Bila kujali kelele na yaliyosemwa juu ya Hayati Magufuli, kuna ulazima wa haraka sana kumpata mwingine wa aina yake

Bila kujali kelele na yaliyosemwa juu ya Hayati Magufuli, kuna ulazima wa haraka sana kumpata mwingine wa aina yake

Una ushahidi kazi kupayuka tu,muliropoka kwa Sabaya kawabwaga Mahakamani mmebaki na aibu.
Weka evidence hapa kwamba watu waliokufa walikufa kwa amri ya JPM,hatutaki hoja za Facebook hapa JF!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Mahakama zipi za kuweza kudhibitisha uchafu wa kiongozi aliyekuwa anatumwa na rais? Tungekuwa na mahakama za haki tusingeona wawekezaji wakitaka mashauri Yao yakaamuliwe kwenye mahakama za nje.

Tungekuwa na mahakama huru na vyombo huru vya uchuguzi, kuanzia huyo magu Hadi hilo genge lake la kina sabaya, makonda nk uovu wao ungewekwa hadharani. Unasema Sabaya Kawabwaga mahakamani, kwenye mahakama hizi hizi zinazopigiwa simu Moja?!
 
JPM alipaswa awe kiongozi wa juu wa nchi amabazo azina mfumo wa kidemokrasia, hakika angeweza kuijenga hiyo nchi.

Huku kwenye demokrasia, angeishia kama alivyo ishia, kuua, kuumiza, kunyang'anya na kupora,

Aliipenda nchi hii na kuwapenda wanao msikiliza na kumtii, Aliwachukia wote wenye mawazo mbadala na tofauti na yeye,

Kama kuna mtu anamtaka JPM mwingine, atengeneze nchi yake kisha ampeleke huko sio hapa kwetu.
JPM angekuwa kiongozi mzuri sana kama angeitenga kanda ya ziwa iwe nchi. Ajiuzulu Urais wa Tanzania na awe raisi wa hiyo nchi . Aliwapenda sana ndugu zake mwishowe wakawa wanafiki kwake. Hela walizopiga badala ya kutengeneza ajira walliishia kununua magari na kuongeza vimada. Aliwasihi wanunue viwanja chato wao wakaona ujinga. Alikuwa na vision kubwa sana kwa Kanda ya Ziwa. Angeshinda hadi tuzo ya Nobel.
 
JPM angekuwa kiongozi mzuri sana kama angeitenga kanda ya ziwa iwe nchi. Ajiuzulu Urais wa Tanzaniana awe raisi wa hiyo nchi . Aliwapenda sana ndugu zake mwishowe wakawa wanafiki kwake. Hela walizopiga badala ya kutengeneza ajira walliishia kununua magari na kuongeza vimada. Aliwasihi wanunue viwanja chato wao wakaona ujinga. Alikuwa na vision kubwa sana kwa Kanda ya Ziwa. Angeshinda hadi tuzo ya Nobel.
Kwa bahati mbaya kabisa, nadhani hili huna ushahidi nalo zaidi tu kwa sasa upo ili ulinde tonge lako
 
Kipindi cha JPM kulikuwa na unafiki wa hali yajuu. Na ni kipindi ambacho watu wasiopenda kazi(wanasiasa) walipiga sana hela. Waliokuwa wanafanya kazi hawakupandishiwa mishahara. Waliokuwa wanajituma na biashara walifungiwa akaunti zao za bank na pesa zao kuchukuliwa. Kuna watu walifunguliwa kesi za kudaiwa kodi toka miaka ya tisini ili waondoke kariakoo ili Jpm aweke watu wake kariakoo. Serikali haitakiwi kupewa kipaumbele, viongozi wanatakiwa waishi maisha ya chini sana. Kipindi hicho hicho ndio kwa mara ya kwanza watu waliteuliwa kishabiki bila kuangaliwa uwezo. Mama Samia anaendeleza alichofanya JPM, amejaza watu wa visiwani kama JPM alivyojaza watu wa kanda ya ziwa, anaipendelea ZNZ kama JPM alivyopendelea chato na kanda ya ziwa. Tatizo sio Rais tatizo ni mfumo na JPM ndiye Rais pekee aliyetumia nguvu zake za kikatiba kwa asilimia 100. JPM alikuwa Rais wa wavivu na wategemezi. Nawataarifu watanzania wenzangu zama za ujamaa hazipo hakuna atakayekuja kukutetea na kukubeba. Kwenye maisha inabidi ujipambanie wewe mwenyewe.Tanzania hatuendelei kwa sababu bado watu wanashikilia sera za kijamaa ambazo zilitoweka dunia nzima toka miaka ya 90.
Ukweli 100% ndani ya bandiko hili.
 
Nimepitia maoni ya watu lakini nimegundua kwamba watu wengi hawajui bayana nini au nani hasa mchawi wa kuwepo kwa hali hii mbaya iliyopo hapa nchini?
Tz tunahitaji taasisi imara na madhubuti kabisa ya kuweza kutuvusha hapa tulipo na kusonga mbele. Mahali pa kuanzia mabadiliko ni kupatikana kwa Katiba Mpya itakayotokana na Maoni, Mawazo na Fikra za Raia wote wa nchi hii.
Exactly. Mambo sijui ya kutaka kuongozwa na walevi wa madaraka hayana nafasi.
 
Hata kama staandika matarajio yenu, kifupi ni kwamba, Tanzania inahitaji tena na kwa haraka mno mtu mwenye mfanano na hayati JPM,

Watanzania acheni kuendekeza ujinga, uzembe na ulalamishi

Wengi wenu ni walalamishi na msiopenda kabisa kufanya kazi, (wavivu wa kupindukia) mnapenda starehe bila kujali mnachoingiza

Familia zote masikini chanzo ni baba legelege, baba asiyeweka mfumo na mwongozo thabiti juu ya watoto wake, ni kuandaa mababa wengine walioferi maisha tokea kwa makuzi yao

Nikikumbuka kipindi cha huyo mwamba, kila mtu alipenda kufanya kazi, maofisini nako vile vile kwa sababu baba alikuwa ni mchapa kazi, mkemea uzembe, mkemea wezi na kila maovu, JPM aliwakemea mpaka viongozi wastasfu kwa sababu alijua nini anafanya juu ya nchi hii yenye watu masikini na sio tu masini, bali pia ni nchi yenye wajinga wenge!

Hayati Magufuli alikuwa ni mwalimu mzuri wa mapato na matumizi pia, kila kilichokuwa kikipatikana, kilielekezwa sehemu hisika tu na kufuatiliwa kwa ukaribu

Na ndiyo maana karibu kila mradi ulikuwa ukienda vema kwa sababu shilingi ilikuwa haipotei ovyovyo,

Nikiangalia sasa tulipo na tunavyokwenda, tumekopa matrilioni ya shilingi, na bado miradi ya kimkakati inasuasua, nani aseme tupo kwenye njia sahihi? Hivi ni nani mpaka muda huu kawajibishwa kwenye ripot ya CAG iliyovunja records ya upotevu wa mabilion ya shilingi, nani kajihudhuru walau tuweke imani kwa wanaotuongoza? Nani kafikishwa mahakamani ili tuseme tunatendea haki wananchi??

Mgogoro wa Wizara ya Nishati na wananchi, ni kama kumekosekana mtu wa kuutibu huu mgogoro, visingizio viingi na havijawahi kuisha, kwa nini tuwe na mgao wa umeme?? Tunakosa nini yaani, mwenye jibu wa swali hili nitamlipia ya bando la mwezi mzima, kwa nini kuwe na mgao wa umeme Tanzania kama siyo ulegelege na uzembe tu uliokubuhu?

Kama tunataka kuwa nchi inayopiga hatua kiuchumi na kuwa nchi inayoheshimika nje ndani, basi tunamhitaji mfano wa mtu aliyepita, yaani JPM asiyeogopa kufa kwa ajili ya maisha ya wengi ili akabiliane na wezi, mafisadi, wazembe na makuwadi wa kisiasa na machawa yaliyokosa kazi za kufanya, yanaabudu watu ili yalipwe badala ya kufanya kazi halali!

Wale kufokafoka karibuni mfoke, na sababu ni moja tu, maslahi yenu yaliyojengwa kwenye wizi na ujanjaunja, ndiyo huwa hamtakaki viongozi kama hao!

Mwisho, Ipo siku itajulikana iwapo Rasilimali Mungu alizotupa zilipaswa kulindwa kwa nguvu na kwa jicho la husuda kama alivyokuwa akifanya JPM na au tuendelee kuziona ni kama Mungu alituwekea kwa bahati mbaya na hatuzitaki!
Hakika
 
JPM amesahihisha au ameleta uchafu wa aina nyingine? Mbaguzi huyu, muuaji, msababisha hasara, …. Hivi watanzania akili zenu zipo wapi?
Shida yako wewe ni mdini. Kobaz zilipokubana ukadhani ni Jpm.

Kimsingi nyie watu wa Ulojo msingempenda Jpm
 
22112018.jpg
Screenshot_20221119-094007.png
Screenshot_20221119-093841.png
 
Back
Top Bottom