Ila Kwa maamuzi ya ikifika mwakani nataka kila ofisi iwe Dodoma, leo hii Dodoma iko functional by 90%, jambo ambalo watangulizi wake hawakuweza.

Ngoja tuone, wakubwa wa sasa wana model gani.
 
Bwana Drifter, umeandika mambo mengi sana muhimu, ambayo machache nakubaliana nayo kabisa. Demokrasia ni muhimu kwasababu mwanadamu anahitaji kuwa huru ili aweze kukua na kujiendeleza, japo uhalisia kuhusu suala la uwekezaji lina taswira tofauti. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja baina ya uwekezaji na demokrasia. Hili la Demokrasia na Uwekezaji ni wimbo ambao wengi hupenda kuuimba japo uhalisia wake ni mdogo, kwasababu uwekezaji unategemea zaidi ubepari uliokomaa (Imperialism) kuliko demokrasia.

Tangu kuzaliwa kwa ubepari mnamo karne ya 18, uwekezaji umekuwa ukisukumwa zaidi na haja ya kukuza faida (Maximization of Profit), eneo la uwekezaji (Area for Investment) , masoko (Market), malighafi (Natural Resources), soko nafuu la ajira (Cheap Labour) na ulinzi (Strategic Security). Hilo la demokrasia ni ziada tu, japo lina umuhimu wake ambao hauwezi kupuuzwa. Sasa hebu turudi kuchambua mifano yako mizuri kabisa uliyoitoa kuhusu Uchina na Singapore:

UCHINA: Marekani alienza kujenga mazingira ya uwekezaji nchini Uchina kuanzia mwaka 1972 kipindi Uchina iko chini ya Mao Zedong na Zhou Enlai. Japo nakubali kabisa kwamba aliyefungua Uchina alikuwa ni Deng Xiaoping. Mataifa ya Magharibi yalifanya uwekezaji nchini Uchina kwasababu ya uwepo wa soko kubwa (robust market), eneo la uwekezaji (area for investment), uwepo wa rasilimali ( available resources), soko nafuu la ajira (cheap labour) na uwezekano mkubwa wa kukuza faida (Maximization of profit). Suala la demokrasia halikuwa kipaumbele cha makampuni ya Marekani.

Mpaka sasa Uchina ndiyo taifa lenye soko nafuu la ajira dunia nzima, tena lina wataalamu wengi. Mpaka kufika mwaka 1971, mataifa ya Magharibi yalikuwa na tabaka la kati kubwa sana (The Largest Middle-Class), ambalo lilikuwa linataka mishahara mikubwa, huku serikali nayo ikiwa inatoza kodi kubwa kwa wazalishaji. Takwimu zinasema hivi, fundi Mchundo anayetengeneza gari kule Marekani kwa mwaka 1970's alilipwa $9,180 (Average Wage) kwa mwaka, pamoja na marupurupu mengine, ilhali fundi mchundo wa Uchina alilipwa asilimia 3% ya huu mshahara wa mfanyakazi wa Marekani.

Kimahesabu, kwanini ukomae kuzalisha nchini Marekani kwenye gharama wakati unaweza kupeleka viwanda vyako kule Uchina ambapo gharama za uzalishaji zipo chini, halafu kuna soko kubwa pia ??? Nadhani hili tuliangalie vizuri, tunaposema kwamba Demokrasia ndiyo iliwavutia Wamarekani kwenda kuwekeza nchini Uchina. Binafsi, nadhani maslahi na pesa rahisi ndizo zinapeleka uwekezaji nchini Uchina.

SINGAPORE: Lee Kuan Yew, ndiye aliyemshauri Deng Xiaoping kuruhusu uwekezaji kutoka nchi za Magharibi. Wachina walikuwa wanaisoma Singapore kwa miaka mingi sana na kutambua kwamba soko nafuu la ajira (Cheap Labour) ndiyo silaha kubwa ambayo wangeweza kuitumia, hasahasa ukizingatia kwamba wao ndiyo wenye taifa lenye watu wengi. Hizi mbinu za kibepari zilianza kutumika nchini Singapore, kabla ya kuigwa na Uchina. Singapore kama Uchina, ilikuwa na soko nafuu la ajira ambalo lilijaa wasomi, ndiyo maana unaona miaka ya 60's kulijaa viwanda.

Lakini mbali na hapo sababu za kijiografia, ziliwafanya wazungu wawekeze nchini Singapore, ambazo binafsi naweza kusema ndiyo eneo la uwekezaji (area for investment). Mfereji wa Malacca (The Malacca Strait) ndiyo njia kubwa ya biashara ya majini duniani kote, zaidi ya meli 60,000 zinapita pale kwa mwaka. Hivyo kuwekeza Singapore mbali na sababu za kiuchumi, pia ni sababu za kiulinzi na kimkakati (Strategic Security). Ule mfereji ukifungwa, nchi za Asia kama Uchina, Korea, Australia, Japan, Vietnam ndiyo mwisho wa habari yake.

Marekani analifahamu hivi vizuri, Uchina analifahamu hili vizuri. Kuna Jenerali wa Marekani aliwahi kunukuliwa akisema hivi "If the Chinese start a war in the Pacific, we will F*cking sail those waters and choke them at Malacca" . Hili ninalolisema hapa Raisi wa Uchina, Hu Juntao aliwahi kuliita THE MALACCA DILEMNA, ambalo ndiyo moja ya sababu kubwa iliyopelekea kutaka kujengwa kwa bandaria Bagamoyo (Bagamoyo Mega Project) na bandari ya Gwaddar (Gwaddar Port) kule nchini Pakistan. Hivyo kuwekeza Singapore na zaidi ya faida za kiuchumi tu.

MWISHO: Nakubaliana na wewe kwamba demokrasia ni muhimu, japo siyo kichocheo kikubwa cha uwekezaji. Hapa siongelei swala la maadili (Morality), bali uhalisia. Nchi za Magharibi zimeanza kuwekeza duniani kote miaka 150 hata kabla ya kuanza kueneza hii injili ya demokrasia. Sababu za kipindi hicho ndiyo sababu za kipindi hiki, hazijabadilika. Marekani amewekeza kwa kiwango kikubwa kwenye Ghuba ya Uajemi (The Persian Gulf), siyo kwasababu ya Demokrasia bali maslahi ya kiuchumi na kiusalama. Uhai wa sarafu ya Marekani (The Petro-Dollar) unategemea usalama wa nchi za Ghuba ya Uajemi.

Hivyo tusijidanganye kwamba, demokrasia pekee ndiyo huleta uwekezaji. HAPANA. Hii siyo njia ya moja kwa moja (One Way Road). Kuna sababu nyingine zinazosababisha wawekezaji kufika kwenye nchi fulani. Hata huko Kenya, uwekezaji wa nchi za Magharibi ulikuwepo hata kipindi cha dikteta Daniel Arap Moi, hivyo kuna sababu za kuangalia kila nchi kivyake (Treat every case by its own merit), kuliko kuja jibu la pamoja (General Answer) kuhusu uwekezaji na demokrasi, ukilinganisha nchi za Kenya na Tanzania.

Kiujumla mazingira ya uwekezaji nchini Tanzania ni MABOVU SANA, na hili halitokani na kukosa demokrasia peke yake au kuwepo kwa udikteta. Kuna masuala kedekede yanayochangia mazingira kuwa mabovu, umuhimu wa uwekezaji kwa muwekezaji (The Strategic Importance of the Investment to the investor, both financially and security-wise). Nina mengi ya kusema, pamoja na takwimu, japo sina muda wa kufanya hivyo.......
Nawe umeandika mengi lakini umeshindwa kuelewa hoja yangu ya msingi. Kwa kifupi, sijasema demokrasia ni lazima kwa kuvutia wawekezaji. Sote tunajua wawekezaji wanavutiwa na mazingira rafiki ya uwekezaji haijalishi yamekujaje. Nilichoeleza ni kuhusu hoja yako kwamba mbona uwekezaji unashamiri kwenye nchi zisizo na demokrasia km Rwanda, DRC, China, etc?

Nilichosema ni kuwa kuna madikteta wenye vision, mikakati na utashi wa maendeleo. Hawa hutengeneza mazingira sahihi kuvutia uwekezaji na maendeleo ya kasi katika nchi zao. Nikakupa mifano ya Lee Kuan Yew na Deng Xiaoping. Nikagusia na Kagame anavyojaribu. Hawa “benevolent dictators” wanaruka kiunzi cha demokrasi kujiletea maendeleo katika nchi zao - lakini kwa gharama ya kuminya utawala bora, uhuru na haki za binadamu za watu wao.

Udikteta kama wa DRC au Equatorial Guinea hauna vision unapelekea kwenye failed state. Wawekezaji huko ni wezi tu wa rasilimali - looters, period.

Hapa Tanzania tujiulize tumesimama wapi na tunataka nini hasa, HONESTLY? Sirudii niliyokwishaandika. Bila shaka nimeeleweka.

US na Ulaya wamefika juu zaidi kwa kuelewa kuwa maendeleo ya kweli LAZIMA yaambatane na demokrasia ili yamfaidishe mwananchi. Kwao quality of life must be high. Ndio maana wengi wanakimbilia huko. Hivyo kwao hoja ya benevolent dictatorship kwa ajili ya kuvutia uwekezaji na maendeleo ni hoja muflisi (fallacy). They are above that.
 
Uwekezaji kwenye hii nchi ni mgumu sana, hata yale mabilioni ya IFAD kwaajili ya miradi ya ufugaji wa samaki kupitia vizimba yako kwenye hati hati ya KULIWA na mchwa waliomzunguka Mama.
Hii imekaaje mkuu? naona manispaa ya ilemela wanaiongelea sana
 
Rais mpya wa Kenya amesema nchi yake inakimbiliwa na wawekezji kwasababu kuna demokrasia na hivyo mustakabali wake unatabirika.

Uchaguzi uliyopita umeithubitishia dunia kwamba Kenya Ina misingi imara ya kidemokrasia na hivyo haitayumbishwa na yeyote.

View attachment 2363937

Hapa Tanzania kwa katiba ya sasa ambayo imeweka nguvu na mamlaka makubwa kwa mtu (Rais), mwekezaji gani atakuja kuwekeza?

Tutaendelea kutegemea tozo kama chanzo cha mapato mpaka hapo tutakapopata katiba bora.
Katiba mpya itakuja ila itakuwa imechelewa sana kwenda na nyakati
 
Back
Top Bottom