Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Fatah na Hamasi ni mahasimu wa kisiasa wa kihistoria. Yote yanayotokea huko hususani Ghaza kwa kiasi kikubwa ni matokeo ya mgawanyiko uliopo baina yao wenyewe. Ni ngumu sana kupata suluhu ya mgogoro huu japo inawezekana. Hivi inawezekanaje, Ukingo wa Magharibi (west bank)kuna serikali yake inayoongozwa na Fatah chini ya Mahmud Abas na kule Ghaza kuna serikali yake inayoongozwa na Hamasi chini ya Ismail Hanniyeh. Na kila upande una mawaziri wake.
Ni nani baina ya mahasimu hawa waawili anawakilisha maslahi mapana ya wa Palestine wote?
Mgawanyiko miongoni mwa Jumuiya za kimataifa, na mataifa duniani yanakoleza moto wa mgawanyiko kwenye mgogoro huu, kwa wao kuchagua upande miongoni mwa mahasimu hawa na kuwafadhili kwa hali na mali, hali ambayo inakoleza uhasama, vita, mauaji na kurefusha zaidi upatikanaji wa suluhu ya kudumu katika eneo hili muhimu la mashariki ya kati.
Uvamizi na uchokozi wa Hamasi dhidi ya Israel hivi karibuni ni matokeo ya ufadhili wa mataifa ya ulimwengu na kuchagua upande miongoni mwa mahasimu hawa yaani Hamas na Fatah.
Bila kwanza kuwaweka chini na kuwapatanisha Hamasi na Fataha, ni ndoto kuwa na Taifa la Palestine, ispokua Taifa la Ghaza na Taifa la Ukingo wa Magharibi.
Wasalam...