Bila kujirudi, Kassim Majaliwa atapigwa chini!

Kwa maoni yangu, huku nilipo, naisaidia serikali kuliko ningeteuliwa popote
P
Yawezekana ila Mungu akuangazie nuru za uso wake my Broo, ili upewe taasisi fulani, kwani wewe ni miongoni mwa vyombo vya thamani kwenye nchi hiyo, chombo hiki kikitumiwa kwenye uwanja mpana kitaleta manufaa kwa raia wengi zaidi na Taifa kwa ujumla, alama utakayoacha itaonekana hadi kwa walio vijijini huko Broo
 
Mkuu Emanueli misalaba , mimi hapa nilipo ni taasisi, nadhani niendelee tuu, alama zitatokea baada...
P
 
Tanzania sasa inapitia wakati muhimu sana. Sasa hivi kuna watu wachache ndiyo wameshikilia fungua za amani na katiba ya nchi yetu. Watu hao ni Rais Samia, Kinana, Mbowe, Rais Mwinyi, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Lissu na Zitto. Hawa ndiyo watu muhimu kwenye Katiba yetu ijayo

Waziri Mkuu Majaliwa ana matatizo mawili makubwa

1. Kitendo cha kuengua mpinzani wake wa uchaguzi ili apite bila kupigwa inaonesha alikuwa anapenda ule mfumo na hii imemfanya kutokuaminika kabisa na wapinzani

2. Kitendo cha kukubali hadharani kwamba alikuwa anawatumia wakina Sabaya kule kwa Mbowe kumemwaribia sana.

Kwa mwenendo wa sasa Rais Samia pamoja na Mwinyi wanahitaji viongozi wa upinzani ili waweze kupeleka taifa mbele.

Waziri mkuu bila kutafuta njia ya kutubu na kusema wazi kabadilika itabidi atolewe kwa manufaa ya umma.

Hivyo anaweza kutafutia issue kama Spika Ndugai au tu Rais kufanya mabadiliko ya kawaida au anaweza kutubu na kujirudi kitu ambacho hajafanya mpapa sasa.

Mbowe kwa sasa ana nguvu kuliko Majaliwa. Na akiweka kichwa ngumu na kujifanya ni mzalendo yatamkuta ya Ndugai.

Namshauri awahi haraka sana kuweka msimamo wake wazi bila hivyo atapigwa chini kwani hatakuwa anasaidia nchi au chama
Ramli chonganishi
 
Nyoka ni nyoka awezi kuwa samaki .ccm wanalindana wakilamba asali
mimi hata sielewi nini kinaendelea kwa sasa ???nchini kama vile tuko kwenye kampeni ya 2025,wanchi wanahitaji huduma mbalimbali kama za elimu, bado watoto wetu wanakaa chini , hakuna dawa za kutosha kwenye hospitali zetu, huduma za maji safi na salama , tatizo la ajira kwa vijana bomu kubwa, mfumo kwa bei haswa bei vyakula ,nk.lakini mjadala ni sijui lissu,PM ulafi wa madaraka ndiyo umeuteka discussion ....hichi kizazi taabu kwelikwali ...na logoff sitaki makuu...
 
mbona sie wananchi wa kawaida tunampenda tu waziri mkuu wetu, nyie anawapa tabu gani?
 
Kwa mwenendo wa sasa Rais Samia pamoja na Mwinyi wanahitaji viongozi wa upinzani ili waweze kupeleka taifa mbele.
Hili ni jambo zuri ambalo mpaka sasa Kenya wametuzidi.

Uke ugaidi unao iandama Kenya bila umoja wao wangekuwa kama Somalia
 
mjinga wewe Majaliwa ndugu yetu hanaga mambo ya 'kimamama' na mauchafu kama hao ndugu zenu.

Naomba aachwe jamaa ni wa pekee.
 
mbona sie wananchi wa kawaida tunampenda tu waziri mkuu wetu, nyie anawapa tabu gani
Wakati gwiji la siasa Tanzania mzee EDO anaachia ngazi pale mjengoni Dodoma alisema nanukuu...mheshimiwa spika nimetafakari kwa kina nakagundua kuwa tatizo ni uwaziri mkuu , leo asubuhi nimeandika barua rais naachia ngazi , mwisho wa kunukuu,, akabwaga manyanga, kile kiti ni kigumu saaana , mwombeeni PM , The guy is vey smart.....nani mwajibikaji kwa wanchi, he knows kuanzia anayeshindia mihogo mpaka anakula pizza anahitaji huduma gani .......
 
Kwa mwenendo wa sasa Rais Samia pamoja na Mwinyi wanahitaji viongozi wa upinzani ili waweze kupeleka taifa mbele.
Usimwamini binadamu kiasi hicho.... Hata wapinzani hawajiachii kiasi hicho wanajua kilichopo mbele yao...... Ccm imuhitaji mpinzani!!!!!! ....... Nachojua upinzani wanafahamu mbivu na mbichi
 
Wakati gwiji la siasa Tanzania mzee EDO anaachia ngazi pale mjengoni Dodoma alisema nanukuu...mheshimiwa spika nimetafakari kwa kina nakagundua kuwa tatizo ni uwaziri mkuu , leo asubuhi nimeandika barua rais naachia ngazi , mwisho wa kunukuu,, akabwaga manyanga, kile kiti ni kigumu saaana , mwombeeni PM , The guy is vey smart.....nani mwajibikaji kwa wanchi, he knows kuanzia anayeshindia mihogo mpaka anakula pizza anahitaji huduma gani .......
Smart? Anapita bila kupingwa?
 
Tanzania sasa inapitia wakati muhimu sana. Sasa hivi kuna watu wachache ndiyo wameshikilia fungua za amani na katiba ya nchi yetu. Watu hao ni Rais Samia, Kinana, Mbowe, Rais Mwinyi, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Lissu na Zitto. Hawa ndiyo watu muhimu kwenye Katiba yetu ijayo

Waziri Mkuu Majaliwa ana matatizo mawili makubwa

1. Kitendo cha kuengua mpinzani wake wa uchaguzi ili apite bila kupigwa inaonesha alikuwa anapenda ule mfumo na hii imemfanya kutokuaminika kabisa na wapinzani

2. Kitendo cha kukubali hadharani kwamba alikuwa anawatumia wakina Sabaya kule kwa Mbowe kumemwaribia sana.

Kwa mwenendo wa sasa Rais Samia pamoja na Mwinyi wanahitaji viongozi wa upinzani ili waweze kupeleka taifa mbele.

Waziri mkuu bila kutafuta njia ya kutubu na kusema wazi kabadilika itabidi atolewe kwa manufaa ya umma.

Hivyo anaweza kutafutia issue kama Spika Ndugai au tu Rais kufanya mabadiliko ya kawaida au anaweza kutubu na kujirudi kitu ambacho hajafanya mpapa sasa.

Mbowe kwa sasa ana nguvu kuliko Majaliwa. Na akiweka kichwa ngumu na kujifanya ni mzalendo yatamkuta ya Ndugai.

Namshauri awahi haraka sana kuweka msimamo wake wazi bila hivyo atapigwa chini kwani hatakuwa anasaidia nchi au chama
We ni schizophrenic. Majaliwa akiambiwa avunje serikali yake,haitakuwa kwa ajili ya Mbowe.
 
Kwani waliokuwa kwa Magufuli hawakuwa na chuki kwenye kipindi chao ?
Naona chadema sio chama Cha kuwakimboa wananchi Tena ,ni chama chakulipiza YOYOTE alikuwa awamu ya tano,SS wananchi ambao tuliokuwa tunakuamini Sasa kinatutia mashaka
 
Back
Top Bottom